Swahili MEDIA

Swahili MEDIA

Share

🔴 HABARI, MATUKIO NA MICHEZO
🟢 MAWASILIANO PIGA:0713114698
🔵

17/08/2026
17/08/2026

Mkazi wa [kusafisha koo] mtaa wa Ramishye katika manispaa ya Bukoba Frank Stanley anapigania maisha yake katika hospitali ya rufaa ya kanda Bugando jijini Mwanza kufuatia kile kinachodaiwa kuwa ni kupigwa vibaya na kupoteza fahamu akiwa mikononi mwa jeshi la polisi.
Kwa mujibu wa taarifa Stanley amelazwa katika wodi namba sita tangu Agosti 8, 2026 huku ndugu zake wakieleza kuwa hali yake kiafya bado ni mbaya.

Baba mzazi wa Frank Stanley Stanley Ndibalema Shurazi anasema tangu mwanawe alipok**atwa na askari polisi Julai 30 mwaka 2026 familia imekuwa ikipitia wakati mgumu na kuteseka kisaikolojia.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Blasius Chatanda amethibitisha kuk**atwa kwa kijana huyo,Chatanda ameeleza kuwa Stanley alik**atwa na makachero wa polisi kufuatia tuhuma za kuhusika na matukio ya wizi. Hata hivyo kuhusu tuuma za kuteswa na kujeruiwa vibaya akiwa mahabusu,Kamanda huyo anasema shauri hilo kwa sasa linashughulikiwa na mamlaka husika.

17/08/2026

Hali ya taharuki imejitokeza katika Mtaa wa Madukani, Kata ya Sokoni, jijini Arusha, baada ya mtoto mwenye umri wa miaka minane, Karen Michael, kugongwa na pikipiki katika barabara inayoelekea Paloti.

Tukio hilo limeibua hasira kwa wananchi wa eneo hilo, ambao wamedai kuwa barabara hiyo imekuwa ikihusishwa na ajali mara kwa mara, hali inayowahatarisha watembea kwa miguu, hususan watoto.

Kutokana na hali hiyo, wananchi wameamua kufunga barabara hiyo na kukaa njiani wakishinikiza mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kwa kuweka matuta (bumps) ili kupunguza mwendo wa magari na pikipiki na kuzuia ajali zaidi.

16/08/2026

Mtoto wa miaka saba,

mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule moja ya msingi iliyopo kijiji cha Sokon II, wilayani Arumeru mkoani Arusha, anadaiwa kubakwa na mwanaume mmoja maarufu babuu ambaye ni mlinzi wa shule moja ya sekondari katika eneo hilo.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Agosti 2, 2026, baada ya mtoto huyo kwenda katika shule hiyo iliyopo jirani na nyumba yao hivyo alikuwa akiwafuta ndugu zake wanaosoma hapo.

16/08/2026

MTOTO mwenye umri wa miezi minne ametelekezwa katika kituo kidogo cha magari ya abiria yanayosafiri kutoka Babati kuelekea Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara.
Mtoto huyo anadaiwa kutelekezwa na abiria mmoja aliyedai kuwa anatokea Arusha na kuelekea Mwanza, ambapo alimkabidhi mtoto huyo mama mmoja mjasiriamali Glory Lazaro aliyekuwa akifanya biashara ya kuuza bidhaa mbalimbali katika kituo hicho.

Kwa mujibu Glory Lazaro, tukio hilo limetokea majira ya saa kumi jioni, Agosti 15, 2026, ambapo abiria huyo alimuachia mtoto na kuendelea na safari bila kurejea.

Glory amesema hali hiyo imemweka katika mazingira magumu, kwani tayari ana watoto watano anaowahudumia, hivyo ameiomba Serikali pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kumsaidia katika malezi na mahitaji ya mtoto huyo.

