Mn Boxing Media Tanzania

Mn Boxing Media Tanzania

Share

I'm Gentleman

Karibu kwenye ukurasa bora wa Mchezo wa ngumi nchini Tanzania kwa habari za ndani na Kimataifa hapa ndo nyumbani kwake sisi ni Familia ya Masumbwi.
🇹🇿🇰🇪🇺🇬🇿🇦🇨🇩🇬🇭🇿🇼🇿🇲🇺🇲🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿🇯🇵

25/08/2026

Moja kati ya vitu vinavyowavutia mashabiki wengi wa mchezo wa Masumbwi ni matokeo ya Knockout (K.O) na Technical Knockout (TKO) hasa pale mpambano unapofikia hatua ambayo mmoja kati ya wapinzani wawili anaanguka na kulamba sakafu ya ulingo (Canvas).

Kwa kipindi cha miaka mingi katika tasnia ya mchezo wa Masumbwi hapa nyumbani, mashabiki wamepata kushuhudia mapambano mbalimbali yaliyomalizika kwa Knockout za kutisha, huku baadhi yake yakiwaacha mashabiki wakishikilia vichwa kutokana na ukubwa wa pigo lililomaliza pambano.

Na kwa kweli, k**a si mipango ya Mungu, huenda baadhi ya mabondia waliowahi kuanguka kwenye mapambano hayo tusingekuwa tunawaona leo.

Hapa nimekuletea baadhi tu ya mapambano yaliyomalizika kwa K.O / TKO hatari yaliyowahi kufanyika hapa nyumbani, k**a yanavyoonekana kwenye mpangalio wa video clips hapo chini :

1️⃣ Ibrahim Class 🆚 Gustavo Pina Melgar raia wa Mexico 🇲🇽

📅 30/09/2022

Class alishinda kwa K.O raundi ya 9 kati ya 10.

2️⃣ Joseph Maigwisya 🆚 Hussein Itaba

📅 15/07/2023

Maigwisya alishinda kwa K.O raundi ya 5 kati ya 6.

3️⃣ Juma Choki 🆚 Salim Chazama raia wa Malawi 🇲🇼

📅 26/12/2021

Choki alishinda kwa K.O raundi ya 3 kati ya 6.

4️⃣ Ramadhani Iddi “Bonnie Sellah” 🆚 Ramadhani Kondo

📅 22/10/2023

Bonnie alishinda kwa K.O raundi ya 1 kati ya 8.

5️⃣ Allan Kamote 🆚 Twalibu Mchanjo

📅 31/01/2020

Kamote alishinda kwa K.O raundi ya 4 kati ya 8.

6️⃣ Ally Sewe Jr 🆚 Mohammed Mnemwa

📅 24/01/2025

Sewe Jr alishinda kwa K.O raundi ya 1 kati ya 4.

7️⃣ Ramadhani Mkwakwate 🆚 Isack Chaka

📅 30/08/2025

Mkwakwate alishinda kwa K.O raundi ya 1 kati ya 8.

8️⃣ Amani Bariki 🆚 Hemed Habibu

📅 20/11/2022

Bariki alishinda kwa TKO raundi ya 8 kati ya 8.

9️⃣ Dullah Mbabe 🆚 Francis Cheka

📅 26/12/2018

Dullah Mbabe alishinda kwa K.O raundi ya 6 kati ya 8.

Hizo ni baadhi tu ya Knockout za Hatari zilizowahi kutokea kwenye ulingo kupitia mapambano yaliyofanyika hapa nyumbani.

Je kati ya hizo Knockout 9, ipi unaihesabu kuwa ilikuwa K.O/TKO kali zaidi? Au kuna Knockout nyingine hatari ambayo unadhani ilipaswa kuwepo kwenye orodha hii shusha comment yako familia.

Mn Boxing Media Tanzania

19/08/2026

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Shabani Pazzy maarufu k**a “Dullah Mbabe,” yupo kwenye mbio za kusaka na kuvunja rekodi ya bondia mkongwe na lejendari wa mchezo hapa nchini, Rashid Ally Matumla maarufu k**a “Snake Boy.”

Kwa mujibu wa mtandao wa kuhifadhi takwimu na rekodi za mabondia wote duniani, Rashid Matumla ndiye bondia mwenye idadi kubwa zaidi ya ushindi wa knockout katika historia ya ngumi za kulipwa nchini Tanzania.

