18/12/2023
Weekend hii tulikuwa Mbeya Kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam.
Mchezo ulimalizika kwa ushindi wa penati 6 kwa 5 na tukafanikiwa kufuzu hatua inayofuata.
Weekend hii tunawakabili Mapinduzi katika muendelezo wa michezo ya First League katika Uwanja wa Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi
29/11/2023
Our Team Our Family TRA Kilimanjaro FC "Moshi Warriors "
Kigoma we are Coming Very Soon..
24/11/2023
Jumamosi Hii November 25 mwaka ni Zamu yetu tena kutoa burudani ya kiwango Toshelevu!
Kwa Uchakavu wa Shilingi 2000 tu unafurahia burudani ndani ya dimba la Chuo Kikuu cha Ushirika.
12/11/2023
Baada ya kupoteza mchezo uliopita leo tumeshinda ugenini mabao Matatu kwa Sifuri dhidi ya Kurugenzi .
Inaendelea
27/10/2023
Operations Point 3 Inaendelea tena kesho katika Dimba la Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi Dhidi ya Tanesco.
23/10/2023
Timu yetu ya TRA Kilimanjaro FC " Moshi Warriors " Imeanza Safari ya Matumani Makubwa kuelekea Championship.
Ni baada ya kuibuka na ushindi wa bao mbili kwa sifuri dhidi ya Alliance FC kutoka Mwanza.
Sasa iko chimbo ikijiandaa na mchezo Mwingine Jumamosi hii dhidi ya Tanesco FC katika dimba la Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
.
18/10/2023
Jumamosi hii 21.10. Mwaka huu saa kumi kamili jioni katika dimba la Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kutakuwa na Mchezo mzuri Sana.
TRA Kilimanjaro FC " Moshi Warriors " Fahari ya Kilimanjaro wataikaribisha Klabu Soka ya Alliance kutoka mwanza ukiwa ni mchezo wa kwanza katika muendelezo wa michezo ya ligi ya kwanza ( First League) msimu huu wa 2023/2024.
Ewe Mkazi wa Kilimanjaro na Kaskazini kwa ujumla. Tenga Shilingi 2000 tu kwa Ajili ya Kiingilio chako uje kushuhudia mtanange huu maridhawa kabisa.
14/10/2023
TAARIFA
Kesho Jumapili 15.10.2023 kutakuwa na mchezo wa kirafiki utakaowakutanisha TRA Kilimanjaro FC iliopo First League dhidi ya Polisi Tanzania iliopo Championship katika Dimba la Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi Saa kumi kamili jioni.
Huu ni mchezo mzuri na muhimu kuelekea mchezo wa kwanza wa kimashindano kwa TRA Kilimanjaro FC utakopigwa October 21 mwaka huu saa kumi kamili jioni katika dimba hilohilo la Ushirika dhidi ya Klabu Soka ya Alliance Kutoka Mwanza.
Kiingilio cha mchezo huo ni Shilingi Elfu moja tu!
Imetolewa Na Idara Ya Habari
TRA Kilimanjaro FC.