29/07/2026
TAPELI MPYA MJINI
Club ya Simba yatambulisha tapeli mpya mjini wakimwita victor osmen ibrahim dombia,licha ya club ya simba kutoonesha kiwango kizuri kwenye michuano ya kagame secafa cup, kuna huyu mchezaji amejizolea umaarufu kwa kuonesha kiwango kibovu zaidi. je apewe muda au big no kwake?
29/07/2026
π¨π£ Kinda wa Barcelona aliyezaliwa mwaka 2010, Ebrima Tunkara, ambaye ana asili ya Gambia lakini anaiwakilisha Hispania katika timu za vijana, amewashangaza wachezaji wa kikosi cha kwanza kutokana na nguvu na umbo lake la kipekee, licha ya kuwa na umri wa miaka 16 tu. Alizaliwa Lamoi, Gambia, kabla ya kuhamia Hispania akiwa mtoto pamoja na familia yake.
Mwezi uliopita, Tunkara alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora (MVP) wa Mashindano ya Ulaya kwa timu za chini ya miaka 17 (U17 Euro), baada ya kuhusika kwenye mabao matano (mabao na pasi za mabao) katika michezo minne. π«
Kocha Hansi Flick pamoja na Barcelona wanamuona k**a mmoja wa vipaji vikubwa vya baadaye, ndiyo maana amepewa nafasi ya kufanya maandalizi ya msimu mpya akiwa na kikosi cha kwanza.
π La Masia inaonekana imeibua tena lulu nyingine yenye uwezo mkubwa wa kuwa nyota wa baadaye. π₯Ά
24/07/2026
simba kamleta kwenu dombia ibrahim
22/07/2026
yanga wamehitimisha kwa upande wa wazawa kwa chuma hiki
22/07/2026
NJIA 6 AMBAZO MWANAUME UNAWEZA KUZITUMIA KUJIKWAMUA KWENYE UMASIKINI
Hizi ni njia sita ambazo mwanaume anaweza kutumia kujinasua kutoka kwenye umaskini:
Jifunze ujuzi unaouzwa sokoni β Jifunze taaluma k**a udereva, ujenzi, ufundi, teknolojia, kilimo cha kisasa au biashara. Ujuzi huongeza nafasi za kupata kipato.
Anzisha biashara au kazi ya pembeni β Usitegemee mshahara pekee. Anza biashara ndogo inayolingana na uwezo wako na uikuze hatua kwa hatua.
Dhibiti matumizi na weka akiba β Tumia chini ya unachopata, epuka matumizi yasiyo ya lazima, na tenga sehemu ya kipato kwa akiba au uwekezaji.
Wekeza badala ya kutumia kila kitu β Wekeza kwenye kilimo, mifugo, vifaa vya kazi, hisa, au biashara yenye uwezo wa kukua kwa muda mrefu.
Jenga mtandao wa watu wenye malengo β Zunguka na watu wanaokuhamasisha kufanya kazi, kujifunza, na kutafuta fursa mpya badala ya wanaokurudisha nyuma.
Kuwa na nidhamu na uvumilivu β Mafanikio ya kifedha yanahitaji kufanya kazi kwa bidii, kujifunza kila siku, kutokata tamaa, na kuwa na mpango wa muda mrefu.
Kauli nzuri ya kuhitimisha ni:
"Umaskini hauondoki kwa bahati, unaondoka kwa maarifa, nidhamu, kazi na maamuzi sahihi yanayorudiwa kila siku."
22/07/2026
unadhani mtasingwa ataavaa jezi namba ngapi?
22/07/2026
Klabu ya Azam FC imemtambulisha rasmi kiungo Donovan Makoma 27, raia wa Ufaransa kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Birkirkara inayoshiriki Ligi kuu Nchini Malta.
Kiungo huyo mkabaji mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amewahi kuchezea timu ya Taifa ya Ufaransa ya umri chini ya miaka 16.
via
22/07/2026
wydad wakanusha kujihusisha na makubaliano kati yao na simba dhidi ya mchezaji wao selemani mwalimu waapa kuchukua hatua kuhusu simba kutangaza kumpakiza mchazaji huyo