Global Foot

Global Foot

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Global Foot, Sports Event, Osofia, Kigoma.

Msafiri Sports Hub | Taarifa Moto za Michezo
⚽️ Habari, Matokeo & Takwimu
🌍 EPL | La Liga | Serie A | Bundesliga | Ligue 1 | NBC
🔥 Hashtags #MsafiriSports #FootballUpdates
📲 Matukio Mubashara & Uchambuzi

KWA MATANGAZO KARIBU
PIGA 0756170880

03/07/2026

Yanga wanatakiwa kulipa kiasi cha milioni 100 kwa makosa ya kutumia nyumba pembezoni mwa uwanja badala yake vyumba vya kubadilishia nguo. Pia viongozi wao wamepelekwa k**ati ya maadili.

Swali langu ni je hakuna sheria au kiwango kilichowekwa ajili ya makosa k**a hayo?
Au tu ni kile ambacho k**ati itaamua kilipwe?

28/06/2026

Mwamba alipitia vipingamizi vingi alipokuwa ligi ya bongo wengine walienda mbali kabisa mpaka kumlinganisha na kina George Mpole na wengine hadi kuchangisha pesa ili kupambana naye.

Bart against all odds Mayele huyooo kombe la dunia na bao kaweka tena bao la kikatili kabisa ambalo lililipa Congo nguvu ya kuendelea mbele Kabla Yoane Wissa kuweka goli la tatu...

Photos from Global Foot's post 28/06/2026

🚨🇨🇻 TETESI MPYA: Nahodha wa timu ya taifa ya Cape Verde national football team, Ryan Mendes, anachunguzwa kufuatia tuhuma za ubakaji.

Kwa mujibu wa mwanamke mmoja, aliambia polisi wa New Zealand kuwa Mendes anadaiwa kumbaka katika hoteli moja wakati timu ya Cape Verde ilipokuwa nchini humo kwa mechi ya kirafiki mjini Auckland mwezi Machi 2026.

Mwanamke huyo baadaye aliiandikia FIFA pamoja na Cape Verde Football Federation akiomba Mendes aondolewe kwenye michuano ya Kombe la Dunia, lakini anadai hakupata majibu yoyote.

Inaripotiwa kuwa Shirikisho la Soka la Cape Verde lilisema suala hilo ni la binafsi linalomhusu Mendes.

28/06/2026

Vinara wa mabao kombe la dunia 2026 : ⚽️

⚽️⚽️⚽️⚽️⚽️⚽️
🇦🇷 Lionel Messi — 6

⚽️⚽️⚽️⚽️
🇫🇷 Ousmane Dembélé — 4
🇫🇷 Kylian Mbappé — 4
🇳🇴 Erling Haaland — 4
🇧🇷 Vinícius Júnior — 4

⚽️⚽️⚽️
🇳🇱 Brian Brobbey — 3
🇧🇷 Matheus Cunha — 3
🇨🇦 Jonathan David — 3
🇳🇿 Elijah Just — 3
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Harry Kane — 3
🇨🇭 Johan Manzambi — 3
🇲🇦 Ismael Saibari — 3
🇸🇳 Ismaïla Sarr — 3
🇩🇪 Deniz Undav — 3
🇨🇩 Yoane Wissa — 3

28/06/2026

🚨🚨 OFFICIAL: Timu 16 ambazo zimeondolewa hatua ya makundi kwenye kombe la dunia ❌

🇸🇦 Saudi Arabia
🇰🇷 South Korea
🇨🇼 Curaçao
🏴󠁧󠁢󠁳󠁣󠁴󠁿 Scotland
🇭🇹 Haiti
🇮🇶 Iraq
🇮🇷 Iran
🇯🇴 Jordan
🇳🇿 New Zealand
🇺🇿 Uzbekistan
🇵🇦 Panama
🇶🇦 Qatar
🇨🇿 Czech Republic
🇹🇳 Tunisia
🇹🇷 Türkiye
🇺🇾 Uruguay

28/06/2026

Lionel Messi alipomgusa moyo mtoto mdogo kwa zawadi isiyosahaulika. 🩵

Akiwa na umri wa miaka 5 tu, Murtaza Ahmadi kutoka Ghazni, Afghanistan aligusa mioyo ya watu duniani baada ya picha zake kusambaa akiwa amevaa jezi ya Messi aliyojitengenezea kwa mfuko wa plastiki wa rangi ya bluu na nyeupe.

Kaka yake ndiye aliyemtengenezea jezi hiyo, kwa sababu baba yao hakuwa na uwezo wa kumnunulia jezi halisi ya Messi.

Habari hiyo ilipomfikia Messi, kwa kushirikiana na UNICEF, alimpelekea Murtaza jezi mbili zenye saini yake pamoja na mpira wa miguu.

Na k**a hiyo haikutosha, baadaye mwaka huo ndoto ya Murtaza ilitimia alipata nafasi ya kukutana uso kwa uso na Messi, akiwa mmoja wa watoto waliomsindikiza uwanjani kabla ya mechi ya FC Barcelona kuanza. 🥹❤️

11/06/2026

🚨 KOMBE LA DUNIA 2026 LINAANZA LEO, LAKINI KUNA MAMBO YANAYOIBUA MASWALI MAKUBWA! 🌍⚽

Wakati dunia ikisubiri kwa hamu mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia 2026, matukio kadhaa ya kushangaza na yenye utata yameripotiwa siku chache zilizopita:

🇨🇭 Mshambuliaji wa Uswisi, Embolo, alichelewa kujiunga na timu kutokana na matatizo ya visa.