Matumla ameshuka ulingoni mara 72, akishinda mapambano 49, ambapo 34 kati ya ushindi huo amepata kwa njia ya knockout's.

Anayemfukuzia kwa ukaribu zaidi ni Dullah Mbabe, ambaye hadi kufikia mwaka huu ana jumla ya mapambano 54, ameshinda 37, huku 32 kati ya ushindi huo akiwa ameyapata kwa njia ya knockout's.

Dullah Mbabe ana nafasi kubwa ya kuifikia rekodi hiyo kwa sababu mbili kuu. Kwanza, bado ni bondia active na anaendelea kucheza mapambano ya ngumi za kulipwa. Pili, aina yake ya uchezaji inampa nafasi kubwa ya kuendelea kusaka zaidi aina ya ushindi wa knockout's.

Dullah ni bondia anayetokea kwenye kundi la staili ya 'Slugger' ajajaaliwa ufundi (Skills) au ujuzi mwingi wa ngumi bali hutegemea zaidi kupiga ngumi kalii nzito nzito zenye nguvu na uwezo wa kumuumiza mpinzani.

Mara nyingi Dullah hupigana akiwa karibu kabisa na zone ya mpinzani (Punching Range) akitafuta nafasi ya kuachia ngumi nzito na kumaliza pambano kabla ya muda wake eyidha kwa njia ya K.O au TKO.

Silaha yake kubwa zaidi ni mkono wa kulia, mkono ambao umewahi kuwaangusha (knockdown) na kuwafanya baadhi ya wapinzani wake wengine washindwe kuendelea na pambano kabisa, akiwemo Francis Cheka, Paulo K**ata, Mada Maugo, Twaha Kiduku (knockdown), Hussein Itaba (knockdown) n.k.

Kwa sasa, Dullah Mbabe amebakiza ushindi wa knockout mbili pekee ili kufikisha jumla ya KO'S 34, sawa na rekodi inayohusishwa na Mkongwe Rashid Matumla “Snake Boy.”

Wazaramo wanasema "Kidile Mwali Kivika" acha tusubiri na tuone 😃.

Mn Boxing Media Tanzania

17/08/2026

Mmoja kati ya wadau na wafuasi wetu pendwa wa kurasa zetu za mchezo wa Masumbwi hapa nchini za Mn Boxing alitutumia ujumbe siku ya leo kuhusu hitaji lake la kutaka kuona pambano kali litakalowakutanisha mabondia mahiri hapa nchini, Nasibu Ramadhani maarufu k**a ‘Pacquiao’ dhidi ya Salim Jengo maarufu k**a ‘Mtango Messi’.

Ujumbe wake huo ulikuwa unasomeka hivi :

“Naomba uwasilishe hili ombi langu kutoka kwa mapromota. Natamani kuwaona mabondia Salim Mtango Messi na Nassibu Ramadhani Pacman kabla hawajamaliza ubora wao kabisa au kuzeeka. Tulione pambano kati yao, hebu gusa hilo familia.”

Ombi hili huenda likawa ni hitaji la wadau wengi hapa nchini ambao kwa hakika wangetamani kuliona pambano hilo, kwani Nasibu na Mtango kiasili wote ni mabondia wenye vipaji halisi katika mchezo huu wa Masumbwi.

NASIBU PACMAN 🔴🥊

Nasibu ni bondia anayetumia mguu wa mbele wa kulia (Southpaw) kiuchezaji jamaa ni Boxer pia ni Counter Puncher mzuri sana, mwenye uwezo wa kucheza kwaku Box ndani na nje, huku akiwa na wepesi wa mwili na uharaka wa mikono.

Mzuri sana katika mashambulizi ya Double Hooks, Combinations, Body Punches na Counter Punching. Pia hutumia vyema mbinu za kujilinda k**a Head Movement, Slip, Bobbing & Weaving na Blocking, vitu vinavyomfanya kuwa bondia hatari ndani ya ulingo.

Baadhi ya mabondia mashuhuri ambao amewahi kuwapiga ni Loren Japhet, Issa Nampepeche, Haidary Mchanjo na Fadhil Majiha.

MTANGO MESSI 🔵🥊

Mtango ni bondia anayetumia mguu wa mbele wa kushoto (Orthodox) anaetokea kwenye kundi la staili ya Boxer Puncher lakini pia ni Counter Puncher mzuri sana, mwenye uwezo wa kucheza kwa Box nakucheza ndani kwa kufuata nakupigana.

