Liverpool habari

Liverpool habari

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Liverpool habari, Dar es Salaam.

Shabiki kindakindaki wa Liverpool!
🔴 Kuishi kwa moyo wa "You'll Never Walk Alone."
📊 Habari za wachezaji, takwimu, na uchambuzi wa mechi moja kwa moja.
🔥 Mabingwa wa kweli, tunaandika historia kila msimu

09/06/2026

🚨 CURTIS JONES AWEZA KUONDOKA LIVERPOOL?

Liverpool hawana mpango wa kumuuza Curtis Jones, lakini wanaweza kusikiliza ofa iwapo kiungo huyo ataomba kuondoka mwenyewe majira haya ya joto.

Taarifa zinaeleza kuwa Liverpool wanamthamini Jones kwa takribani pauni milioni 35, huku Inter Milan wakitajwa kuwa klabu iliyoonesha nia kubwa zaidi ya kumsajili hadi sasa.

Cha kuvutia zaidi, Federico Chiesa amefichua kuwa Jones amewahi kumuuliza kuhusu maisha ya soka na maisha ya kawaida nchini Italia, jambo linaloendelea kuongeza tetesi za uwezekano wa kiungo huyo kuhamia Serie A.

Je, Liverpool wanapaswa kupambana kumbakiza Curtis Jones au waachie aondoke ikiwa atahitaji changamoto mpya?

🔴

06/06/2026

CHIESA AFUNGUKA KUHUSU MUSTAKABALI WAKE LIVERPOOL

Winga wa Liverpool, Federico Chiesa, ameweka wazi kuwa anahitaji kupata muda wa kucheza mara kwa mara, na endapo hilo halitatokea ndani ya Premier League atalazimika kutafakari chaguo jingine.

> “Nataka kucheza mara kwa mara. K**a sitapata mwendelezo wa kucheza kwenye Premier League, nitapaswa kutafuta sehemu nyingine.”

Chiesa pia alikiri kuwa msimu wake wa kwanza Anfield haukuwa rahisi kutokana na kukosa nafasi nyingi za kucheza.

> “Katika mwaka wangu wa kwanza Liverpool, kwa kweli sikupata kucheza sana.”

Hata hivyo, nyota huyo wa Italia amesema bado hajafanya uamuzi wowote kuhusu kuondoka. Atashiriki ziara ya maandalizi ya msimu nchini Marekani kabla ya kufanya mazungumzo na klabu pamoja na kocha mpya wa Liverpool, Andoni Iraola.

> “Nitaenda kwenye ziara ya pre-season Marekani, kisha nitazungumza na klabu na kocha mpya Iraola, halafu tutaona kitakachotokea.”

Kauli hizi zinaashiria kuwa mustakabali wa Chiesa ndani ya Liverpool bado uko wazi, huku maamuzi ya mwisho yakitegemewa baada ya mazungumzo yake na benchi jipya la ufundi.

Je, unaona Chiesa anapaswa kubaki Liverpool na kupigania nafasi yake, au ni muda wa kutafuta changamoto mpya? 🔴🇮🇹

05/06/2026

🚨 NGUMOHA ATULIE, HAKUNA KWENDA MAHALI POPOTE! 🔴

Kuna kelele nyingi sokoni, lakini ukweli ni kwamba Rio Ngumoha hana mpango wa kuondoka kwa sasa.

Inaripotiwa kwamba Bayern Munich walikuwa wameenda mbali zaidi kwenye mazungumzo na mchezaji huyo wa Liverpool mwenye umri wa miaka 17. Tarehe 26 Mei, pande zote mbili zilikuwa zimefikia makubaliano ya maneno (verbal agreement), baada ya Ngumoha kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na kocha Vincent Kompany.

Hata hivyo, mambo hayakuendelea mbele zaidi ya hapo. Hakukuwa na hatua rasmi za kumalizia dili, na mazungumzo yalikwama kabla ya kufika hatua ya mwisho.

Kwa sasa, ujumbe ni mmoja tu kutoka upande wa mchezaji: bado yupo Liverpool, na hana haraka ya kuondoka.

Hii ni ishara nzuri kwa mashabiki wa Liverpool ambao wamekuwa wakihofia kupoteza moja ya vipaji vinavyoonekana kuwa na mustakabali mkubwa klabuni.

🔴 Ngumoha bado ni mali ya Anfield — na saga inaonekana kupoa kwa sasa.

05/06/2026

Je, unaamini Alexander Isak atakuwa mmoja wa nyota watakaotikisa msimu ujao?

05/06/2026

🚨 BAYERN MUNICH WAGONGA HODI KWA RIO NGUMOHA

Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa Bayern Munich wameanza kufuatilia kwa karibu uwezekano wa kumsajili Rio Ngumoha, winga mwenye umri wa miaka 17 wa Liverpool ambaye anaonekana kuwa miongoni mwa vipaji vikubwa vinavyochipukia ndani ya klabu hiyo.

Hata hivyo, Liverpool wameweka wazi msimamo wao kwamba Ngumoha hauzwi kwa sasa, huku mipango ya klabu ikiwa ni kuimarisha safu ya ushambuliaji badala ya kuipunguza.

Mashabiki wa Liverpool, mnalionaje hili? Je, Liverpool wamefanya jambo sahihi kwa kusimama kidete na kukataa mawazo yoyote ya kumuachia Rio Ngumoha, au mnaona kuna mazingira ambayo yangeruhusu dili k**a hili kufanyika?

Tuambieni maoni yenu kwenye sehemu ya maoni. 🔴👇

05/06/2026

🚨🔴 HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA LIVERPOOL!

Alisson Becker amefanya uamuzi wa kubaki Liverpool na kutimiza mkataba wake, akijitoa kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa angalau msimu mmoja zaidi.

Taarifa zinaeleza kuwa uamuzi huo ulifikiwa hata kabla ya kuondoka kwa Arne Slot, huku mazungumzo kuhusu mustakabali wake Anfield yakiwa yameanza muda mrefu kabla ya mabadiliko hayo ya benchi la ufundi.

Hii ni habari kubwa kwa Liverpool, kwani wanaendelea kuwa na mmoja wa makipa bora zaidi duniani ndani ya kikosi chao. Uzoefu, utulivu na uwezo wa Alisson vitakuwa muhimu katika safari ya Reds kuelekea mafanikio msimu ujao.

🔴🧤 Alisson stays. Liverpool stays strong.

05/06/2026
05/06/2026

🚨 EXCL: Liverpool continue to push hard for Kennet Eichhorn, with fresh talks taking place over the last 48 hours. 🔴

The 16-year-old’s camp are keeping all options open. A loan move to Bayer 04 Leverkusen is also being considered as part of Liverpool’s plan. 🇩🇪

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Website

Address


Dar Es Salaam