🇮🇶 Nyota wa Iraq, Aymen Hussein, alihojiwa kwa karibu saa 7 baada ya kuwasili nchini Marekani.

🇮🇷 Iran ilikumbwa na changamoto kubwa za visa, huku wajumbe wao 15 wakinyimwa vibali vya kuingia.

🇸🇴 Omar Artan wa Somalia, aliyeshinda tuzo ya Mwamuzi Bora wa Afrika 2025 kutoka CAF, alinyimwa ruhusa kuingia Marekani na hivyo kuukosa mashindano hayo.

🇿🇦 Wajumbe wa Afrika Kusini uliwasili kwa kuchelewa baada ya baadhi ya wanachama kushindwa kupata visa kwa wakati.

🇸🇳 Baadhi ya maafisa wa Senegal walifanyiwa ukaguzi mkali wa usalama, wakalazimishwa kuvua viatu, jambo lililosababisha madai ya ubaguzi.

🇺🇿 Timu ya Uzbekistan ilikaguliwa kwa kutumia mbwa wa kunusa mabomu, huku video za tukio hilo zikisambaa duniani kote.

🏴󠁧󠁢󠁳󠁣󠁴󠁿 Baadhi ya mashabiki wa Scotland walifutiwa vibali vya ESTA siku chache kabla ya safari zao.

💸 Mashabiki wengi waliokuwa tayari wamenunua tiketi na kuweka nafasi za hoteli walikataliwa visa, na hivyo kupoteza fedha nyingi sana.

👇 Wewe unaonaje?
Kombe la Dunia linapaswa kuunganisha watu wote bila vikwazo, au usalama wa nchi mwenyeji unapaswa kupewa kipaumbele hata k**a wengine wataathirika?

🔥 Je, haya ni matukio ya kawaida au kuna jambo kubwa zaidi linaendelea nyuma ya pazia? 👇⚽🌍

26/05/2026

Kuna nini kinaendelea hapa...

25/05/2026

Real Madrid walimwacha Samuel Eto’o akiwa na miaka 16 peke yake kabisa kwenye uwanja wa ndege wa Barajas, Madrid.
Hakukuwa na kiongozi wa klabu wa kumpokea.
Hakukuwa na mtafsiri.
Hakukuwa hata na gari la kumchukua.

Alikuwa ni kijana mdogo kutoka Cameroon, mwenye ndoto ya soka na hakuwa hata anajua aende wapi.
Mtu mmoja aliyekuwa anafanya kazi ya usafi usiku barabarani — Mwafrika mwenzake — alimwona akiwa amepotea, akamsubiri na kumpeleka mwenyewe hadi kwenye uwanja wa mazoezi wa Real Madrid. Mpaka leo Eto’o bado ana mawasiliano na huyo mtu.

Na hicho ndicho kilikuwa “ukaribisho” wake Madrid.
Badala ya kupewa nafasi, Real Madrid wakamzungusha kwa mikopo Leganés, Espanyol na Mallorca. Hakuna imani. Hakuna nafasi ya kweli ya kuonyesha uwezo wake.

Mwaka 2000, baada ya tayari kushinda medali ya dhahabu ya Olimpiki na AFCON akiwa bado mdogo, Madrid wakamuuza kwa pauni milioni 4.4 tu.

Akiwa Mallorca ndipo dunia ilianza kumuona Samuel Eto’o halisi.
Magoli 70.
Mfungaji bora wa klabu.
Mchezaji Bora wa Afrika mara mbili.
Florentino Pérez alipojaribu kumrudisha Madrid… Alikuwa tayari amechelewa.

Barcelona wakamnunua kwa euro milioni 24 — karibu mara tano ya fedha ambazo Madrid walimuuza.
Na Eto’o hakusahau alivyopuuzwa.

Mwaka 2005 Barcelona walipotwaa La Liga, Eto’o alisimama Camp Nou mbele ya mashabiki 98,000 na kuongoza nyimbo za kubeza Madrid:
“Madrid bastards, salute the champions!”
Alipigwa faini ya euro 12,000.
Lakini kwake haikuwa pesa — ilikuwa ni kisasi cha heshima yake.

Baadaye akaenda kufunga kwenye fainali tatu tofauti za UEFA Champions League na kuweka historia kwa kushinda trebles mbili mfululizo akiwa na klabu mbili tofauti — jambo ambalo hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kufanya.

Yote haya… yalianza siku ambayo Real Madrid walishindwa hata kutuma gari la kumfuata kijana mmoja kutoka Cameroon.

Na hapo ndipo Historia ya mpira ilibadilika milele. 👀🔥

12/05/2026

Wakala wa FIFA kutoka nchini Uganda, Ronnie Santos Mwine Fred ameripoti kuwa, Maskauti wa vigogo wa 🇹🇷Uturuki Fenerbahçe SK wamekuwa 🇹🇿Tanzania kwa siku ya 4 sasa, na sababu pekee ni nyota kijana wa timu ya taifa ya 🇺🇬Uganda "The Cranes" Allan Okello!
Na Watamfuatilia tena katika mchezo ujao dhidi ya Dodoma Jiji.

Katika mechi ya kwanza waliyomtazama, alifunga mabao 2 na kutoa assist 1 dhidi ya Coastal Union

Young Africans S.C. wanatajwa kuhitaji takribani dola milioni 3 (Tsh 7.8B) kwa nyota huyo wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Kigoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address


Osofia
Kigoma
ELKAKA