Michael Noel

Michael Noel

Share

This page is personal, based on professional journalist

18/01/2026

Hii penati nadhani Brahim Diaz k**a amecheza fair play ili mchezo uanze upya.

18/01/2026

Kwa hali hii nafasi ya pili kwa Simba sc ligi kuu msimu huu inaweza isiwepo.

Droo ya 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar inaendelea kuiweka pabaya Simba sc kwenye mbio za Ubingwa.

07/05/2025

KUKOPESHA WASANII WASIO NA ELIMU YA FEDHA SERIKALI IMEKOSEA- MUSUKUMA

Mbunge wa Geita Joseph Kasheku Musukuma wakati akichangia kwenye bajeti ya wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amekosoa kitendo cha serikali kupitia mfuko wa sanaa kukopesha mabilioni ya fedha wasanii ambao wengi wao wameshindwa kurejesha mikopo hiyo.

Amesema Wasanii wengi hawana elimu ya fedha, hivyo wengi wao wameitumia mikopo hiyo kununua magari ama kuoa na hivyo kujikuta wanashindwa kutimiza malengo ya mikopo waliyopewa.

Mbunge Msukuma amesema ni vyema mikopo hiyo ikatolewa kwa watayarishaji (producers) badala ya kukopesha wanaoonekana kwenye Tv (Luninga) kwa kuangalia mionekano yao (shape) kitendo kinachosababisha serikali kukosa marejesho ya mikopo hiyo.

07/05/2025

KISA DERBY MUSUKUMA ATAKA BODI YA LIGI IVUNJWE

Mbunge wa Geita Joseph Kasheku Musukuma amemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuja na Majibu yanayoeleweka kuhusiana na mvutano unaoendelea baina ya Klabu ya Yanga, TFF, Bodi ya Ligi na Simba sc baada ya kuahirishwa mchezo wa Watani wa Jadi Yanga sc vs Simba sc Machi 08 mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam na Yanga sc kuweka msimamo wa kutocheza tarehe nyingine iliyopangwa.

Katika sehemu ya mchango wake Bungeni Jijini Dodoma wakati wa wasilisho la Bajeti ya Wizara hiyo, Musukuma ameshauri iundwe bodi mpya ya ligi iliyo huru badala ya hii inayopokea maelekezo.

Nini maoni yako juu ya Mchango huu wa Msukuma? Tuandikie

07/05/2025

PROF KABUDI AOMBA BAJETI YA TSH BIL. 519,660,073,000

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia kwa Waziri wake Prof. Palamagamba Kabudi imeliomba Bunge kuridhia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/26 ikiwa na makadirio ya shilingi bilioni mia tano kumi na tisa milioni mia sita sitini na elfu sabini na tatu (519,660,073,000).

Bajeti ya wizara hiyo imesomwa leo Mei 07, 2025 na Waziri Prof. Kabudi Bungeni Jijini Dodoma.

04/11/2024

Early voting is coming to a close today in the United States as the nation gears up for election day tomorrow. Who is the most suitable candidate for enhancing Africa's diplomatic relations and development?

01/11/2024

KOCHA MPYA MANCHESTER UNITED

Ni Ruben Amorin aliyekuwa akiinoa Sporting ya Ureno.

30/10/2024

UKIAMBIWA MWANAUME ATAKULA KWA JASHO NDIO HII SASA.

HT' Singida BS 0-0 Yanga sc.

28/10/2024

Asipopewa Ballon d'or itakuwa ni dhulma na ukatili.

Ni usiku wa Leo Paris Ufaransa. K**a watafanya uporaji na kumpa Rodri itakuwa ni anguko la hizi tuzo.

Photos from Michael Noel's post 27/10/2024

BOCCO, DILUNGA, NDEMLA WAJERUHIWA AJALINI

Basi la klabu ya JKT Tanzania limepata ajali leo eneo la Mbweni wakati kikosi kikirejea Dar es salaam kutoka mkoani Dodoma baada ya mchezo wa Jana dhidi ya Dodoma Jiji.

Taarifa iliyotokewa na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Jemedari Said Kazumari imeeleza kuwa basi hilo lilikuwa likiendeswa na Capl Hassan Bakari ambapo liliacha njia na kutumbukia mtaroni.

Wachezaji waliopata maumivu kufuatia ajali hiyo ni John Bocco, Dany Lyanga, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Hassan Kapalata, Maka Edward, Mohamed Bakari, Hassan Machezo, Salum Gado na Gamba Matiko.

Wachezaji hao waliopata maumivu wapo chini ya uangalizi wa madaktari.

Mungu awaponye na kuwarejesha katika Afya yao ya kawaida waendelee na majukumu ya kuipambania timu yao.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


6404
Dar Es Salaam