VETA

VETA

Share

This is an official account for the Vocational Education and Training Authority (VETA).

20/08/2026
Watu wenye ulemavu wanaotaka kupata ujuzi wa ufundi stadi sasa wana fursa ya kusoma bila kulipa karo katika vyuo vya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), baada ya Mamlaka kuweka utaratibu wa kugharamia karo zao.

Meneja Uhusiano na Masoko wa VETA, Sitta Peter, amesema utaratibu huo ulianza mwaka 2025 na unalenga kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata fursa sawa ya kupata ujuzi, kujiajiri au kuajiriwa.

Akizungumza katika Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayoendelea mkoani Tanga, Sitta amesema waombaji wenye ulemavu wanapaswa kufanya maombi na kufuata taratibu za udahili katika vyuo vya VETA, huku karo zao zikilipwa na Mamlaka.

Amesema wanafunzi hao wataendelea kugharamia mahitaji yao binafsi kulingana na mazingira ya mafunzo, ikiwemo usafiri kwa wanaosoma kutwa au mahitaji binafsi kwa wanaoishi bweni.

Sitta amesema fursa za mafunzo ya VETA zinapatikana kwa Watanzania wenye viwango mbalimbali vya elimu, kuanzia waliomaliza elimu ya msingi hadi wenye shahada na shahada za uzamili, huku kila mmoja akiwa na fursa ya kuchagua stadi inayoweza kumsaidia katika ajira au kujiajiri.

Aidha, amesema VETA inaendelea kutekeleza Mradi wa Elimu na Stadi kwa Ajira zenye Tija Awamu ya Pili (ESPJ II), unaolenga kuanzisha vituo 15 vya umahiri katika maeneo mbalimbali ya mafunzo ya ufundi stadi.

Amesema vituo hivyo vitaongeza ubora wa mafunzo na kuwaandaa wahitimu wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira, ikiwemo fursa za ajira nje ya Tanzania kupitia vyeti vya kimataifa. 20/08/2026

Watu wenye ulemavu wanaotaka kupata ujuzi wa ufundi stadi sasa wana fursa ya kusoma bila kulipa karo katika vyuo vya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), baada ya Mamlaka kuweka utaratibu wa kugharamia karo zao. Meneja Uhusiano na Masoko wa VETA, Sitta Peter, amesema utaratibu huo ulianza mwaka 2025 na unalenga kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata fursa sawa ya kupata ujuzi, kujiajiri au kuajiriwa. Akizungumza katika Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu inayoendelea mkoani Tanga, Sitta amesema waombaji wenye ulemavu wanapaswa kufanya maombi na kufuata taratibu za udahili katika vyuo vya VETA, huku karo zao zikilipwa na Mamlaka. Amesema wanafunzi hao wataendelea kugharamia mahitaji yao binafsi kulingana na mazingira ya mafunzo, ikiwemo usafiri kwa wanaosoma kutwa au mahitaji binafsi kwa wanaoishi bweni. Sitta amesema fursa za mafunzo ya VETA zinapatikana kwa Watanzania wenye viwango mbalimbali vya elimu, kuanzia waliomaliza elimu ya msingi hadi wenye shahada na shahada za uzamili, huku kila mmoja akiwa na fursa ya kuchagua stadi inayoweza kumsaidia katika ajira au kujiajiri. Aidha, amesema VETA inaendelea kutekeleza Mradi wa Elimu na Stadi kwa Ajira zenye Tija Awamu ya Pili (ESPJ II), unaolenga kuanzisha vituo 15 vya umahiri katika maeneo mbalimbali ya mafunzo ya ufundi stadi. Amesema vituo hivyo vitaongeza ubora wa mafunzo na kuwaandaa wahitimu wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira, ikiwemo fursa za ajira nje ya Tanzania kupitia vyeti vya kimataifa.

Photos from VETA's post 20/08/2026

SEKIBOKO: VIJANA GEUZENI UJUZI KUWA AJIRA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Husna Sekiboko, ametoa wito wa kuimarishwa kwa elimu na mafunzo ya ufundi na ujasiriamali nchini, akisema ujuzi wa vitendo unaweza kuwa silaha muhimu kwa vijana katika kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa kujiajiri na kuunda ajira kwa wengine.

Amesema hayo jana, tarehe 19 Agosti, 2026 akiwa kwenye banda la VETA katika Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, Jijini Tanga.

Sekiboko amesema badala ya vijana kuhitimu na kuendelea kusubiri ajira, wanapaswa kutumia ujuzi wanaoupata katika vyuo vya ufundi kuanzisha shughuli za uzalishaji, huku Serikali ikiendelea kuweka mazingira ya kuwawezesha kupata vitendea kazi, mitaji na masoko.

Amesema changamoto ya ukosefu wa ajira inahitaji suluhisho linalowafanya vijana kuwa sehemu ya uzalishaji, akisisitiza kuwa kijana mwenye ujuzi ana uwezo wa kujiajiri na baadaye kuwa mwajiri wa wengine.

“Ni bora kijana kuanza na kile kidogo alichonacho na kujenga shughuli yake mwenyewe, kwa sababu anaweza kujiajiri na baadaye kuajiri wengine. Kwa kufanya hivyo, anakuwa amefanya zaidi kwa ajili yake mwenyewe na jamii yake kuliko kusubiri ajira pekee,” amesema.

Ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea banda la VETA na kukutana na vijana na wanachuo na wahitimu wa VETA ambapo amesema ameona uwezo mkubwa walionao katika kutengeneza bidhaa na kutoa huduma zinazoweza kukidhi mahitaji ya jamii.

Kwa mujibu wa Sekiboko, vyuo vya ufundi stadi vina nafasi kubwa katika utekelezaji wa jitihada za kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa sababu vinawapatia vijana ujuzi wa vitendo ambao unaweza kutumika moja kwa moja katika uzalishaji.

Amesema ili ujuzi huo uwe na matokeo makubwa zaidi, vijana wanahitaji mazingira mazuri ya kujifunzia, vifaa vya kufanyia kazi na fursa za kupata mitaji ili kugeuza ujuzi wao kuwa biashara na ajira.

Amehimiza vijana kutumia fursa zinazotolewa na Serikali na taasisi mbalimbali kupata ujuzi na mitaji, akisema mtaji mdogo unaweza kuwa mwanzo wa shughuli kubwa endapo utatumika vizuri.

“Lengo ni kuondokana na utamaduni wa kusubiri ajira pekee. Kijana akipata ujuzi, anaweza kuutumia kuzalisha ajira yeye mwenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa katika taasisi,” amesema.

Amesema hatua hiyo pia inaweza kusaidia kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 kwa kuongeza idadi ya vijana wanaoshiriki katika uzalishaji na kujenga uchumi kupitia ujuzi, ubunifu na ujasiriamali.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


VETA Head Office, 12 VETA Road, 41104 Tambukareli, P. O. Box 802, Dodoma Tanzania, Email: Info@veta. Go. Tz Telephone: +255 26 2963661 Fax: +255 22 2863408 Url: Www. Veta. Go. Tz
Dodoma
PLOTNO.18

Opening Hours

Monday 07:30 - 21:30
Tuesday 08:00 - 21:30
Wednesday 07:30 - 21:30
Thursday 07:30 - 21:30
Friday 07:30 - 21:30