20/07/2026
KWA MAMA WOTE WANAOLEA WATOTO PEKE YAO (SINGLE MOTHERS) … TAFADHALI MSIKATE TAMAA NA WATOTO WENU. ❤️🥹
Mvulana mdogo aliye kwenye picha hizi alilelewa na mama yake mzazi ambaye hakuwahi kukata tamaa, hata pale maisha yalipompa sababu nyingi za kufanya hivyo.
Kutana na Sheila Ebana, mwanamke shupavu aliye nyuma ya mafanikio ya supastaa wa soka, Lamine Yamal.
Sheila, ambaye anatokea Equatorial Guinea, alihamia nchini Hispania akitafuta maisha bora. Alikuwa mama kijana wakati Lamine alipozaliwa mwaka 2007.
Baada ya kutengana na baba wa Lamine alipokuwa na takribani miaka mitatu, Sheila alichukua jukumu kubwa la kumlea mwanawe, akifanya kazi mbalimbali ili kupata chakula na kumsaidia mwanawe kufuatilia ndoto yake ya kucheza soka.
Pesa zilikuwa chache. Maisha yalikuwa magumu. Lakini hakuruhusu changamoto za maisha ziwe sababu ya kuacha kumuamini mwanawe. Alimtia moyo, alimuunga mkono na kuhakikisha anaendelea kufuatilia mapenzi yake ya soka.
Leo, yule mvulana mdogo amekuwa bingwa wa Kombe la Dunia la FIFA na mmoja wa vipaji bora zaidi vya vijana katika historia ya soka. Akiwa na umri wa miaka 19 tu, wengi tayari wanaamini kuwa ana uwezo wa kuwa miongoni mwa wachezaji wakubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya soka.
Kwa hiyo, kwa kila mama anayelea mtoto peke yake: Changamoto unazopitia leo haziamui maisha ya baadaye ya mtoto wako. Endelea kumpenda. Endelea kumuamini. Endelea kumuombea.
Mafanikio yako makubwa zaidi huenda yasiwe tu maisha unayojijengea wewe mwenyewe, bali pia maisha unayomwezesha mtoto wako kuyafikia.
Leo dunia inamshangilia Lamine Yamal… lakini nyuma ya kila makofi na pongezi, kuna mama ambaye kujitolea kwake kulifanya jambo lililoonekana kuwa haliwezekani liwezekane. ❤️🙌🏽
19/07/2026
Rodri amecheza vizuri na amepiga pasi nyingi, hilo halina ubishi… lakini Messi amefanya mengi zaidi katika kuibeba timu yake. 🔥
Messi alikuwa na takwimu nzuri karibu kila idara — magoli, assists, pasi muhimu na mchango mkubwa kwenye ushindi wa timu yake. 🐐🇦🇷
Lakini leo wamempa Rodri tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano! 😭💔
🤔 WADAU, kwa upande wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano…
Mko upande wa Rodri au Messi? 👀
Kwa upande wangu, Messi alistahili tuzo hiyo kwa asilimia 100 bila hata ya mashaka.
14/06/2026
SIMBA SC YAZIDI KUONESHA UBORA — ISHARA YA “BINGWA AJAYE?”
Simba SC imeendelea kuonyesha kiwango cha juu sana uwanjani, ikionyeshabishara za kuwa ndiyo bingwa ajaye wa ligi Kuu NBC kutokana na mchezo wake wa leo dhidi ya Pamba jiji.
Katika mchezo huo, Simba ilitawala vipindi vingi vya mchezo, ikitengeneza nafasi kadhaa muhimu za kufunga. Hata hivyo,uamuzi wa mwamuzi umewagharimu Simba nafasi mbili za wazi, ikiwemo nafasi ya wazi ya Mpanzu pamoja na tukio lingine ambalo Naliona lilistahili penalti dakika za mwisho Mwamuzi kawanyonga.
Licha ya kushinda lakini uamuzi huo umeathiri matokeo Kwa sababu Simba Ilistahili kushinda hata Mabao Matano, licha ya kuonyesha kiwango bora uwanjani.
Kwa upande wa uchezaji, Simba imeonekana kuwa na Umiliki mzuri wa mpira, Mashambulizi ya haraka na ya hatari, Nidhamu ya kiufundi ya hali ya juu, Wachezaji kuonyesha ubora binafsi, hasa kwenye eneo la mwisho.
Kwa kiwango hiki,Simba inaendelea kujijenga k**a timu yenye uwezo mkubwa wa kutwaa ubingwa msimu huu.
Swali kubwa linalobaki ni moja: Je, kuna timu inayoweza kuizuia Simba k**a itaendelea kucheza hivi?
12/06/2026
Juzi kati Niliona kaimu mkurugenzi wa TBC Akisema Hawa wanaomiliki Visimbimbuzi huwa wanawaminyia quality sio haki kwa sababu wao Huwa hawana camera wote wanapokea matangazo na alisema jambo Hilo wamelilalamikia sana TCRA
Kwa kawaida wauzaji wa matangazo ya Kombe la Dunia FIFA Huwa wanatoa LINK ambayo wote mnaipata moja ndio maana ikikata kwa mrusha matangazo mmoja lazima wote mpotee hewani kwa ukanda huo.