Ana nguvu, wepesi mzuri wa mwili nani hatari katika mashambulizi ya Counter Punching, Combinations, Body Punches na Right Overhand.

Kwa upande wa ulinzi Mtango hutumia vyema Head Movement, Slip, Bobbing & Weaving na Blocking ulinzi ambao humsaidia kujilinda na kumfanya kuwa bondia hatari ndani ya ulingo.

Baadhi ya mabondia mashuhuri ambao amewahi kuwapiga ni Loren Japhet, Issa Nampepeche, Cosmas Cheka na Baina Mazola.

Kwako mdau ungependa kuliona pambano hilo likifanyika kati ya Nasibu Ramadhani dhidi ya Salim Jengo shusha maoni yako hapo chini.

Mn Boxing Media Tanzania

15/08/2026

Kwenye video clip hii ni pambano la ndani lililowakutanisha mabondia wa Ghana, Moro Inusah Kanla dhidi ya mpinzani wake Ebenezer Lamptey, pambano ambalo mwisho wake uliwaacha mashabiki midomo wazi kwa mshangao.

Moro na Lamptey walikutana kwenye pambano la utangulizi la raundi 8, katika mapambano ya "The Spirit Fight Night" yaliyofanyika katika ukumbi wa Kalabash Event Complex, Pokuase, Accra, Ghana.

Pambano hilo lilimalizika mapema kwenye raundi ya pili, baada ya Moro Inusah Kanla kuibuka mshindi kwa K.O. Hata hivyo, namna pambano hilo lilivyomalizika iliibua mshangao mkubwa kwa miongoni mwa mashabiki kutokana na mazingira na mbinu zilizotumika katika umaliziaji wa pambano hilo.

Lamptey aliingia kwenye pambano hilo akichukua nafasi ya Stephen Abbey raia wa Ghana ambaye hapo awali ndiye aliyepangwa kuwa mpinzani wa Moro. Lakini baada ya mabadiliko hayo, Lamptey ndiye aliyepanda ulingoni na hatimaye akakutana na matokeo ambayo yaliwafanya aibu waone mashabiki.

Kwako mdau wa masumbwi, wewe umeielewa hiyo K.O? Au Aibu Unaona Wewe. 😃

Mn Boxing Media Tanzania

14/08/2026

Leo nimekuandalia orodha ya mabondia sita wa Tanzania ambao walipata kujitangaza na kupata umaarufu mkubwa kupitia mapambano mbalimbali ya ngumi za kulipwa yaliyokuwa hatua muhimu katika safari zao za kimchezo ambapo baadhi yao walipata umaarufu kupitia ushindi mkubwa, wengine kupitia mapambano yaliyowapa nafasi ya kuonekana zaidi mbele ya mashabiki.

1. HASSANI MWAKINYO JR / Tarehe 08/09/2018 jijini Birmingham nchini England akiwa underdog aliandika historia kwa kumtwanga bondia Sam Eggington wa England kwa TKO kwenye raundi ya pili kati ya raundi 10 ushindi ambao ulimpa umaarufu mkubwa hapa nchini na kumfungulia milango ya mapambano makubwa ya ndani naya kimataifa nakupata pia fursa za kibiashara.

2. TWAHA KIDUKU / Tarehe 28/08/2020 alikutana na Dullah Mbabe katika pambano la marudiano la pili la raundi 10 ambalo Twaha aliibuka mshindi kwa pointi ushindi ambao ulimpa umaarufu mkubwa zaidi nchini kwa kumfungulia fursa za kibiashara na kupata mapambano makubwa ya ndani naya kimataifa hapa nchini.

3. MFAUME MFAUME / Tarehe 5/02/2017 alipata nafasi ya kupanda ulingoni kwenye jukwaa kubwa ambapo alikutana na bondia Mohammed Matumla katika pambano la raundi nane na Mfaume akaibuka mshindi kwa matokeo ya TKO kwenye raundi ya saba ushindi ambao ulimpa umaarufu mkubwa wakujulikana nakupata fursa ya mapambano ya ndani na kimataifa hapa nchini.

4. SAID BWANGA / Tarehe 24/03/2023 akiwa na muda mfupi wa maandalizi alipambana na Emmanuel Mwakyembe katika pambano la raundi 8 lililoishia kwa sare lakini kiwango alichoonyesha kilimpa umaarufu na kumfungulia milango ya mapambano makubwa ya ndani.

