Sports Attack

Sports Attack

Share

Page hii ni Kwaajili ya taarifa za kimichezo ndani na nje ya Tanzania �

08/07/2026

Zaidi ya wabunge 30 wa Bunge la Ulaya wameunga mkono barua inayoitaka Kamati ya Maadili ya FIFA kumchunguza Rais wa FIFA, .

Mambo muhimu:

Wabunge hao wanataka kufanyika uchunguzi wa maadili ili kubaini k**a mawasiliano ya Infantino na Donald Trump's kuhusu kusimamishwa kwa Balogun yalikiuka kanuni za FIFA zinazotaka kutokuwepo kwa ushawishi wa kisiasa.

Mjadala huu umeibuka baada ya FIFA kubatilisha adhabu ya kadi nyekundu ya Balogun, jambo lililomruhusu kucheza mechi iliyofuata ya Kombe la Dunia ya Marekani, kufuatia taarifa kwamba Trump aliwasiliana na Infantino.

Wabunge hao wanasema tukio hilo limeathiri imani ya umma kuhusu uhuru wa FIFA, na wanataka kuwepo kwa uwazi kamili kuhusu jinsi uamuzi huo ulivyofikiwa.

• Infantino amekanusha kuwepo kwa ushawishi wa kisiasa, akisisitiza kwamba uamuzi huo ulifanywa kwa kujitegemea kwa kuzingatia taratibu za kinidhamu za FIFA.

(Chanzo: ABC, ESPN na Euronews)

08/07/2026

RASMI SASA

Shirikisho la soka la nchini Misri limewasilisha rasmi malalamiko likidai uchunguzi ufanyike kuhusu maamuzi ya waamuzi katika kipigo chao dhidi ya Argentina kwenye Kombe la Dunia

Rais Hany Abo Rida ameamua kuchukua hatua dhidi ya mwamuzi wa Ufaransa François Letexier pamoja na wasaidizi wake akiomba timu ya waamuzi wa Ufaransa iondolewe katika mechi zilizobaki za mashindano kutokana na makosa yao makubwa yaliyoathiri mchezo.

08/07/2026

UTATA JUU YA UTATA

Homa ya malalamiko dhidi ya ushindi wa utata wa Argentina wa mabao 3-2 dhidi ya Misri imezidi kupanda baada ya nguli wa soka wa Ufaransa, Thierry Henry, kulipuka na kuponda maamuzi ya mwamuzi yaliyowanyima Farao goli lao la pili. Henry ameweka wazi kuwa uamuzi huo wa kufuta goli la Misri kwa madai ya madhambi madogo dhidi ya beki Lisandro Martínez haukuwa wa haki na uliharibu kabisa taswira ya mchezo huo wa hatua ya 16 bora.

​Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal na Barcelona ameshindwa kuficha hisia zake akidai kuwa kile kilichotokea uwanjani ni unyang'anyi wa mchana kweupe dhidi ya wanyonge. "Sasa hapa imepita kiasi cha aibu. Misri, Afrika, na ulimwengu mzima wa soka wameibiwa. Lile lilikuwa goli muhimu sana katika mchezo huu. Mwamuzi alifanya uamuzi mbaya na wa hovyo sana," alisema Henry akionyesha kukasirishwa na kiwango cha uamuzi kilichoathiri matokeo.

​Henry ameenda mbali zaidi kwa kutoa shinikizo kwa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) akitaka kutoa majibu ya kuridhisha kwa wadau wa soka k**a mashindano hayo yataendelea kuonekana yana mbebeo maalum. Alihitimisha kwa kusema, "FIFA itabidi iuambie ulimwengu wa soka na kutoa maelezo k**a Argentina itashinda mchezo huu," kauli inayoungana na mfululizo wa lawama kutoka kwa magwiji wengine k**a Didier Drogba na José Mourinho kuhusu upendeleo unaodaiwa kufanywa ili kuwabakiza mabingwa watetezi mashindanoni.

