13/06/2026
๐จ OFFICIAL: Kiungo wa zamani wa Klabu ya Simba SC ๐น๐ฟ, Deborah Fernandez ๐จ๐ฌ hapo jana aliisaidia Klabu yake ya Swehly FC ๐ฑ๐พ kubeba Ubingwa wa Ligi Kuu Nchini Libya ๐ฑ๐พ baada ya kushinda kwa Penalti 4-3 dhidi ya Al Nasr baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Al Nasr ๐ฑ๐พ ni Klabu ambayo wanachezea wachezaji watatu wa zamani wa Simba SC, Kibu Denis ๐น๐ฟ, Steven Mkwala ๐บ๐ฌ na Fabrice Ngoma ๐จ๐ฉ.
13/06/2026
Mikel Obi kabla ya mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia kati ya Mexico na Afrika Kusini:
"Leo Waafrika wote tunaishangilia Mexico! Mnajua kwa nini? Tunataka Afrika Kusini waondoke mapema warejee nyumbani kulinda ajira zao. Tukiwashabikia, watasema tunawanyang'anya kazi zao!"
Ni mbayaaaaaa!๐๐คฃ๐คฃ
follow us
11/06/2026
๐จ HABARI MPYA:
Mwamuzi wa soka kutoka Somalia, Omar Artan, ameteuliwa kusimamia mechi inayosubiriwa kwa hamu kati ya Paris Saint-Germain F.C. na Aston Villa F.C. huko Salzburg katika michuano ya UEFA Cup 2026.
Hii ni hatua kubwa kwa mwamuzi huyo, ambaye hapo awali alikosa nafasi ya kushiriki katika Kombe la Dunia baada ya kunyimwa ruhusa ya kuingia nchini Marekani.
09/06/2026
For the first time in history, weโll have ๐ African teams in the FIFA World Cup! ๐คฉ๐ซถ
09/06/2026
Klabu ya Kagera Sugar imeungana na Geita Gold FC kurejea Ligi kuu ya soka ya NBC Tanzania bara baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Kengold FC katika uwanja wa Kaitaba, Kagera na kufikisha pointi 68 ambazo haziwezi kifikiwa na Mbeya Kwanza na Polisi Tanzania waliopo nafasi ya tatu na nne mtawalia zikiwa zimesalia mechi mbili Ligi kutamatika.
Kocha Juma Kaseja amewarejesha Wanankurukumbi Ligi kuu wakifikisha jumla ya alama 68 baada ya kushinda mechi 21, sare 6 na vichapo viwili kwenye michezo 28 ikiwa ni msimu mmoja tu tangu washuke daraja mwishoni mwa msimu wa uliopita.
MSIMAMO ๐4๏ธโฃ Championship
1. Geita Gold FC โ mechi 28 โ pointi 71
2. Kagera Sugar โ mechi 28 โ pointi 68
3. Mbeya Kwanza โ mechi 28 โ pointi 60
4. POLISI Tz FC โ mechi 28 โ pointi 60
06/06/2026
Ameskika Leo wakala wa Jean Claude Girumugisha kupitia mahojiano ya kwenye Crown FM Radio.
Akisema yakuwa Kwa sasa thamani ya mteja wake inafika mpaka Dola million 1.5 za kimarekani Ambayo ukiileta kwenye fedha zetu za kibongo ni karibia billion 3 na point kadhaaaa na hakuishia hapo akasema viongozi wa Yanga walimfuata kuulizia huduma ya mteja wake walipotajiwa bei bado hawajpeleka mrejesho kwake.