5. KARIMU MANDONGA / Tarehe 26/03/2022 alipoteza kwa TKO kwenye raundi ya kwanza dhidi ya Christopher Magambo lakini pambano hilo likawa ndo mwanzo wa umaarufu wake mkubwa kwa haiba, kauli na namna yake ya kujitangaza vilimfanya kuwa kipenzi cha mashabiki na kupata fursa nyingi za kibiashara na mapambano.

6. JUMA CHOKI / Tarehe 15/09/2019 alikutana na mpinzani wake Emmanuel Mwakyembe katika pambano la raundi 8 ambalo Choki alionyesha kiwango kikubwa na kuibuka mshindi kwa pointi, ushindi ambao ulimpa umaarufu na kumfungulia milango ya mapambano makubwa ya ndani naya kimataifa.

Mn Boxing Media Tanzania

12/08/2026

Bondia wa ngumi za kulipwa mwenye uraia wa Ivory Coast na Ufaransa, Michel Soro ambaye ni Bingwa wa Dunia wa IBO katika uzani wa Middleweight kg 72.5 amesema amepanga kuwapa nafasi mabondia kutoka Tanzania kushiriki katika mapambano anayoyaandaa barani Afrika.

Soro alijulikana zaidi nchini Tanzania baada ya kumshinda bondia Mtanzania Hassani Mwakinyo Jr katika pambano la ubingwa wa Dunia wa IBO lililofanyika nchini Ivory Coast tarehe 10 Juni 2026.

Baada ya kupita takribani miezi miwili tangu pambano hilo MN Boxing Media ilipata nafasi ya kuwasiliana na Michel Soro mmoja wa mabondia wanaotambulika Duniani ili kupata mtazamo wake kuhusu maendeleo ya mchezo wa ngumi barani Afrika pamoja na mchango anaotarajia kutoa kwa mabondia wa Tanzania.

Soro, ambaye pia anajihusisha na uandaaji wa mapambano kupitia Dream Ring Promotion, alisema :

“Kwanza kabisa, ningependa kusema kwamba nimeugundua Tanzania kuwa ni nchi ya ajabu yenye mabondia wakubwa na mahiri.

Hakika Tanzania ina mabondia wazuri sana.
Mimi ni bondia, lakini pia ninafanya shughuli za kuandaa mapambano ya ngumi katika bara la Afrika. Tayari nimepanga kuanza kuwapa nafasi mabondia wa Tanzania kupigana katika matukio ninayoyaandaa.

Katika usiku wa mapambano unaofuata, nitamshirikisha Amiri Matumla, kwa sababu licha ya kupoteza pambano lake, ameonyesha kwamba ni bondia mwenye kipaji, hasa ukizingatia umri wake mdogo nina amini kwamba ana mustakabali mzuri sana mbele yake.

Afrika imejaa vipaji vya kweli. Kinachohitajika ni kuwapatia mfumo mzuri wa maendeleo na kuwafanya wapate nafasi ya kupigana mara kwa mara.

Kupitia mfumo wetu wa Dream Ring Promotion, tutaendelea kuandaa mapambano mara kwa mara na kuwapa nafasi zaidi mabondia wa Afrika kushiriki. Nina hakika kwamba ndani ya miaka michache ijayo, tutazalisha mabingwa wa dunia kutoka Afrika.

Kwa mabondia, ushauri ambao ningependa kuwapa ni kwamba wajitoe kikamilifu katika mazoezi. Kazi na kazi zaidi, bila kuchoka kutafuta namna ya kuendelea kuboresha uwezo wao.

Matokeo mazuri yatafuata.”

Ujumbe wa Michel Soro unaongeza matumaini mapya kwa mabondia wa Tanzania, hasa kwa wale wanaotafuta fursa za kupanda katika viwango vya kimataifa.

Mn Boxing Media Tanzania

12/08/2026

Uzani wa Lightweight kg 61.2 miongoni mwa uzani ambao mpaka kufikia mwezi Agosti 2026 umeendelea kuwa na ushindani mkubwa na mkusanyiko wa mabondia wengi maarufu na wakali nchini Tanzania.

Miongoni mwa majina yanayopatikana katika uzani huu ni Juma Choki, Salim Mtango, Said Bwanga, Said Chino, Said Mkola, Francis Miyeyusho, Ahmed Pelembela, Bonnie Sellah na Salim Hussein Shella huku kila mmoja akiwa na historia na rekodi yake katika mchezo wa ngumi za kulipwa.

