Kothbiro KE

Kothbiro KE

Share

Kothbiro is Kenya's biggest offseason football tournament that started in the1970s.

28/08/2026

*STATEMENT YA MWANAHABARI NA FORMER FOOTBALLER WA TOYOYO - KWA WAKAAZI WA ZIWANI*

Mimi ni mkaazi wa Ziwani na mwanahabari ambaye nimechezea Camp Toyoyo, Jericho.

Nimeona maendeleo na vita ya Toyoyo.

Toyoyo ilijengwa na turf na Mheshimiwa Bernard Mutura - mzaliwa wa Bahati aliyecheza hapo mguu tupu. Ilikua mega project kwetu. Ilihost KPL, World Cup Trophy Tour, Chapa Dimba, na Wazee Premier League.

Lakini baadaye, kulingana na treasurer wa uwanja (iko on record), Mheshimiwa George Aladwa - mbunge wa sasa - anadaiwa kupokea Shilingi Milioni 1 kutoka kwa uwanja eti ni kulipa deni la ujenzi. Kwa sheria za CDF, hakuna kulipa deni kwa pesa za CDF. Hizi ni allegations ambazo mpaka leo hazikujibiwa vizuri. Nilipojaribu kumuhoji, sikuweza kumpata tena.

Toyoyo ilikua inachaji 4k kwa masaa mawili, na 20k kwa mechi ya Premier League. Kwa hesabu ya mtaa, hiyo ni karibu 800k kwa mwezi. Lakini Jericho All Stars na youth team ya Raul na Swaleh hawakupata chochote.

*Funzo kwa Ziwani:*

Sisi wa Ziwani tumepewa habari na kiongozi wetu wa nyumba kumi kuwa kuna allocation ya kumaliza Ziwani Ground, wakati huo huo ground haikufungwa na ili-host Kothbiro mbele yetu sote.

Mimi sisemi ni wizi. Nasema ni allegations tunazopewa k**a wakaazi, na tunahitaji majibu.

Kabla hatujaweka turf Ziwani, tuulize maswali ambayo Jericho haikuuliza mapema:

1. Pesa ya uwanja itasimamiwa na nani?
2. Revenue ikija, community team itapata nini?
3. Mtaa utapata masaa mangapi bure?

Maendeleo bila uwazi, ni vita tu.

*Mkaazi wa Ziwani, Mwanahabari wa zamani wa Camp Toyoyo

23/08/2026

MIMI NI ZIWANI. 6TH MARCH 2026 SIJASAHAU.*
>
> Usiku wa 6th March 2026, mvua ilibeba Nairobi. Mimi mwenyewe hapa Ziwani nilikosa mahali pa kulala . Tuliona magari 71 yakisombwa.
>
> *Archive ya serikali inasema:*
> - 23 walikufa Nairobi pekee (NPS)
> - 25 kitaifa
> - 29 waliokolewa
> - 2 missing Kibra, nyumba 3,500 ziliingia maji
>
> *LATEST:* Kenya Met wanasema mvua kubwa inarudi tena *October huu 2026.* El Nino kali.
>
> *SERIKALI NI SISI WANANCHI.* Katiba Article 7(3)(b) inasema unaweza kuongea na lugha yoyote - Sheng, Kikuyu, Luo, Kamba, Sign Language.
>
> *SWALI:* Mvua ikirudi tena, tutajiokoaje wenyewe?
>
> Toa maoni yako hapa comment. Hii ndio dialogue ya Tuwajibike.
>
> *TOURNAMENT UPDATE:* Registration inaendelea. Bado hatujapanga tournament bado. Registration ongoing.
>
> *Contact: 0706480416*
>

18/08/2026

WANANCHI NDIO SERIKALI.
SI MANENO. NI KAZI. 🇰🇪

Article 1(3) inasema mamlaka ni yetu.
Moja kwa moja au kupitia wawakilishi.

Dallas ilifundisha: Ukiokolea uwanja, unatengeneza mabingwa.
Sasa Tukiokolea mazingira, tunatengeneza mustakabali.

JUMAPILI 9 AUGUST 2026
Aggrey Gardens, Nairobi
Organized by Gated Ziwani CBO
Inspired by Dallas Muthurwa Boxing Club

USIWEKE SUMU KWA MWILI WAKO.
USIWEKE SUMU KWA JAMII YAKO.

