Tengo online tz

Tengo online tz

Share

°KWA HABARI ZA MICHEZO °TETESI ZA MICHEZO °NA MIJADALA KUHUSU MICHEZO ° NDANI NA NJE YA TANZANIA °FOLLOW, LIKE, COMMENT, SHARE,

WE ARE THE BEST IN TOWN

02/09/2026

✅Mwanetu Hasheem Kindemile amefurahi mwenyewe Baada ya kukutana na Role model wake Peter Shalulile.

Msimu Jana kuna mechi jamaa yetu alipiga Ile shangilia ya Shalulile Baada ya kufunga goli.

02/09/2026

Klabu ya Malkiya Sports Club ya nchini Bahrain imekamilisha rasmi usajili wa kiungo Naby Camara, ambaye ametua kikosini hapo k**a mchezaji huru baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuachana na miamba ya soka la Tanzania, Simba SC. Staa huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo ya Bahrain.

02/09/2026

PRINCE DUBE MCHEZAJI BORA WA MWEZI WA NANE LIGI YA ZIMBABWE

Nyota wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa anakipiga klabu ya Hardrock ya Zimbabwe Prince Dube ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi wa nane ligi kuu ya Zimbabwe

Kwenye mwezu wa nane Dube amefunga magoli mannne na kutoa pasi tatu za magoli.

Photos from Tengo online tz's post 02/09/2026

Yupi mchezaji bora wa ligi mwezi wa nane kati ya Libasse Gueye na Max Nzengeli

LIBASSE GUEYE
🎯Mechi 5
📌Assist 5
⚽Magoli 1
👋Mchezaji bora wa mechi 3

MAX NZENGELI
🎯Mechi 5
📌Assist 0
⚽Magoli 3

02/09/2026

MZIZE NA DICKSON JOB WABAKIA JOHANNESBURG KWA AJILI YA VIPIMO

Nyota wa Yanga SC, Clement Mzize na Dickson Job, wameondoka Dar es Salaam pamoja na msafara wa timu kuelekea Botswana, lakini safari yao imeishia kwa muda Johannesburg, Afrika Kusini.

Wawili hao wamebaki kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya katika hospitali walikofanyiwa upasuaji awali.

Kwa mujibu wa Ali Kamwe, hakuna haraka ya kuwarejesha uwanjani hadi majibu ya vipimo yatakapothibitisha kuwa wako tayari kurejea kwenye ushindani.

Wakati huo huo, timu ya Yanga SC tayari imewasili salama nchini Botswana kwa ajili ya mchezo dhidi ya Gaborone United utakaopigwa Jumamosi, Septemba 5, saa 2:00 usiku kwa saa za Tanzania.

02/09/2026

✅Golikipa Mputi Jafari hatokuwa sehemu ya kikosi cha Songea United msimu ujao kwa sasa ametimkia ligi kuu Zanzibar katika timu ya Wembe Fc.

01/09/2026

𝗬𝗔𝗙𝗔𝗛𝗔𝗠𝗨 𝗠𝗔𝗕𝗔𝗗𝗜𝗟𝗜𝗞𝗢 𝗠𝗔𝗞𝗨𝗕𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗘𝗡𝗬𝗘 𝗞𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔 𝗬𝗔 𝗦𝗜𝗠𝗕𝗔 𝗞𝗨𝗧𝗢𝗞𝗔 𝗞𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔 𝗬𝗔 𝗭𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗠𝗣𝗔𝗞𝗔 𝗛𝗜𝗜 𝗞𝗔𝗧𝗜𝗕𝗔 𝗠𝗣𝗬𝗔 🦁🔴⚪

-Kuondoa neno mwekezaji na kutamkwa WAWEKEZAJI. (Haijataja idadi ila lazima wawe waeekezaji maana yake kuanzia wawili)

-Muundo wa Bodi ya Wakurugenzi itatokana na wajumbe 8 kutoka Simba SC (51%) na wajumbe 6 kutoka kwa wawekezaji ambao watamiliki 49% miongoni mwao. (SIO MWEKEZAJI MMOJA)

-Mwenyekiti wa Bodi atachaguliwa na wajumbe wa pande zote KUPIGA KURA kwa majina/jina litakalopendelezwa (SIO KUTEULIWA NA MWEKEZAJI) k**a ambavyo ilikuwa awali ambapo kulikuwa na mwekezaji 1.

-Bodi ya Wakurugenzi itaajiri CEO na Sekretarieti, sio k**a ilivyokuwa wakati mwekezaji akiwa mmoja ambapo alikuwa anateuliwa na Mwekezaji Bodi inamuidhinisha.

NB: Usichangie k**a huna/hujaiona Katiba iliyoidhinishwa Februari 2026.

01/09/2026

✅Chilambo Hii ni Mali Safi kabisa, mngoni kwenye viunga vya msimbazi baada ya erasto nyoni kutoka msimbazi haijachukua mda amepatikana mngoni kiraka pia no comment anaenda kupeperusha bendera ya taifa na bendera ya wangoni wa uku songeaaaaa ..

Photos from Tengo online tz's post 01/09/2026

....Nyota wa Tanzania Alphonce Mabula Msanga amemjibu shabiki mmoja aliyecomment kuwa JS Kabilyie wamempa hela nzuri lakini ingekua vizuri zaidi K**a angeenda ulaya na sio kurudi Africa

..Alphonce amerplay hiyo Comments kwa Kusema Kibunda,Kibunda Kaká we Live Once kwa maana ya kwamba pesa ndo imemfanya Alphonce aichague JS Kabliyie na sio timu Nyingine huku akiongeza kwa kusema tunaishi Mara moja..

..Kumbuka Js Kabylie ya Algeria imemlipa kiasi cha $870,000(2.3 Billion) K**a Signing on Fee kwa miaka miwili atakayoitumikia hii timu hii pesa ni Mali ya Mabula kwa maana hakuwa na mkataba na timu yoyote.

.Pia Mabula atakunja mshahara wa $31,000(tsh 81mil) kwa kila mwezi na tayari Kabylie wamemlipa mshahara wote wa mwaka mzima $372000( tsh 983).

..Vipi ingekua wewe hii ofa ungeikataa naamini huwezi tumuache kijana afaidi matunda ya kipaji chake.

..Wakuu Mpira unalipa achaneni na masuala ya kuwapeleka watoto kwenda kusoma a.e.i.o..
u tuwapeleke kwenye shule za vipaji watatusaidia baadae.

Photos from Tengo online tz's post 01/09/2026

✅Waamuzi wa Tanzania Nasir Salum, Mohamed Mkono, Ally Ramadhani na Ahmed Arajiga wameteuliwa na CAF kuchezesha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) JS Saoura (Algeria) vs Horoya AC ( Guinea) utakaochezwa uwanja wa Miloud Hadefi Septemba 4, 2026

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Mbinga
Dar Es Salaam