Elcapitano Maestro

Elcapitano Maestro

Share

1️⃣. Sports Pundit (English & Swahili) 2️⃣. i'm the best football analyst in africa

12/08/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

YANGA SC MABINGWA NGAO YA JAMII BAADA YA KUIFUNGA SIMBA 2026.

Elcapitano Maestro 🗣 Mlango mmoja unapofungwa jaribu kufungua mwingine ndicho walichofanya yanga.

Yanga walimtaka sana Fei wa Azam, lakini kumpata Albert Kangwanda ni moja ya chaguo sahihi kwao.

Kangwanda MVP ligi ya Zambia msimu uliopita alifunga mabao ya kutosha na assists na ukiangalia ligi ya zambia na Tanzania hakuna utofauti mkubwa.

ipo hivi...👇

Kiungo anapokuwa na uwezo wa kufunga ni sawa na kuwa na namba 9 kivuli ambae utakuwa unanufaika nae pindi timu inapoenda kushambulia.

Yanga wanapaswa wampe muda mwingi wa kucheza Kangwanda akiweza kuzoea mazingira atafanya vizuri sana k**a alivyokuwa zambia.

Moja ya shida kubwa kwa yanga ni kutokuwa na namba 6 ambayo ataifanya timu ianze kucheza kutokea chini.

ili uweze kufanikiwa klabu bingwa Afrika ni lazima uwe na aina hio ya namba 6 huwa ni msaada mkubwa kushusha presha ya mechi na kuwarudisha mchezoni wachezaji wenzake wakati mechi ikiendelea...

hilo eneo la namba 6 ni eneo nyeti sana kwa timu za waarabu siri yao ya ushindi huanzia hapo.

Kuhusu Simba...👇

Wana uwezo wa kumiliki mpira nguvu hio wanayo na ni jambo kubwa sana lakini kwenye mechi kubwa lazima uwe na plan zaidi ya moja.

yaani kazi inabidi ibaki kwako mpinzani ufungwe na plan a au b.

Plan A ya Simba ni kumiliki mpira huku wakiwachezesha mawinga wao lakini plan hio ikiwa chini ya ulinzi hapo ndipo utapoona nafasi ya Fei toto katika kikosi cha Simba.

Simba watafanya uamuzi mzuri sana ikiwa itampata mchezaji huyo kutoka Azam ikiwezekana hii post mfikishieni MO.

akiuliza imetoka wapi mtamwambia imetoka kwa mchambuzi bora zaidi wa soka barani Afrika (Elcapitano Maestro).

💁🏾‍♂️

11/08/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Elcapitano Maestro 🗣 Leo nilipata wasaa wa kusikiliza vipindi vyenu vya michezo redioni nimeona wachambuzi wenu wengi kuna namna wanashindwa kuongea uhalisia.

Labda pengine wanatanguliza mahaba zaidi katika taaluma yao ya uchambuzi.

Ningekuwa katika moja ya kipindi naona waTz mngefurahia sana 😄 na ku enjoy sayansi ya soka kwa ujumla wake, tatizo hakuna ofa nzuri iliyokuja.

🗣Wapo wachambuzi wanaosema kwamba Sele Mwalimu hakuwa mchezaji muhimu sana kwa Simba kwasababu alikuwa akitokea sana benchi.

..Jibu langu kwenu "Huwezi kutoa pesa nyingi umchukue mchezaji kwa mkopo kisha umuweke benchi tena mchezaji ambae anauzoefu na hio ligi.

Nadhani, huenda kuna vipengele vya kimkataba vinabana kwa Simba kumpa dakika nyingi za kucheza labda akicheza dakika nyingi zaidi kuna bonus lazima iongezeke, (waarabu tunajuana ukiweka dini pembeni sisi ni wazuri wa biashara).

Kwa dakika chache alizokuwa akipewa mwalimu bado alikuwa akionesha anastahili muda mwingi wa kucheza kuhusu hili wadau wa mpira tunalielewa."

Kwanini imekuwa pigo kubwa kwa Simba baada ya kuondoka mwalimu...

Baada ya Pre Season ya Simba kumalizika na kwa washambuliaji waliokuwepo ulikuwa unaliona pengo la Sele Mwalimu uzuri hata wao Simba waliona hili ndomana siku yao ya maadhimisho waliuthibitishia umma kwamba Mwalimu bado yupo.

Lakini wakati unajenga timu nae mpinzani wako anajenga timu yake na kwa bahati mbaya zaidi huyo mpinzani anajua k**a wewe ni bora k**a yeye tu, hapa ndipo tatizo lilipoanzia.

Misimu miwili mfululizo Yanga ili achukue ubingwa wa ligi ni mpaka asubiri mechi ya mwisho ya ligi na anaemfukuza ni yule yule wa siku zote.

