Ibrah de fundi

Ibrah de fundi

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Ibrah de fundi, Sport & recreation, Dar es Salaam.

29/08/2025

USHINDI MKUBWA ZAIDI WA BLUCE LEE

Muigizaji maarufu zaidi kuwahi kutokea
Bluce Lee aliwahi kusema kuwa moja ya ushindi mkubwa zaidi katika maisha yake ni ule alioushinda ugonjwa mkubwa uliokua unamuandama

Mnamo mwaka 1970 Bluce Lee aliumia vibaya mno uti wa mgongo alipokua akifanya mazoezi ya weightlifting nakupelekwa hospitali ambapo madaktari walimwambia kuwa inabidi aachane na sanaa ya uigizaji kutoka na tatizo ilo ambalo lilimlazimu kulala tu kwenye kitanda nakushindwa kusimama kwa muda wa miezi sita

Ndipo alipoamua kuanza kusoma vitabu mbali mbali zaidi ya vitabu 200 vya afya mwili na tiba za kisayansi nakuanza mpango maalumu wa mazoezi ambao ulimsaidia mpaka kuweza kusimama tena..

Funzo Haijalishi ni hali gani uliyonayo kwasasa lakini ukiweka juhudi nakutokata tamaa siku moja utainuka nakutimiza malengo yako hapa nazungumza na wale ambao wamekataa dhidi ya malazi mbali mbali nakuona kuwa mwisho wakutimiza ndoto zao umefika hapana jipe moyo simama tena nakuelekea ndoto zako..

29/08/2025

UMAARUFU MKUBWA BAADA YA KIFO

Pichani ni mchoraji maarufu wa kipindi cha zamani mnamo miaka ya 1890 Bwana Vicent van gogh nakupata umaarufu zaidi baada ya kufariki

Vicent van gogh alizaliwa mwaka 1853 uko nchini uholanzi alikua na kaka yake aliyeitwa Theo ambae ndiye aliyekua akimsaidia sana hapo baadae

Vicent van gogh alifanikiwa kichora mochoro mingi zaidi wakati wa uhai wake lakini cha ajabu aliuza mchoro mmoja pekee tu hali iliyomfanya kuwa na mawazo mengi mpaka kukumbwa na tatizo la afya ya akili

Nasiku moja ndipo mwili wake ulikutwa ukiwa umepigwa risasi eneo la tumboni ukiwa ndani ya chumba wengi wakisema kuwa aliamua kujiua yeye mwenyewe ingawa hakuna uthibitisho mkubwa kuhusu kuuliwa wengi waliamini ameamua kujiua yeye mwenyewe

Lakini cha ajabu baada tu yakifo chake ndipo watu walipoanza kufutilia kazi zake hususani za sanaa ya uchoraji na picha zikaanza kuuzwa kwa kasi zaidi na dola nyingi zaidi nakupata umaarufu mkubwa ingawa yeye mwenyewe tayari alikua ameshafariki...

Funzo maisha siku zote hayatakupa kile unachotaka daima na wakati mwingine watu hawataweza kujua thamani yako na umuhimu wako pale utakapoamua kujitenga nakua mbali nao kwahiyo kuna ni muhimu kukaa mbali na watu waliokuzoea au mazingira fulani ili kujenga tu thamani yako.....

29/08/2025

MAMA HAKUAMINI ALIPOSIKIA NIKO UFARANSA..

Sadio mane anasema alizaliwa katika nchi ya senegal ndani ya kijiji kiitwacho Bambali mnamo mwaka 1992 kijiji masikini zaidi nchini senegal

Baba yake alikua ni himamu wa msikiti na alifariki wakati sadio mane akiwa mdogo sana hali iliyoleta majonzi zaidi kwa wakati huo akiwa na ndoto kubwa ya kucheza mpira na mara nyingi wazazi wake walimtaka azingatie zaidi masomo na si kitu kingine

Kutokana nahali ya kimasikini kijijini kwako sadio mane ilibidi atoroke kijijini kwao nakuelekea mji mkuu wa senegal yaani Dakar ikiamini huko atapata nafasi yakucheza nakuonekana zaidi

Alifanikiwa kufika katika kituo cha akademi ya Generation foot akiwa hana viatu vizuri vya mpira hali ilifanya kila mmoja amtazame nakumcheka yeye halujali ila pale alipopata nafasi yakuingia uwanjani alifanya vitu vikubwa vilivyofanya kila mtu amshangae

wakati huo familia yake ilikua haitambui chochote kuhusu sadio mane wapi alipo na anafanya nini mpaka pale akademi hiyo ya Generation foot ilipompa nafasi yakwenda Kufanya majaribio Ufaransa katika klabu ya Metz nakufanikiwa..

Anasema siku ambayo siwezi kusahau ni pale nilipopiga simu ya mjomba wangu kwanjia ya whatsapp nakuambia kuwa nataka niongee na mama baada ya kumuona mama yake sadio mane alilia kwa furaha nakumwambia mama sasa niko Ulaya ufaransa mama yake hakuamini kwa urahisi mpaka alipomuelewesha zaidi nakujikuta wote wakilia kwa furaha..

funzo sadio mae anasema haijalishi uko wapi mazingira gani lakini ukiamua na kuwa imani yote kwa MUNGU yanawezekana ila kikubwa zaidi usisahau kule ulipotoka ndio maana leo hii sadio amejenga vituo vikubwa kijijini kwao vya michezo pamoja na hospitali na nyumba za ibada imani maauzi yote yanawezekana....

09/02/2024

Kuna wakati inatulazimu kwenda mbali ili kujitafuta wenyewe kwanza
Football is long life
Dear God bless us

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Dar Es Salaam