17/08/2026

TIENDA LIT: KUMBUKA MIZI 🔥

Dallas Muthurwa ilitoa:
Robert Wangila - Dhahabu ya kwanza Afrika Olympics
Suleiman Bilali - Two time Olympian aliyeokoa street kids
Gold - Silver Medalist Sydney

Tuliipigania uwanja huu na Family Bank tukashinda.
Lakini bado kuna mtu anakula revenue ya social hall.

K**A TULIOKOLEA UWANJA, TUOKOLEE NA MAPATO YAKE.

9 AUGUST 2026 - Aggrey Gardens
Tufunze, Tucheze, Tujenge

16/08/2026

"HAIKUA NA KASI" - Frederic Kanoute

Aliposema hivyo baada ya kuja Ziwani, nilielewa.
Sio vijana wetu hawana talent. NI KIWANJA.

K**a msamizi wa Kothbiro Biro na mchezaji wa zamani, nimeona:
- Vijana wakijeruhiwa kwa sababu ya hard surface
- Talent ikipotea kwa sababu ya vumbi na mashimo
- Ndoto zikifa kabla hazijaanza

Leo serikali inajenga stadium ya AFCON. Tunasema ASANTE.
Lakini bila viwanja mashinani k**a vya ZIWANI, hiyo stadium itakua tupu.

TUWAJIBIKE inasema:
1. Linda viwanja vya mitaa
2. Boresha surface
3. Hifadhi Mtaa wa Kwanza Kenya

Talent ya Kenya iko. Tunahitaji tu kiwanja mzuri.
:





13/08/2026

HONGERA MHESHIMIWA NICHOLAS MUSONYE 💚🇰🇪

Hongera kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa AFCON 2027 Executive Committee. Hii ni heshima kubwa kwa Kenya.

Nakumbuka CECAFA ulisema: "Wakenya hawapendi soka la ndani, wanapenda bar na soka la Ulaya."
Lakini CHAN ilituonyesha Wakenya wakija kwa wingi. Changamoto ilikuwa ticketing na organization.

K**a Waswahili husema "Ikitembea k**a Bata, ni Bata". Na Wazungu husema "Insanity is doing the same thing and expecting different results".

Mwaka ujao tuna-host AFCON 2027. Maombi yangu 3:
1. USALAMA: Watu wa usalama wakikosa kulipwa mshahara yao, sisi na wageni tuko hatarini.
2. UCHUMI: Hii ni fursa ya kuuza Kenya zaidi ya utalii.
3. UWAZI: Kesi ya Ksh 45M ya FKF bado tunangoja majibu.

Bado nakumbuka kitabu chako "Reviving Kenyan Football" na wakufunzi James Sianga, Joe Oyando, Mohamed Kheri, Mahmoud Abbas. Tunakisubiri kwa hamu.

Tuko nyuma yako Mheshimiwa. Lakini pia tutakuwa macho. Tusilete Kenya aibu.


Musonye Kenya Federation Leopards SC

07/08/2026

*BARUA WAZI KWA COACH BELDINE ODEMBA*
_Baada ya Harambee Starlets Kuchujwa WAFCON 2026_

Mheshimiwa Coach Beldine,

Kwanza *HONGERA KUBWA*.
Kufikisha Harambee Starlets WAFCON sio jambo dogo. Katika nchi ambayo *zero investment* imefanywa kwa football ya wasichana, wewe umeonyesha kuwa inawezekana.

Ninajua uchungu wa kutolewa. Ninajua pia mzigo uko nao.

*1. UKWELI KUTOKA MASHINANI*
Tatizo si wewe. Tatizo ni mfumo.
Licha ya pesa, bado watu hawahudhurii mechi za wanawake hata kwa Premier League au ligi za chini. Ni wajibu wa mashabiki pia kuhudhuria na kuwapa wasichana motisha. Bila wanja umejaa, hakuna sponsorship. Bila sponsorship, hakuna maendeleo.

Federation? K**a kawaida yao tumezoea kudorora kwao.
Hii *new regime ya Hussein Mohamed* iliahidi mabadiliko. Lakini chini ya ardhi mambo imekuwa mbaya zaidi.

*2. KUHUSU MWELEKEO WA FEDERATION*
Coach, nakuhimiza. *Chochote kitafanyika, hiyo environment ni toxic*.
Niko na hakika kabisa Federation itajaribu kukugeuzia maneno na kukufanya uwe kiongozi wa kushindwa.