Suala la ubora wa picha linategemeana na mambo mawili makubwa…! Picha yenu mnayopokea mnaitoaje au wamiliki wa ving’amuzi wataminya au kufifiisha picha kwa kiwango gani.
Wengi wamekuwa wakishangaa ubora wa matangazo ya Kombe la Dunia kwenye televisheni hasa TBC Pale wanapoona ipo chini. Hapa kuna ufafanuzi:
1️⃣ FIFA / Wamiliki wa Matangazo
Hawa ndio wenye haki halisi za matangazo.
Wanaamua ubora wa picha, codec na kiwango cha compression kabla matangazo hayajafika kwenye televisheni na wao ndio wanapanga Michezo ipi ionyeshwe Bure hasa kwenye channel za Taifa.
2️⃣ Televisheni za Taifa (TBC, UBC, KBC, SABC)
Hawana kamera zao wala hawatengenezi matangazo moja kwa moja LIVE.
Wanapokea link ya matangazo kutoka kwa wamiliki wa hakimiliki na kuonesha tu kile kilichotumwa.
Ubora wa picha unategemea wamiliki wa matangazo, si televisheni za taifa. Pia wanapangiwa na FIFA Michezo ya kuonyesha.
3️⃣ Providers wa Decoders (Wenye Visimbimbuzi na wengine)
Hawa ndio wanaominya ubora kwa upande wa package za viewers.
Wanaweza kufifiisha picha, kuweka watermark, au kupunguza ubora kwenye package ya chini ili kulinda maslahi yao ya kibiashara.
Hivyo, ukiangalia ubora mdogo kwenye TV yako ya satellite/cable, hii ni kwa sababu ya provider, si TBC au FIFA. Hawa kwakuwa wananunua haki za Matangazo Huwa wanaonyesha Michezo yote.
📌 TBC na televisheni za taifa ni wasambazaji tu, hawana udhibiti wa ubora wa awali na pia wanapangiwa Michezo ya kuonyesha Bure.
Lakini mpaka sasa watu huwa Wana Kariri wakisema Camera za TBC sio Kali hawajui kitu Kuwa TBC Wala hao wenye Ving'amuzi Huwa hawana Camera yeyote huko Wala kuamua Quality ipi pale wao Huwa wanapewa link na wenye Haki za Matangazo lakini Kuna hujuma Huwa wanazipata.
11/06/2026
"Unapoulizwa uraia wako, unajibu kuwa wewe ni Mtanzania. Lakini kwa nini baadhi ya watu kutoka Zanzibar hujitambulisha kwanza k**a Wazanzibari badala ya Watanzania, wakati Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuunda Tanzania?
Ukweli ni kwamba Zanzibar ilikuwa taifa lenye mamlaka yake kabla ya Muungano wa mwaka 1964. Ndiyo maana wengi wao bado wanajivunia utambulisho wao wa Kizanzibari sambamba na Utanzania wao. Kwa upande wa Tanganyika, ilifutwa baada ya Muungano, jambo ambalo limefanya utambulisho wake kupungua kadri miaka ilivyopita.
Kwa mtazamo wangu, lengo la mwisho la Muungano lilipaswa kuwa kuwa na serikali moja ya Tanzania. Hata hivyo, hadi leo bado kuna mfumo wa serikali mbili, jambo linaloendelea kuibua mijadala kuhusu mustakabali wa Muungano.
Tukiiangalia Marekani, majimbo mengi yaliungana na kuunda taifa moja lenye serikali kuu, huku kila jimbo likiwa na mamlaka ya kujisimamia katika maeneo mbalimbali. Wananchi wake wanajivunia majimbo yao, lakini mbele ya yote wanajitambulisha k**a Wamarekani.
Hoja ambayo Haji Manara ameizungumza inaibua mjadala muhimu. Tanganyika ilijifuta ili kuunda Tanzania kwa nia njema ya kuimarisha Muungano. Wapo wanaoamini kwamba k**a lengo lilikuwa kuwa na taifa moja lenye utambulisho mmoja, basi mfumo ungepaswa kuelekea kwenye serikali moja ili kuondoa mijadala ya mara kwa mara kuhusu pande mbili za Muungano.
Hata hivyo, hili ni suala la kisera na kikatiba linalohitaji mjadala mpana wa kitaifa, kwa kuzingatia historia, maslahi na makubaliano yaliyounda Muungano wenyewe, tutakapoanza mchakato wa katiba mpya tunapaswa kupitia upya Muundo wa Muungano wetu ili panapo lalamikiwa pawekwe sawa.
10/06/2026
John Heche, hoja yako inaonekana kupuuza uhalisia wa muundo wa Muungano. Kumbuka kuwa zipo Serikali mbili zinazotambulika kikatiba: Serikali ya Tanzania na Serikali ya Zanzibar. Kila Mzanzibar ni Mtanzania, lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar.
Kinachozungumziwa hapa ni suala la maslahi na haki za Wazanzibari ndani ya mamlaka yao. Afya si jambo la Muungano, hivyo Serikali ya Zanzibar ina mamlaka ya kuweka na kusimamia sera zake katika sekta hiyo kwa mujibu wa sheria zilizopo.