16/08/2026

Hali ya taharuki imejitokeza katika Mtaa wa Madukani, Kata ya Sokoni, jijini Arusha, baada ya mtoto mwenye umri wa miaka minane, Karen Michael, kugongwa na pikipiki katika barabara inayoelekea Paloti.

Tukio hilo limeibua hasira kwa wananchi wa eneo hilo, ambao wamedai kuwa barabara hiyo imekuwa ikihusishwa na ajali mara kwa mara, hali inayowahatarisha watembea kwa miguu, hususan watoto.

Kutokana na hali hiyo, wananchi wameamua kufunga barabara hiyo na kukaa njiani wakishinikiza mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kwa kuweka matuta (bumps) ili kupunguza mwendo wa magari na pikipiki na kuzuia ajali zaidi.

Kwa sasa, wananchi hao wanaendelea kuwepo barabarani wakisubiri mamlaka kuchukua hatua kuhusu kilio chao.

15/08/2026

Mtoto wa miaka saba, mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule moja ya msingi iliyopo kijiji cha Sokon II, wilayani Arumeru mkoani Arusha, anadaiwa kubakwa na mwanaume mmoja maarufu babuu ambaye ni mlinzi wa shule moja ya sekondari katika eneo hilo.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Agosti 2, 2026, baada ya mtoto huyo kwenda katika shule hiyo iliyopo jirani na nyumba yao hivyo alikuwa akiwafuta ndugu zake wanaosoma hapo.

15/08/2026

Baada ya tukio lililotokea kwenye geti la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,la vijana watatu kudaiwa kupotea njia walipokuwa wakielekea Babati kwa ajili ya msiba ambapo walikutana na askari watatu wanaodaiwa kuwapa adhabu kali huku mmoja wao akipoteza maisha.

SWAHILI MEDIA imefika eneo hilo na kufanikiwa kumpata Ashura Moses ambaye alishuhudia tukio hilo wakati akiendelea na biashara yake ndogo ndogo karibu na geti hilo amesema,Vijana hao walikuwa watatu na walikuwa wamepanda pikipiki moja na kuingia katika barabara ya kuelekea Ngorongoro.

Aidha shuuda ameiele SWAHILI MEDIA kuwa aliowao askari wawili wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro pamoja na askari mmoja wa jeshi la polisi wakiwasimamisha vijana hao kwa kufunga geti na kuwachukua vijana hao na kuwapeleka asipojua yeye.

Kwa upande mwingine amesema hakuweza kusikia mazungumzo yao sababu yeye alikuwa mbali kidogo k**a mita 15 hivyo alichokiona ni askari hao walizima pikipiki ya vijana ghafla na kuiburuza.

14/08/2026

Vijana mbalimbali wamejitokeza katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha, kwa ajili ya kumuaga na kumsindikiza katika safari yake ya mwisho kijana mwenzao aliyefariki dunia siku mbili zilizopita katika tukio lililotokea eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Kijana huyo alikuwa akisafiri pamoja na wenzake wawili kuelekea Babati kwa ajili ya kuhudhuria msiba, lakini walipoteza njia na kuelekea upande wa Ngorongoro. Wakiwa katika eneo hilo, walikutana na tukio lililosababisha kifo cha kijana huyo, huku wenzake wawili wakijeruhiwa.

Leo, mwili wake umefanyiwa taratibu za kuuaga katika Hospitali ya Mount Meru, kabla ya kusafirishwa kwa ajili ya mazishi katika eneo analotoka.

Vijana wenzake wameeleza uchungu mkubwa kutokana na kifo chake, huku wakilaani kile walichodai kuwa ni kitendo cha kikatili dhidi ya mwenzao na kuhoji sababu zilizofanya kijana huyo kupoteza maisha kwa namna hiyo.

14/08/2026

ASKARI WA ARUSHA AONGEA KWA BUSARA MAKABURINI MAZIKO YA KIJANA ALIYEUAWA NA ASKARI, POLISI NI RAFIKI

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Arusha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Arusha