Kumbuka: Hii ofisi ya Hussein, hata VP wake walitaka kukutimua Beldine walipoingia ofisi kabla mechi za kimataifa za wanawake zianze. Sasa watajaribu kutumia hii nafasi ya kuchujwa kukumaliza.

*Tafadhali usiruhusu.*
Wewe ni muhimu kuliko hiyo kiti. Hadhi yako ni muhimu kuliko politics zao.

*3. URITHI WAKO*
Nakukumbuka ukicheza ukiwa msichana mdogo. Nilikuhoji kuhusu changamoto mlipitia wakati league ya wasichana ilikua inafadhiliwa na UNICEF. Ile deal iliharibiwa na corruption kutoka kwa then Ministry of Sports.

Licha ya hizo changamoto zote, umekuwa jasiri. Umeongoza wanawake hadi WAFCON. Umefungua milango kwa wasichana wengi mashinani. *Tunakuhitaji huko mashinani.*

Umefanya ya kutosha Coach.
Badala ya kujiharibia hadhi wakisubiri wakutimue, chagua wakati wako. Toka ukiwa umesimama.

Shukrani kwa damu, jasho na machozi yako kwa bendera.

*Sisi mashabiki tuko nyuma yako. Sio Federation.*
*Tujenge soka la wasichana pamoja. Ziwani na kila wanja.*

02/08/2026

sheria kadhaa *zimeletwa / amended* na FIFA/IFAB za 2026 na zilitumika kwa mara ya kwanza kwenye *World Cup 2026* iliyoanza Juni 11th

*1. MAPIGO MAPYA YA VAR*
VAR sasa inaweza kuingilia kwa:
- *Kadi ya pili ya njano iliyokosewa* - ikiwa ni wazi kuwa ilikuwa makosa
- *Utambulisho mbaya* - mchezaji mbaya kupewa kadi
- *Pembe iliyopatikana vibaya* - k**a ni makosa dhahiri na hacheleweshi mchezo
- *Foul kabla ya set piece* 77c5

_Note:_ IFAB walisema VAR ilitumiwa vibaya mara 2 kwenye WC, mfano Embolo vs Argentina aee5

*2. KUFUNIKA KWA MKONO MDOMONI = KADI NYEKUNDU*
K**a unafunika mdomo kwa mkono, jezi au mkono wakati wa ugomvi = *Red Card moja kwa moja*.
Lengo: kupambana na matusi ya kibaguzi k**a ile ya Prestianni vs Vinicius.
Mazungumzo ya kirafiki hayahesabiki ada2b5b477c5

*3. KUTOA WACHEZAJI - SHERIA MPYA*
- *Dakika 10 kuondoka uwanjani* ukibadilishwa. Ukichelewa, mchezaji anayeingia atangoja dakika 1 baada ya kuanza tena
- *Acha uwanja kwa kupinga mwamuzi* = Red Card
- *Timu ikiacha mchezo* = inafungwa moja kwa moja cd8777c5

*4. KUZUIA KUPOTEZA MUDA* ⏱️
- *Hesabu ya sekunde 5* kwa throw-in na goal-kick. Ikimalizika, throw-in inaenda kwa upinzani, goal-kick inakuwa kona
- *Mchezaji aliyetibiwa uwanjani* lazima atoke dakika 1 baada ya mchezo kuanza 7bce

*5. SHERIA MPYA YA MAGOLKIPER 2026/27*
Inajaribiwa England msimu wa 2026/27:
K**a mchezo umesimama kwa jeraha la gokipa, *kocha lazima atoe mchezaji 1 wa uwanjani kwa dakika 1*. Hii ni kuzuia "tactical timeouts".
Isitumike k**a: amepigwa foul, amepatana na mchezaji, au anavuja damu 2cf9

*6. KADI NJANO - WORLD CUP 2026*
- *Kadi za njano zinapanguswa* baada ya group stage na baada ya robo fainali
- *Kadi za njano + red ya moja kwa moja* za preliminary hazihamishi kwenye final 4ce4

*7. MENGINEYO*
- *Goal ikifuata advantage* - mchezaji aliyefoul hatapata njano tena
- *No timeout wakati gokipa anapata matibabu* - wachezaji wote wabaki uwanjani

01/08/2026
Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Nairobi?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Address


Nairobi