08/07/2026

MBAPPÉ AMJIBU VIKALI SENETA WA PARAGUAY BAADA YA KAULI ZA KIBAGUZI

Baada ya Ufaransa kuiondoa Paraguay katika Kombe la Dunia, seneta wa Paraguay, Celeste Amarilla, alizua mjadala mkubwa kwa kutoa kauli zilizotajwa kuwa za kibaguzi dhidi ya nyota wa Ufaransa, Kylian Mbappé. Amarilla alimshambulia Mbappé kwa kumtaja k**a "Mkameruni aliyekoloniwa anayejifanya Mfaransa", pamoja na kauli nyingine zilizolaaniwa na wengi duniani.

Leo, Mbappé alivunja ukimya kupitia mitandao yake ya kijamii na kutoa ujumbe mkali wa kupinga ubaguzi wa rangi:

🗣️ "Bi Celeste Amarilla, wewe ni mwanamke wa kudharaulika na hustahili kabisa nafasi uliyonayo.

Huwawakilishi wananchi wa Paraguay, taifa ambalo limeonyesha moyo, jasho na heshima kubwa katika mashindano haya.

Kutokana na kauli zako za wazi za kibaguzi, dunia sasa imeanza kusahau safari ya kihistoria ya Paraguay katika Kombe hili la Dunia na badala yake imebaki ikiona taswira mbaya unayoipa nchi yako mbele ya ulimwengu.

Sitawahi kuruhusu watu k**a wewe wapate uhuru wa kueneza chuki na ubaguzi wa rangi duniani."

Kauli hiyo ya Mbappé imepokelewa kwa pongezi na mashabiki wengi, wakieleza kuwa ameonyesha msimamo thabiti dhidi ya ubaguzi wa rangi na kutetea utu wa binadamu.

Soka linaweza kututenganisha kwa ushindani, lakini heshima, usawa na utu vinapaswa kutuunganisha daima.

07/07/2026

Kocha nguli wa soka duniani, José Mourinho, amebatiza mchezo wa ushindi wa mabao 3-2 wa Argentina dhidi ya Misri kuwa ni "filamu iliyoandaliwa matokeo tangu mwanzo," akilalamikia vikli maamuzi ya marefa na chumba cha VAR yaliyowaumiza Farao hao wa Misri. Mourinho amefunguka kwa hisia kali akidai kuwa mchezo huo haukuwa wa haki na kwamba Misri haikupoteza kwa sababu ya soka, bali kwa sababu ya "script" (maandishi) ya mashindano hayo yanayobeba upendeleo kwa upande mmoja.

​Katika uchambuzi wake, Mourinho alifafanua jinsi maamuzi kadhaa ya utata yalivyopindua mchezo huo ambao Misri iliongoza kwa mabao 2-0 mapema, akitolea mfano pale nahodha Mohamed Salah aliponyimwa faida ya kufunga goli, huku beki Cristian Romero akifanya madhambi mabaya yaliyotaka "kuuvunja mguu wa Salah vipande viwili" bila kupewa kadi yoyote. Zaidi ya hayo, alilalamikia VAR kurudisha nyuma mchezo "hadi zama za mawe" ili tu kutafuta kisingizio chochote cha kufuta goli la Misri, sambamba na kunyimwa penati ya wazi ya dakika ya 93 baada ya Salah kuangushwa ndani ya boksi.

​Tukio hilo la mwisho lilitoa mwanya kwa Argentina kufanya shambulizi la kushtukiza lililomwezesha Enzo Fernández kufunga bao la ushindi, jambo lililomfanya Mourinho kuhitimisha kwa hasira: "Unapocheza dhidi ya hii timu ya Argentina, kuwa mbele kwa mabao 2-0 haitoshi, kwa sababu haujaribu tu kuwafunga wanaume 11 uwanjani. Unajaribu kuishinda filimbi. Unajaribu kuishinda chumba cha VAR. Unajaribu kushinda 'script' nzima ya mashindano. Huu sio mpira wa miguu tena. Ni filamu, na mwisho wake umeshapangwa kabla hata wachezaji hawajatoka kwenye koridoro kuelekea uwanjani."

07/07/2026

AMERIKA KUSINI SAFARI HII WAKO VIBAYA SANA.
Yaani kwa kifupi Amerika Kusini wajipange tena

07/07/2026
07/07/2026

ROBO FAINALI SASA

07/07/2026

Uswiss 3
Colombia 2

07/07/2026

Colombia wanakosa Tena penati nyingine hapa

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Mbeya?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address


Uyole
Mbeya