Flowin vitus

Flowin vitus

Share

Journalist, Newswriter &Reporter, RedioPresenter &GraphicDesigner, DigitalContentCreator

13/08/2026

Afisa lishe wa Hospitali ya Rufaa mkoani Iringa Pendo Yaredi, amesema ukiaachana na mtu aliyefikisha umri wa miaka 18 kutambulika k**a mtu mzima mama ambaye amekidhi vigezo vya kunyonyesha ni yule yupo kwenye umri wa uzazi.

Katika maelezo yake Yaredi amesema kwa mujibu wa tafiti za kisayansi ni kwamba mama aliyekidhi umri wa uzazi anaanzia umri wa miaka 15 mpaka miaka 49, ukiachana na ile mitazamo ya kuwa mtu mzima ni yule aliyetimita miaka 18.

13/08/2026

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kiwa Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Caroline Levitt, atajiuzulu wadhifa huo mwishoni mwa mwezi huu.

Katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii Trump amesema kwamba Levitt anaondoka kwenye nafasi hiyo ili kutumia muda zaidi na watoto wake wadogo pamoja na familia yake, akisema kuwa anaelewa na kuheshimu uamuzi huo kikamilifu.

Trump amemtaja Caroline Levitt kuwa miongoni mwa wasaidizi wake anaowaamini zaidi.

Aidha, Trump ameongeza kuwa Levitt sasa atakuwa mmoja wa washauri wake muhimu wa nje ya serikali na ataendelea kuwa sauti yenye ushawishi ndani ya Chama cha Republican.

Levitt, mwenye umri wa miaka 28, aliteuliwa kuwa msemaji wa Ikulu mwaka jana na kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kushika wadhifa huo.

13/08/2026

Khoudia Diop, mwanamitindo wa Senegal anayejulikana duniani k**a “Melanin Goddess,” amepata umaarufu mkubwa kutokana na rangi yake ya ngozi nyeusi yenye mvuto wa kipekee.

Gazeti la mitindo na Urembo la The Glamour liliwahi kumuweka Melanin kwenye orodha ya mabinti warembo Afrika kufuatia muonekano wake wa asili.

Safari yake katika ulimwengu wa mitindo imemsaidia kupinga mitazamo ya zamani kuhusu viwango vya urembo na kuonyesha umuhimu wa kuwapa nafasi watu wenye rangi mbalimbali za ngozi katika tasnia ya fashion.

Mara kadhaa Diop amekuwa akitajwa k**a mwanamke mwenye mwanamvuto wa kipekee kutokana na ngozi yake ya asili inayovutia macho ya watu wengi duniani. Pia ametumia umaarufu wake kuhamasisha watu, hasa vijana wa Afrika, kujikubali, kujiamini na kujivunia mwonekano wao wa asili.

Photos from Flowin vitus's post 13/08/2026

Hii hapa list ya wachezaji waliocheza timu moja katika maisha yao ya soka............

Nani anaongezeja kwenye list...?

13/08/2026

Mashetani wekundu Manchester United wametwaa Kombe la pili kwenye pre-season baada ya kubeba Kombe la BoyleSports Cup kufuatia ushindi wa 5-4 wa mikwaju ya penalti dhidi ya Leeds United ambapo mchezo ulitamatika kwa sare ya 1-1.

FT: Man United 1️⃣-1️⃣ Leeds United (P 5-4)
⚽ Zirkzee 16'
⚽ Aaronson 29'

12/08/2026

Kwa mujibu wa kocha mkuu wa klabu ya Simba SC Steve Barker ni kwamba “Dirisha bado liko wazi mpaka lifungwe bado tuna muda na lolote linaweza kutokea ndani ya muda uliobaki k**a kuongeza Mchezaji mwingine”

12/08/2026

Klabu ya Chelsea imeweka Ijumaa saa 11:00 jioni kwa saa za Uingereza kuwa muda wa mwisho wa Manchester City kukamilisha dili la kumsajili kiungo Muargentina Enzo Fernández kufuatia hitaji la kocha Maresca akitaka kumtumia nyota huyo.

Ikumbukwe Manchester City imekuwa kwenye mazungumzo na wawakilishi wa Enzo kwa siku kadhaa, lakini kwa upande wake Chelsea imeweka msimamo wazi kuwa inataka ada ya £120 milioni, pamoja na masharti ya malipo ambayo tayari yamewasilishwa kwa City.

Katika kutilia mkazo Chelsea imesisitiza kuwa ikiwa £120 milioni hazitalipwa kabla ya Ijumaa saa 5:00 usiku, Enzo hataruhusiwa kujiunga na Manchester City msimu huu ikiongezwa kuwa hakuna punguzo katika mauzo ya nyota huyo.

12/08/2026

(🏟 New Amaan Complex)

FT: Yanga SC 1️⃣-0️⃣ Simba SC
⚽️ Kangwanda 32'

12/08/2026



HT: Yanga SC 1-0 Simba SC

⚽️ Kangwanda 32'

12/08/2026

Kikubwa halikosekani tukio...........

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Iringa?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Iringa