Lady Ayshah

Lady Ayshah

Share

Business & Digital Marketing Coach
Founder – WIDBN (Women in Digital Business Network)
Je, biashara yako ipo mtandaoni lakini haiuzi?

Mimi nakusaidia ➡️content inayovutia wateja,Ads & mbinu sahihi
Mafunzo na ushaur 👇
https://wa.me/message/TAVGVSA3P4P6F1

01/09/2026

RIZIKI YAKO HAIWEZI KUKOSEA ANWANI

September hii,usiingie kwenye biashara ukiwa na presha ya kutaka kila kitu kitokee kwa wakati ulioupanga

Kuna siku utauza sana,kuna siku utauza kidogo na kuna siku hutauza kabisa,usiruhusu siku ambayo haikuenda k**a ulivyotarajia ikufanye usahau mambo yote ambayo Mungu ameshakupa

K**a umeomba riziki, pia jifunze kushukuru hata kabla hujaiona kwa sababu sisi tunapanga lakini Mwenyezi Mungu ndiye anayejua wapi na lini riziki yetu itakutana nasi

Jukumu lako si kujua itakuja lini,jukumu lako ni kuhakikisha unapambana,unaweka juhudi na unatengeneza mazingira ya kukutana nayo

Mwezi mpya, moyo wa shukrani zaidi, kumbuka juhudi ni zako riziki ni ya Mungu ishi na hii

Uwe mwezi wa neema na baraka kwenye utafutaji wako,Mwenyezi Mungu akuongezee wateja zaidi kwenye biashara yako

Photos from Lady Ayshah's post 31/08/2026

Wafanyabiashara wengi wanapenda kuonyesha bidhaa zao lakini wanasahau jambo moja muhimu mteja hanunui bidhaa kwa sababu tu ipo

Ananunua kwa sababu anaamini bidhaa au huduma hiyo inaweza kumsaidia kutatua tatizo, kufikia hitaji au kupata matokeo anayoyataka

Marketing nzuri haizungumzii biashara yako tu

Inazungumza na tatizo la mteja

Leo pitia content zako 3 za mwisho zinaonyesha bidhaa yako tu au zinaonyesha pia tatizo unalotatua au hitaji la mteja?

30/08/2026

Something is about to change

Msimu mpya
Safari mpya
Fursa mpya

WOMEN IN DIGITAL SEASON 3

Are you ready? Stay tuned

Photos from Lady Ayshah's post 29/08/2026

Mteja mpya hanunui bidhaa tu,ananunua uhakika kwamba hata yeye hatopoteza pesa

Ndiyo maana picha za wateja,orders na feedback ni social proof inayopunguza mashaka na kuongeza trust kabla ya purchase.

Usiache kupost kuhusu wateja wako na feedback zao wakati mwingine hicho ndicho kinachomshawishi mteja mpya anayekufuatilia kimya kimya

28/08/2026

Mwaka huu hatuzungumzii tu biashara

Tunazungumzia fursa zinazopatikana kupitia digital
Jinsi unavyoweza kutumia mitandao ya kijamii kujenga brand yako,kuongeza visibility, kukuza network na kufungua milango ya opportunities mpya

Iwe wewe ni mfanyabiashara, mwajiriwa,content creator,professional au una kipaji unachotaka kukifanya kijulikane uwepo wako mtandaoni unaweza kuwa zaidi ya followers na likes unaweza kuwa connection yako na fursa yako

WOMEN IN DIGITAL SEASON 3
FROM VISIBILITY TO OPPORTUNITY
Your Digital Presence Is Your New CV

Are you ready?

Photos from Lady Ayshah's post 27/08/2026

Usichoke kujituma kwa sababu hujaona matokeo bado

Kuna vitu Mungu anakuandalia ambavyo huwezi kuviona leo,kazi yako si kujua lini vitatokea,kazi yako ni kuhakikisha unapofika wakati wake,wewe uko tayari

Usisahau hili ➡️ RIZK NI YA MUNGU LAKINI JUHUDI NI ZA KWAKO

Save hii kwa siku ambayo utahisi k**a juhudi zako hazina maana na share kwa mpambanaji mwingine anayehitaji kukumbushwa hili leo

26/08/2026

Usijenge biashara yako kwa kusubiri wengine watumie pesa kurusha tangazo halafu wewe uje kujaza comment kwenye tangazo lake ukitangaza biashara yako

K**a unataka kuvutia wateja wenye thamani, brand yako yenyewe lazima ionyeshe thamani, professionalism na sababu ya mteja kukuchagua

Marketing si kufuata matangazo ya wengine.

Ni kuwa na mkakati unaofanya biashara yako ionekane, ijenge trust na iwafikie wateja sahihi

Save hii k**a reminder

Ushawahi kuona mtu akifanya hivi kwenye ads zako? Tuambie kwenye comments

24/08/2026

USISUBIRI KILA KITU KIKAMILIKE NA UWE TAYARI

K**a una wazo la biashara,una ujuzi unaotaka kuugeuza kuwa huduma au unatamani kujifunza skill mpya usiruhusu hofu ikuzuie kuanza.

Anza na ulicho nacho,Jifunze hatua kwa hatua, boresha kila siku zingatia juhudi zako na usiache dua

Huhitaji kujua kila kitu kabla ya kuanza,unahitaji kuanza ili ujifunze zaidi

Zima zile sauti zinazokuambia HUWEZI,MUDA BADO,HII SIO KWA AJILI YAKO WEWE,BADO HUJAWA TAYARI,UTASHINDWA

Wazo lako linaweza kuwa mwanzo wa kitu kikubwa anza na epuka kuomba ushauri kwa kila mtu

Ungependa kuanza kujifunza skill gani au kuanzisha huduma gani?,je kuna hofu inakuzuia na hujui utaanza vipi mtandaoni COACH WAKO NIPO HAPA link ya whatsupp kwenye Bio

24/08/2026

Si kila kinachotokea kwenye biashara kinahitaji kuwa content

Jenga brand kwa kuonesha thamani,uzoefu wa wateja, feedback na mazingira ya kazi sio nini unakiingiza kila siku

Kuna taarifa zinaweza kujenga trust kwa wateja,lakini nyingine ni bora zibaki kuwa taarifa za ndani za biashara

Jenga visibility kwa mkakati bora na sio ule unaokupotezea biashara yako

Vitu gani katika biashara sio muhimu kuwa content? Share kwenye comment na wengine wajifunze

23/08/2026

Kila notification inaweza kuwa ujumbe kuhusu tatizo linalohitaji hatua ili kulinda account na visibility yako

Usipuuze ielewa na chukua hatua na usipojua nini ufanye mtafute mtaalam akusaidie

Save hii post na share na mwingine anayehitaji kujua.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


Dar Es Salaam