Badala ya kuwalaumu viongozi wanaotekeleza sheria, ni vyema kuelekeza hoja kwenye marekebisho ya sheria hizo k**a unaona zina mapungufu. Wanaotekeleza sheria hawapaswi kulaumiwa kwa kufuata mfumo uliowekwa kisheria.
Aidha, Zanzibar ina taasisi zake na majukwaa yake ya kujadili masuala yanayowahusu Wazanzibari. K**a Watanganyika wanahitaji jukwaa maalum la kujadili masuala yao kwa namna hiyo, basi mjadala wa kuirejesha au kuipa nguvu Tanganyika unaweza kufunguliwa kwa uwazi.
Wazanzibari wengi wanajivunia utambulisho wao wa Kizanzibari sambamba na ule wa Kitanzania. Hivyo, si sahihi kila mara kutafsiri utetezi wa maslahi ya Zanzibar k**a ubaguzi. Kila upande una haki ya kujadili na kulinda maslahi yake ndani ya mfumo wa Muungano uliopo.
17/01/2025
"Kuna Sauti Ina niambia kwamba Yanga Watabakia Wanalia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Kesho, Hii ni Dalili ya MC ALGER kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Huenda Safari ikafika Tamati Kesho"
21/12/2024
WALLACE KARIA AONGOZE TFF HADI KIFO
Laiti ningekua na uwezo ningeweza kumbakiza Wallace karia aendelee kusimamia changamoto za soka hapa Tanzania naaamini ipo siku angezimaliza kabisa.
Katika kipindi chake amefanya makubwa kwenye soka la Tanzania hata ambae haoni basi ni kipofu, Tanzania tuko mbali kidogo japo bado juhudi zinahitajika lakini watu k**a hawa huwa hawajirudii.
hapa ushabiki ni pembeni uhalisia lazim uchukue mkondo wake, Mafanikio ya Mpira yaliyopatikana Katika utawala wake kuanzia Katika Vilabu na Timu ya Taifa kufuzu AFCON mara tatu mfululizo Hilo sio jambo Dogo Lazima apewe Maua yake, Tunatakiwa kufanya maandamano ya amani kushinikiza Wallace Karia awe Rais wa kudumu TFF Ndugu zangu aminini kwamba tutaenda kubaya baada ya Karia
Huyu baba amefanikiwa kupeleka timu mbili robo fainali klabu bingwa, katika utawala wake Yanga pia imefika Mpaka Fainali ya kombe la Shirikisho siyo jambo jepesi
Katika Msafara wa Mamba Hata kenge wapo kwahiyo Hakuna Mtu anayependwa na Watu wote Hata ufanye Nini Lazima uchukiwe na Watu
All In All k**a Kuna Uwezekano Karia aongezewe Muda Hata k**a katiba inasema Muda wake umeisha ifanyiwe marekebisho atawale Mpaka kifo
23/09/2024
JE HUYU KAKA KUCHELEWA KUPATA MAFANIKIO DHIDI YA MDOGO WAKE NI KUBWA JINGA?
"Kaka alizaliwa Mwaka 1935 Mwaka Mmoja Baadae Mdogo wake Naye Akazaliwa ikabidi kaka amuachie Ziwa Mdogo wake
Baada ya Miaka Kadhaa Mdogo wake alipata Mafanikio Zaidi hasa kwenye Anga ya Kimataifa Huku Kaka yake akisubiri Miaka zaidi ya 88 kufikia Mafanikio ya Mdogo wake kwenye Anga ya Kimataifa
Kitu Cha ajabu Baada ya kaka Kuanza Nae kung'aa Kimataifa akaanza kumzodoa Mdogo wake kuwa amechukua Muda Mchache zaidi kukaribia Mafanikio ya Mdogo wake hakumbuki yeye Ndie aliyemuachia Ziwa Mdogo wake na yeye Ndie alipaswa kuwa mstari wa mbele kumuonyesha Njia ya Mafanikio Mdogo wake!!!
Je Huyu kaka Ni Kubwa jinga? Miaka 88 alikuwa wapi muda wote kuyafikia Mafanikio ya Mdogo wake??
Bila kuwa na "D 2" Huwezi Kuelewa 😀
22/09/2024
MASHABIKI WA YANGA MNA MATATIZO GANI?
Licha ya Kuwa na Uongozi Imara Engineer Hersi Said na Arafat Haji Chini ya Udhamini wa Muwekezaji Gharib Said Mohamed (GSM) ambao Umeifanya Yanga kuwa Moja ya Timu Tishio kukutana nayo Barani Afrika lakini Bado Mashabiki wa Yanga hawaonekani Kuisapoti Timu Yao Asilimia 100% Hasa Kwenda Uwanjani
Unadhani Mashabiki wa Yanga wana matatizo Gani kwanini hawapendi kwenda Uwanjani? Uwanja Mdogo k**a New Aman Complex Mashabiki wameshindwa Kuujaza Full House
Mashabiki wa Yanga mnataka Nini 😢