Hata hivyo kwa mujibu wa viwango vya BoxRec mtandao unaohifadhi takwimu na rekodi za mabondia wote duniani Gabriel Morris Gervas maarufu k**a 'Gabby' ndiye bondia anayeshikilia nafasi ya juu zaidi katika orodha ya mabondia wa Tanzania kwenye uzani wa Lightweight.

Kinacho mtofautisha Gabriel katika orodha hii ni daraja lake la nyota ambapo ana nyota 3 kamili ⭐⭐⭐ kiwango ambacho hakijafikiwa na bondia mwingine yoyote aliyekuwepo kwenye Top 10 hiyo hapo chini.

Nusu nyota : ✨

1. Gabriel Morris Gervas
Rekodi : Ushindi : 12 | KO'S : 8 | Kupoteza : 2 | Sare : 0
Hadhi : ⭐⭐⭐

2. Said Bwanga
Rekodi : Ushindi : 9 | KO'S : 4 | Kupoteza : 2 | Sare : 2
Hadhi : ⭐⭐✨

3. Tano Juma
Rekodi : Ushindi : 8 | KO'S : 2 | Kupoteza : 1 | Sare : 2
Hadhi : ⭐⭐✨

4. Juma Choki
Rekodi : Ushindi : 12 | KO'S : 4 | Kupoteza : 1 | Sare : 1
Hadhi : ⭐⭐✨

5. Salim Shella
Rekodi : Ushindi : 9 | KO'S : 3 | Kupoteza : 0 | Sare : 0
Hadhi : ⭐⭐✨

6. Salim Jengo
Rekodi : Ushindi : 22 | KO'S : 13 | Kupoteza : 5 | Sare : 1
Hadhi : ⭐⭐✨

7. Yahya Abdallah
Rekodi : Ushindi : 6 | KO'S : 4 | Kupoteza : 0 | Sare : 0
Hadhi : ⭐⭐

8. Luqman Kimoko
Rekodi : Ushindi : 9 | KO'S : 2 | Kupoteza : 1 | Sare : 3
Hadhi : ⭐⭐

9. Kato Machemba
Rekodi : Ushindi: 14 | KO'S : 10 | Kupoteza : 4 | Sare : 0
Hadhi : ⭐⭐

10. Said Chino
Rekodi : Ushindi : 25 | KO'S : 16 | Kupoteza : 14 | Sare : 2
Hadhi : ⭐⭐

Mabondia k**a Said Mkola anashika nafasi ya 15 Ahmed Pelembela nafasi ya 22 huku Francis Miyeyusho na Bonnie Sellah wakishika nafasi ya 24 na 25 uzani wa Lightweight mboga moto ugali moto ukija kichwa hutoboi.

Mn Boxing Media Tanzania

10/08/2026

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Mafia maarufu k**a 'Mafia Tank' amemshusha kwa mda bondia Fadhil Majiha maarufu k**a 'Stopper' aliyekuwa kinara wa mizani yote kirekodi hapa nchini (Pound For Pound) kwa mujibu wa mtandao wa kuhifadhii data na rekodi za mabondia wote Duniani (Boxrec).

'Pound Of Pound' maana yake ni mtiririko unaojumuisha mabondia bora kirekodi kwenye viwango vya madaraja yote ya uzito wanaocheza mabondia iwe kwenye ngazi ya nchii, bara au dunia nzima kwa kuanzia kiwango cha chini kabisa cha uzito wa minimumweight kg 48 mpaka uzito wa mwisho wa heavyweight kwenye mchezo wa ndondi na kinacho angaliwa zaidi kwenye upande wa boxrec ni point nyingi alizonazo bondia husika, hadhii na nafasi.

Japo list za Pound for Pound zinazo heshimika zaidi duniani ni list kutoka kwenye viwango vya mikanda mikubwa duniani yani WBC, WBA, WBO na IBF na mashirika ya Ring Magazine, Transnational Boxing Rankings Boards na ESPN ila kwa vile sisi bado hatujafanikiwa kufika kwenye hatua hiyo huwa list ya Pound for Pound kwa mabondia wote kiujumla tunaiyangalia kupitia mtandao wa Boxrec ambapo kwa sasa bondia anayeshika nafasi ya kwanza ni Ibrahim Mafia.

