Dondoo za soka & michezo

Dondoo za soka & michezo

Share

Habari za Ligi mbalimbali,Matokeo ya Mechi mbalimbali Ndani n.a. Njee ya Tanzania,Habari za usajili wa wachezaji n.a. Habari za Michezo mengine

kwa habari mbalimbali za michezo na burudani ulimwenguni

Photos 12/06/2020

Jonas Mkude atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili baada ya kupata majeruhi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC.

Akiwa nje ya uwanja Mkude ataendelea na mazoezi mepesi pamoja na matibabu.

Photos 12/06/2020

EYMAEL Kumekucha Jangwani.
June 12,2020.

Akizungumza na BINGWA jana kutoka Shinyanga, Meneja wa timu hiyo, Abeid Mziba, alisema wamefanya mazoezi chini ya Charles Mkwasa, kwani kocha mkuu anatarajia kuungana na kikosi leo.

Alisema kati ya wachezaji waliokuwa wamebaki Dar es Salaam, kipa Metacha Mnata, amefika jana asubuhi na Bernald Morrison anaweza kufika leo.

“Tupo mazoezini jioni hii (jana) katika uwanja wa Fresho, kocha mkuu atakuwepo katika mazoezi ya kesho, Metacha amekuja na ndege ya asubuhi amewahi lakini pia Morrison atakuja asubuhi (leo),” alisema.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Msafara Dominic Albinus ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji alitaja sababu ya timu hiyo kufika alfajiri kuwa imetokana na changamoto walizopata njiani.

Albinus amezungumza na tofutti ya klabu hiyo, kuwa msafara wa timu hiyo ulichelewa baada ya gari yao kupata hitilafu ya kupasuka tairi ya mbele eneo la Manyoni mkoani Singida.

“Tumechelewa sana, lakini tunawashukuru sana wanachama na mashabiki wa Shinyanga ambao wametusubiri hadi alfajiri kutupokea, hii imetupa faraja kubwa na kwa wachezaji imewatia moyo,” alisema.

Photos 14/08/2019

Kocha Mkuu wa Klabu ya Chelsea, Frank Lampard amethibitisha kuwa kiungo wake N'Golo Kanté atakosekana kwenye mchezo wa leo wa UEFA Super Cup dhidi ya Liverpool utakaochezwa saa 4 usiku
-
Aidha, Lampard amesema atandelea kuwatumia zaidi wachezaji chipukizi ambao ni Mason Mount na Tammy Abraham kwenye kikosi chake

Photos 13/08/2019

MICHEZO: Mkurugenzi wa Klabu ya Barcelona, Eric Abidal amesafiri kuelekea nchini Ufaransa kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Klabu ya Paris Saint-Germain ili kumrudisha Camp Nou Mbrazil, Neymar

> Mchezaji huyo aliondoka Barcelona kwenda PSG kwa usajili uliyoweka rekodi wa Euro milioni 200 mwaka 2017

Photos from Dondoo za soka & michezo's post 01/08/2019

NICOLAS PEPE ASAJILIWA RASMI ARSENAL‬

‪- Mchezaji huyo raia wa Ivory Coast (24) amesaini kandarasi ya miaka mitano kwa dau la Paundi Milioni 72‬

‪- Anakuwa mchezaji ghali kusajiliwa Arsenal‬

‪Unadhani Pepe, Lacazette na Aubameyang watafunga magoli mangapi jumla msimu ujao?‬

Photos 01/08/2019

Guardiola, Klopp washikana mashati tuzo ya Kocha Bora FIFA
Unafikiri ni nani anafaa kuwa kucho bora wa FIFA kwa msimu uliopita

Photos 01/08/2019

Kiungo wa klabu ya Manchester United Paul Pogba amesema kwamba alikua akivutiwa sana kujiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania ila kutokana na muendo wa klabu hiyo hivi sasa anaweza kuwa hana ndoto za kujiunga na klabu hiyo

Photos from Dondoo za soka & michezo's post 01/08/2019

Hizi ndio Jezi mpya za SIMBA SC kwa msimu mpya wa 2019/2020

Photos 01/08/2019

Mancheater united Pia wamewakilisha ada ya paun 80 milion kwa harry maguire na baada ya zile ofa za awali kukataliwa UNITED wanataka kumfanya beeki huyo wa kingereza kuwa beki ghali zaid duniani

Photos from Dondoo za soka & michezo's post 01/08/2019

Uhamisho wa mabadilishano kati ya paul dyabala na Lukaku sasa umebakia hatua chache kati ya manchester united na mchezaji klabu na klabu zimeshakubaliana

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


Msimbazi Sentsr
Dar Es Salaam