Yanga wanaijua hatari ya kuchezea shilingi chooni ndomana kuelekea msimu huu 2026-27 wameona wafanye usajiri wenye nguvu.

Yanga wanaijua hatari ya Simba ni ipi lakini Simba wenyewe hawajui k**a wao ni hatari sana dhidi ya yanga ndomana Simba wanaishi kumtafuta mchawi baadala ya kuungana kuwa kitu kimoja.

💁🏾‍♂️

11/08/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

KUELEKEA KWENYE NGAO YA JAMII KATI YA YOUNG AFRICAN CLUB DHIDI YA SIMBA SPORTS.

Elcapitano Maestro 🗣Mashabiki wa mpira wa miguu wengi wao wana nadharia yao ya kuitafsiri mechi.

Kwasababu wao kila mechi inayokuja mbele wanaona ni wajibu kwa timu yake kupata matokeo.

Kwanini anaona ni wajibu kwake kwasababu ametoa kiingilio chake kushuhudia mechi mubashara.

Lakini uhalisia ni kwamba mechi zinatofautiana malengo.

Kuna mechi ili uibuke mshindi ni lazima ushinde hio mechi.

Kuna mechi ili uvuke hatua inayofuata inabidi unapate sare tu.

Na kuna mechi hata ukipoteza bado unaweza kubeba ubingwa.

Nini maana ya mechi za kirafiki...?

Mechi za Kirafiki lengo kubwa ni kujaribu mbinu mpya, kuwapa wachezaji dakika za kucheza na kujipima.

🗣Kuelekea karikoo derby

Simba kabla ya Derby wamepoteza 0-1 lakini kuelekea kwenye derby simba wana faida ya kuwa na kocha ambae anakijua kikosi chake vizuri na anajua raha ya kuifunga yanga ni ipi kwasababu amefanya hivyo tayari kabla.

Yanga kabla ya derby wamepoteza 1-2 kuelekea kwenye derby kocha wao yanga atatumia muda mwingi kuongea na safu ya ulinzi juu ya namna ya kuwa makini zaidi katika kujilinda.

Mechi ya ngao ya jamii itakuwa ni kati ya kocha wa simba dhidi ya wachezaji wa yanga.

Japo najua hili yanga wanalijua 👆 nao wameamua kucheza mind game ya hatari sana wametangaza kumsajiri Suleiman Mwalimu na sasa habari kubwa si derby tena bali ni usajiri wa mwalimu.

Namna nzuri ya simba kuondoa wasiwasi kwa mashabiki wao ni kuifunga yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

💁🏾‍♂️

10/08/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Elcapitano Maestro 🗣 Baada ya Rodri kuumia kupata jeraha la ACL kocha wa city kwa wakati huo gurdiola aliona mbadala sahihi wa nafasi yake alikuwa ni Bruno Guimarães.

Pep Guardiola alizungumza na bruno lakini makubaliano hayakuweza kufikiwa kwasababu Newcastle walihitaji pesa ya kuvunja rekodi itolewe.

Dili likafa kwa wakati huo na Man City ikakubali kucheza huku ikiwa na pengo la Rodri.

HATIMAE...

Kuelekea 2026-27 Bruno Guimarães amesaini kuijunga na Arsenal.

Mikel Arteta ni kocha ambae anajitahidi sana katika kuchagua wachezaji wa kuwasajiri katika hili nampa sifa.

Bruno Guimarães ni mchezaji mzoefu na mkomavu, ukiwa na Bruno ni sawa na kukaribia kuwa na Rodri.

Kuhusu hili 👆hata pep guardiola analijua.

Mikel Arteta ameifanya safu ya kiungo iwe kamili k**a alivyo ifanya safu ya ulinzi.

ikiwa mikel arteta atafunga usajiri bila kuleta nyota wengine / mwingine wa kiwango cha juu katika safu ya ushambuliaji basi kwa hakika arsenal haitoenda kuchukua Uefa champions league.

Huwezi kubeba ubingwa wa uefa champions league kwa kuwategemea Saka, Martinelli, Madueke wakupe mabao katika mechi za maamuzi.

Kwa Liverpool ya klopp hao wote watatu wanaanzia benchi.

💁🏾‍♂️

Photos from Elcapitano Maestro's post 09/08/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

USHAURI WENYE TIJA KWA VILABU VYA KITANZANIA...(Elcapitano Maestro).

Elcapitano Maestro 🗣 nini maana ya klabu ya mpira wa miguu ?? jibu la uhakika ni kwamba klabu ni wanachama.

Wanachama ndio chanzo cha pesa za kudumu, hapo kuna michango ya kila mwezi, ununuzi wa jezi, tiketi nk kwa ujumla wake kuna mambo mengi sana.

kwa kweli bila wanachama utategemea mdhamini na ikitokea mdhamini akaondoka basi klabu ndio inakufa.

kuhusu hili 👆 kila shabiki wa timu lazima alijue na alitambue.

