16/08/2026
🚨 Cristiano Ronaldo:
“Huu unaweza ukawa MWAKA WANGU WA MWISHO KUCHEZA MPIRA WA MIGUU na nataka kuacha urithi wa kukumbukwa sana.”
“Nimeshapanga vyema siku zangu za usoni za kuachana na soka"
16/08/2026
FULL TIME ⏰
Arsenal 3️⃣ ➖ 0️⃣ Man City
⚽ 1' Calafiori (🅰️ Lewis Skelly)
⚽️ 28' Kai Havertz (🅰️ Tzolis)
⚽️ 48' Odegaard (🅰️ Tzolis)
✅ Arsenal ni mabingwa wa Community Shield 2026
16/08/2026
HALF TIME ⏰
Arsenal 2️⃣ ➖ 0️⃣ Man City
⚽ 1' Calafiori (🅰️ Lewis Skelly)
⚽️ 28' Kai Havertz (🅰️ Tzolis)
Community Shield 2026
15/08/2026
🎙️ Mwandishi wa Habari: “Rúben, baada ya Manchester United kukuachisha kazi mwezi Januari, unajisikiaje kurudi hapa na kuwachapa vibaya sana leo?”
🗣️ Rúben Amorim:“Nina heshima kubwa sana na mapenzi tele kwa Manchester United. Ni klabu kubwa mno, mashabiki wao ni wa ajabu na daima nitathamini muda niliotumia pale. Lakini leo ulikuwa mchezo wa mpira wa miguu tu, na wajibu wetu ulikuwa kuja hapa kuonyesha mbinu zetu na kushindana.
Nadhani tumelifanya hilo vizuri sana. Manchester United wana wachezaji wazuri ajabu na bado naamini watapata mafanikio makubwa. Lakini leo hawakuonekana k**a timu niliyofundisha mimi. Walikuwa wazi mno uwanjani, kulikuwa na mianya kila mahali na kwa nyakati fulani walionekana kukosa umakini.
Tulitambua udhaifu huo na tulijua ni wapi tunaweza kuwaumiza. Tulipofungwa bao 1-0 ilituvuruga, lakini wachezaji walibaki watulivu. Tulivumilia tukasuka mpango wetu polepole na tukaik**ata mechi.
Gonçalo Ramos, Loftus-Cheek na wachezaji wengine wote walikuwa bora sana. Kila mmoja alielewa majukumu yake na kuyatekeleza. Hicho ndicho kilichonifurahisha zaidi.
Naitakia Manchester United kila la kheri. Natumai mara ijayo tutakapokutana, watatupa mchezo mgumu zaidi. Hata hivyo, kwa siku ya leo, AC Milan ilistahili ushindi huu.”
FT: Man Utd 2-4 Ac Milan
15/08/2026
Joao Pedro akiwa na Chelsea kwenye mechi za Pre-season za wazi na za ndani.
Mechi: 7️⃣
Magoli: 8️⃣
Amewaka 🔥 🔥 🔥
15/08/2026
Nahodha wa Manchester United 🏴 Bruno Fernandes amekosa mikwaju ya penati katika mechi mbili mfululizo za maandalizi ya msimu mpya.
❌ 🆚 Leeds Utd (kwenye mikwaju ya penati)
❌ 🆚 Ac Milan (kwenye dakika 90 za kawaida)
15/08/2026
Kocha wa Manchester City, Enzo Maresca amethibitisha kuwa Ruben Dias na Erling Haaland ndio manahodha wa kikosi hicho kuelekea kwenye msimu mpya wa 2026-27
Wachezaji hao wamechaguliwa baada ya kuondoka kwa Bernardo Silva.
15/08/2026
FULL TIME
Polisi Tanzania 1-1 Azam Fc
⚽️ 74’ Abdul Sopu (P)
⚽️ 89’ Anuary Jabir (P)
14/08/2026
FULL TIME ⏰
Singida Black Stars 3️⃣ ➖ 0️⃣ Fountain Gate Fc
⚽ 28' Jonathan Sowah
⚽️ 81' Yusuph Khamis
⚽️ 90' Mathew Tegisi
🇹🇿
14/08/2026
Kocha wa Man City, Enzo Maresca kuelekea kwenye mechi ya Community Shield Jumapili hii dhidi ya Arsenal
"Hii sio mechi ya kirafiki, ni mechi ya kombe. Siku zote k**a kuna mechi ya kombe huwa nahitaji kushinda, tumejipanga kuhakikisha tunabeba"