Sports Arena

Sports Arena

Share

🏟️ Official Page of Sports Arena
📍 Dar es Salaam, Tanzania.
⚽ Habari • Matokeo • Usajili • Uchambuzi

08/08/2026

KUNA TOFAUTI KUBWA KATI YA SIMBA OYEEH NA YANGA BINGWA
😂😂😂

Photos from Sports Arena's post 06/08/2026

A au B unaenda na ipi hapa….?🤔

06/08/2026

Mmhh..!!👀

Photos from Sports Arena's post 06/08/2026

U*i wa Young Africans kwaajili ya msimu ujao wa 2026-27

Je, unaupa asilimia ngapi kati ya 100….?

03/08/2026

LITAKUFA JITU..!!

Peter Shalulile ndani ya U*i wa Yanga SC🔥

03/08/2026

Kuna muda najiuliza huu mgogoro wa Simba ulioibuka ghafla chanzo chake ni nini? au hawa wazee walikua serious nini? Yani sielewi imekuwaje ghafla.

02/08/2026

Je, Fred Duval Ngoma Ameishusha Daraja Olympique de Safi?

Takwimu Zinasemaje?

Baada ya taarifa za Fred Duval Ngoma kuhusishwa na kuondoka Olympique de Safi, kumekuwa na mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa soka, huku baadhi wakihitimisha haraka kuwa kiungo huyo ndiye aliyesababisha timu hiyo kushuka daraja. Lakini je, takwimu zinaunga mkono hitimisho hilo?

Msimu uliopita, Ngoma alikuwa mmoja wa wachezaji waliotegemewa zaidi na Olympique de Safi. Kati ya mechi 30 za ligi kuu ya Morocco, alicheza mechi 27 na alianza kikosi cha kwanza katika mechi 24. Kwa jumla alitumia dakika 2,139 uwanjani, jambo linaloonyesha kuwa alikuwa sehemu muhimu ya mipango ya benchi la ufundi.

Kiufundi, Ngoma anajulikana kwa uwezo wake wa kucheza nafasi ya single pivot katika mfumo wa 4-1-4-1. Ana sifa ya kukaba vizuri eneo la kiungo na kuanzisha mashambulizi kupitia pasi za mbele. Ndiyo maana mara nyingi kocha Mounir Jaouani alimwamini acheze peke yake mbele ya mabeki badala ya kutumia mfumo wa double pivot, huku kiungo Ayman Ouhatti akibaki benchi.

Hata hivyo, jukumu hilo kubwa lilimaanisha Ngoma alibeba mzigo mkubwa wa kuzuia mashambulizi na kuunganisha safu ya ulinzi na ushambuliaji. Mashabiki wengi wa Olympique de Safi waliamini kocha alikuwa amempa majukumu mengi kupita kiasi, hali iliyomfanya aonekane k**a chanzo cha matatizo ya timu wakati changamoto zilikuwa pana zaidi.

Kwa upande wa matokeo ya timu, Olympique de Safi ilimaliza msimu katika nafasi ya 16 ikiwa na alama 22 pekee. Katika mechi 30, ilishinda mechi 3 tu, ikatoa sare 13 na kupoteza mechi 14. Safu ya ulinzi iliruhusu mabao 52 huku timu ikifunga mabao 24 pekee. Takwimu hizi zinaonyesha matatizo ya timu yalikuwa katika maeneo mengi, si kwa kiungo mmoja pekee.

Ndiyo maana ni vigumu kutumia takwimu hizi pekee kumhukumu Ngoma. Katika soka, mafanikio au kushuka kwa timu mara nyingi hutokana na mkusanyiko wa sababu mbalimbali, ikiwemo ubora wa kikosi kizima, mbinu za kocha na kiwango cha washambuliaji pamoja na mabeki.

Historia pia imeshawahi kutoa mifano ya wachezaji waliokuja na rekodi nzuri lakini wakashindwa kufanya vizuri baada ya kuhamia klabu nyingine. Mfano ni Musa Balla Conte, ambaye alisajiliwa na Yanga kutoka Sfaxien kwa ada kubwa baada ya kuwa na msimu mzuri, lakini hakufikia matarajio ya wengi.

Kwa mantiki hiyo, hukumu kuhusu Fred Duval Ngoma inapaswa kusubiri mpaka aonekane katika mazingira mapya na mfumo tofauti wa uchezaji. Kumtangaza kuwa ndiye sababu ya kushuka daraja kwa Olympique de Safi kunaweza kuwa hitimisho la haraka lisilozingatia taswira nzima ya msimu wa timu hiyo.

01/08/2026

FRED NGOMA ni Kiungo Mpya wa Yanga SC✅

01/08/2026

JEZI HUZUA MJADALA, LAKINI MAFANIKIO UWANJANI HUJENGWA NA KIKOSI.

Kila msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unapokaribia, moja ya mijadala mikubwa huanzia kwenye uzinduzi wa jezi za timu. Mashabiki hugawanyika katika makundi mawili; wanaosifia jezi za timu yao na wanaozikosoa za wapinzani wao.

Ukiwauliza Dominic Salamba na Ibrahim Ambokile, huenda wakakuambia jezi ya kijani ndiyo bora zaidi. Ukiwauliza Farhan Kihamu na Wilson Oruma, nao watasisitiza kuwa jezi nyekundu ndiyo yenye mvuto wa kipekee.

Lakini ukweli ni kwamba kila shabiki anaona uzuri zaidi kwenye rangi na nembo ya timu anayoishabikia. Hata katika soka la kimataifa, mashabiki wa Arsenal hujisifia jezi zao kila msimu, lakini ni nadra kumuona shabiki wa Chelsea akinunua jezi ya Arsenal. Vivyo hivyo kwa Tanzania, shabiki wa Simba si rahisi kusema jezi ya Yanga ni nzuri, na shabiki wa Yanga naye si rahisi kuisifu jezi ya Simba.

Hata hivyo, tofauti za maoni hazijawahi kuzuia jezi za klabu zote mbili kuendelea kuvaliwa na maelfu ya mashabiki kila siku. Kila mmoja hununua, huvaa na kujivunia jezi ya timu yake bila kujali maoni ya upande wa pili.

Kinachopaswa kupewa uzito zaidi si muonekano wa jezi, bali ubora wa kikosi. Jezi nzuri haziwezi kufanya pressing, kupiga pasi sahihi, kufunga mabao wala kuzuia mpira usiingie wavuni. Matokeo uwanjani huamuliwa na maandalizi mazuri, ubora wa wachezaji, benchi la ufundi na uwekezaji sahihi katika timu.

Kwa hiyo, wakati mashabiki wakiendelea kufurahia uzinduzi wa jezi mpya, viongozi wa klabu wanapaswa kuelekeza nguvu zaidi katika kujenga vikosi imara vitakavyoshindania mataji. Mwisho wa siku, historia hukumbuka mabingwa na makombe waliyochukua, si uzuri wa jezi walizovaa.

Jengeni timu; jezi ni utambulisho, lakini mafanikio huamuliwa uwanjani.

01/08/2026

Kwanini simba wamesusia kufanya promo ya Jezi za Msimu huu…?🤔

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Masaki?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


Masaki