Ambapo ushindi wake wa Julai 30, 2026 kwenye pambano la kimataifa nala Ubingwa wa WBC international Silver dhidi ya Samuel Laryea raia wa Ghana umempandisha kinafasi kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye uzani wa Bantamweight kg 53 uzani ambao yeye na Majiha wanacheza nakupata pia Nyota 4 kamili huku akichukua kijiti hicho kutoka kwa bondia Majiha ambaye amekuwa bondia kinara kwenye mizani yote toka mwaka 2023 japo januari mwaka huu aliwahii kushushwa kwa mda na bondia Salmin Kassimu kisha akarudi tena wenye nafasi yake.

Lakini kwenye kiti hicho Ibrahim amekaa kwa mda huku wadau wa mchezo wa Masumbwi wakisubiria matokeo ya pambano la Majiha alililocheza Visiwani Zanzibar Julai 31, 2026 ya ingizwe naya someke ambapo alimchapa bondia Nassoro Madimba kwa matokeo ya RTD kwenye raundi ya tatu kati ya nane ili tupate kumuona kinara rasmii wa mizani yote hapa chini.

K**a Ibrahim atamshusha rasmii Majiha au Majiha atarudi kwenye uskani nakuendelea kubaki kwenye nafasi yake kiti bado cha moto Your Better Watch Your Back.

Mn Boxing Media Tanzania

09/08/2026

Bondia wa ngumi za kulipwa mwenye asili ya Tanzania Bruno Tarimo maarufu kwa jina la "Bruno Vifua Viwili” usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kushinda pambano lake la kimataifa nala ubingwa nchini Australia.

Bruno amefanikiwa kushinda pambano la kimataifa la raundi 10 ubingwa wa WBA Oceania katika uzani wa Featherweight kg 57 kwa uamuzi wa pointi wa Majaji wote watatu dhidi ya bondia Jun-Lin Zhao raia wa China lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Coongatta jijini Queensland nchini Australia.

Matokeo ambayo yamemfanya Bruno kuandika kumbukumbu ya kihistoria inayojirudia katika safari yake ya ngumi za kulipwa kwani itakumbukwa kuwa tarehe 24/03/2018 Bruno kabla ya kubadili Uraia aliwahi kutwaa mkanda wa WBA Oceania katika uzani wa Super Featherweight kg 59 kwa kumpiga bondia Billel Dib raia wa Australia nchini humo.

Ushindi ambao ulimpa nafasi nafasi ya kuaminiwa na hatimaye kupata fursa ya kwenda nchini Australia kwa ajili ya kujiendeleza na kusimamiwa kikazi kwenye safari yake ya mchezo wa ngumi na tangu wakati huo Bruno amekuwa na mafanikio mbalimbali katika ngumi za kulipwa akifanikiwa kutwaa mikanda kadhaa ya ubingwa inayotambulika Duniani.

Licha ya kuwa sasa ni raia wa Australia Bruno bado anahesabika ni miongoni mwa mabondia wenye asili ya Tanzania walioingia katika vitabu vya historia kwa kutwaa au kushikilia mikanda ya ubingwa inayotambulika kimataifa na Duniani kiujumla kwa nnje ya mipaka ya Tanzania.

Na hapo nimekuwekea mabondia hao wengine na nchini ambazo walizowahii kutwaa mikanda hiyo :

Ibrahim Class bingwa wa WBC International Silver (Thailand)

Mbwana Matumla bingwa wa zamani wa Dunia wa IBO (South Africa)

Dullah Mbabe bingwa wa zamani wa WBO Asia Pacific (China)

Lupakisyo Shoti bingwa wa IBO International (Romania)

Hassani Mwakinyo Jr bingwa wa zamani wa WBA Pan Africa (Botswana)

Fadhil Majiha bingwa wa zamani wa WBA Pan Africa (South Africa)

Tony Rashid bingwa wa zamani wa ABU (South Africa)

Abdul Ubaya bingwa wa zamani wa WBA Asia (Thailand)

Cosmas Cheka bingwa wa zamani wa WBO Asia Pacific (Thailand)

Hongera Bruno Tarimo historia na mazuri uliyobeba kwenye mchezo wa ndondi nchini Tanzania yataendelea kukumbukwa.

Mn Boxing Media Tanzania

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Website

Address


Mabibo
Dar Es Salaam