Kauli mbiu ya dhahabu ni kwamba...ikiwa unaipenda klabu anza mguu mmoja mbele kwa kuwa mwanachama.

Nina swali kwenu 🤔 👇...?

Timu zetu za KITANZANIA natamani niwaulize..."unawezaje kumshawishi shabiki kuwa mwanachama?? najua mnayo majibu yenu.

Lakini kuna namna tatu za kumfanya shabiki kuwa mwanachama kabla ya kumwambia atoe pesa.

Namna hizo tatu...kuna Faida + Hisia + Fursa kwasababu mwanachama yeye ni binadamu lazima kuwe na mazingira rafiki ya kila mmoja anufaike kwa namna yake yaani klabu + mwanachama...

Klabu nyingi za Tz zinashindwa kusimama imara kwasababu hazina nguvu ya wanachama Boss akiondoka na timu inakufa.

Nikiwa k**a mchambuzi bora zaidi wa soka barani Afrika naona kuna umuhimu mkubwa wa mimi kuwa katika moja ya klabu kubwa zaidi Tz.

Nb: Shabiki anaangalia, ila mwanachama anaangalia na kuamua.

💁🏾‍♂️

06/08/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Elcapitano Maestro 🗣 Liverpool walikuwa wanatoa takriban asilimia 12% ya mshahara wote wa klabu kwa Salah peke yake.

Ndio maana walipoachana naye Juni 2026 Liverpool waliokoa takriban $27.8 milioni.

Salah ameenda Trabzonspor analipwa €17 milioni kwa msimu + 20% ya mauzo ya jezi yake.

Nb: wapo ambao watajiuliza kwanini Salah hakwenda Saudi Arabia.

Jibu ni kwamba Salah amechagua kwenda uturuki kwasababu anataka kubaki ulaya na kupata uhakika zaidi wa kucheza huku akiendelea kupokea mkwanja mrefu.

Uturuki inapambana sana katika kuifanya ligi yao iendelee kutizamwa zaidi duniani huu mpango wao endelevu utakuja kuwalipa.

💁🏾‍♂️

06/08/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Elcapitano Maestro 🗣 ni utani tu... hii picha anaoneshwa Rodri kisha anaulizwa unachagua kwenda Real Madrid au Barcelona 😄.

ingizo la Rodri utakuwa ni usajiri bora sana kwa Barcelona kwasababu rodri bado anaweza kukupa misimu mitatu ya moto sana.

💁🏾‍♂️

06/08/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

John Obi Mikel 🗣️ Nadhani Youri Tielemans ndiye mchezaji bora zaidi aliyesajiliwa ligi kuu msimu huu.

Manchester United wanawezaje kumsajili kwa pauni milioni 35 tu ?

Nilimwona akicheza msimu uliopita na kwenye Kombe la Dunia la FIFA mwaka huu, ni mchezaji mzuri.

Anaweza kutumika katika nafasi ya 6, 8 na 10 na atakuwa mchezaji muhimu kwa Manchester United.

💁🏾‍♂️

06/08/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

Vinicius Jr 🗣️Jose Mourinho anataka nicheze kwa furaha na shauku nilimaliza siku yangu ya kwanza ya mazoezi kwa mafanikio.

Ninaanza kumfahamu kocha wetu mpya na wachezaji na tunahitaji kujiandaa vyema kwa msimu mpya.

💁🏾‍♂️

04/08/2026

DARASA HURU 💁🏾‍♂️

RONALDO NAZARIO 🗣"Kabla ya fainali dhidi ya Ujerumani katika Kombe la Dunia la 2002, jambo la kushangaza lilitokea.

Tulipofika kwenye chumba cha kubadilishia nguo kabla ya mechi, kocha wetu, Luiz Felipe Scolari, alikuwa na kitu cha kutuonyesha kwenye televisheni.

ilikuwa matangazo kutoka O'Globo, chaneli ya Brazil, lakini haikuwa tu kipindi cha kawaida.

kwenye kipindi, walienda katika kila mji wetu kuonyesha jinsi vitongoji na majimbo yalivyokuwa yakisherehekea."

Hatimaye, walifika Bento Ribeiro na hapo hapo, mbele yangu, niliona mitaa nilipokulia nikicheza.

Niliona kuta nilizotumia kupiga mpira wangu, na niliwaona watoto wadogo wamesimama karibu na michoro ya rangi iliyochorwa nasi, k**a nilivyokuwa nikifanya.

Hilo ndilo jambo la mwisho tuliloona kabla ya kuingia uwanjani."

nb: Luiz Felipe Scolari alitoa somo la saikolojia zaidi kwa wachezaji na kuanzia hapo kila mchezaji alikuwa anajua ni nini anatakiwa aende kufanya uwanjani.

💁🏾‍♂️

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


Dar Es Salaam