Ila tuwe wa kwelii k**a thamani ya huyu mchezaji ni billion 3 basi hakuna club yoyote inaweza ikampata hapaa bongo maana usajili wetuu tunaujuwa hakuna Club ya kutoa hiyoo hela k**a kwelii thamani Yake ikoo hivooo
Ameelezea jins alivyomleta kagere simba nakuongezea kua soka la Tanzania analijua vizuri
06/06/2026
Klabu ya Simba SC inatajwa kumuweka katika rada zao mshambuliaji Kevin Bakare Ouato anayekipiga katika klabu ya Asec Mimosa inyoshiriki Ligi Kuu Ivory Coast ๐ฎ๐ณ
Kevin Bakare ambaye alijiunga na Asec Mimosa July 2025 akitokea Club Omnisports de Korhogo (CO Korhogo) ya hapo hapo Ivory Coast
Profile ya yake
Jin: Kevin Bakare Ouato
Kuzaliwa: March 09, 2004
Umri: Miaka 22
Urefu: 184cm
Nafasi: Mshambuliaji/Winga wa Kulia
Klabu ya sasa: Asec Mimosa
Msimu huu akiwa na Asec kwenye ligi kuu kafunga mabao 12 akiwa nafasi ya 03 kwa ufungaji bora nyuma ya miamba 03
Vinara wa upachikaji mabao Ligie 1 LONACI
1. Amani Michael AFAD Plateau - 17โฝ๏ธ
2. Tidiane Diabate - CO Korhogo- 14โฝ๏ธ
3. Souleymane Fofana- Asec Mimosa- 12โฝ๏ธ
4. Kevin Bakare- Asec Mimosa- 12โฝ๏ธ
5. Sindou Bakayoko - Stella Adjame - 11โฝ๏ธ
Takwimu zake katika ligi kuu
Mechi 20
Magoli 12
Assist 03
๐Ligi Kuu โ
๏ธ
Kwenye CAFCL
Mechi 02
Magoli 00
Assist 00
K.Njano 00
K.Nyekundu 00
Asilimia za kuanza kikosi cha kwanza 50%
Wastani wa dakika za kucheza kiwanjani - 75
Combination yake na Souleymane Fofana imechangia maholi 24 yaliyowawezesha wao kutwaa taji la Ligi Kuu Ivory Coast ๐
Simba itakabiliana na upinzani kutoka kwa Al Masry ya Misri na Grenoble Foot ya Ufaransa inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Ufaransa
Je! Simba wataharakisha kufamikisha dili hili??
06/06/2026
๐จKOCHA wa Simba, Steve Barker, amefanya mabadiliko ya muundo wa kikosi chake yanayomuhusu sana Elie Mpanzu ambaye Jumapili iliyopita ya Mei 24, 2026 aliwapa Wekundu hao wa Msimbazi ushindi, akisema sasa Mkongomani huyo atakuwa anacheza k**a mshambuliaji wa kati.
Mechi tatu zilizopita za Simba, Barker amemuondoa Mpanzu kutoka kucheza k**a kiungo anayeshambulia akitokea pembeni na sasa anamuanzisha eneo la mshambuliaji wa kati, mabadiliko ambayo yamemrudisha benchi mshambuliajia halisi Seleman Mwalimu.
Akizungumzia mabadiliko hayo, Barker ameliambia Mwanaspoti kuwa, kwasasa Mpanzu ni mmoja wa washambuliaji wake wa kati ambapo atakuwa anamtumia eneo hilo kuiongezea timu hiyo ubora.
Barker amesema anataka safu yake ya ushambuliaji iwe na watu wenye kasi ambao mara wanapounasa mpira wanatakiwa kukimbia haraka kwenda kushambulia wakati ambao wapinzani wanakuwa bado hawajajipanga sawasawa.
โMpanzu ni mmoja wa washambuliaji wetu kwasasa, nakubaliana na wewe kwamba alikuwa anatumika kuna wakati akitokea pembeni lakini sasa atakuwa anacheza hapo, kuna kitu bora zaidi tunakilenga kutoka kwake,โ
โTunahitaji watu wenye kasi zaidi kule mbele ambao wakati timu pinzani ikipoteza mpira, tunatakiwa kuwa na kasi ya haraka kwenda kuwashambulia kabla hawajajipanga sawasawa na hili limekuwa linafanyika sawasawa.โ