03/07/2026
๐จ DEAL DONE
Mshambuliaji nyota wa Simba Queens, Jentrix Shikangwa, amefikia makubaliano ya kujiunga na klabu ya FC Masar inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini Misri.
Taarifa zinaeleza kuwa awali mchezaji huyo hakuwa na mpango wa kuondoka Simba Queens katika kipindi hiki. Hata hivyo, ofa aliyopokea kutoka FC Masar ilikuwa na mvuto mkubwa na hatimaye kumshawishi kukubali changamoto mpya ya kucheza soka la kulipwa nchini Misri.
Jentrix tayari amewasili nchini Misri kwa ajili ya kukamilisha taratibu za mwisho za usajili wake. Akikamilisha uhamisho huo, ataungana na Mtanzania, Hasnath Ubamba, ambaye tayari anaitumikia FC Masar.
Kwa upande wa Simba Queens, wamebariki uhamisho huo na tayari wameanza mchakato wa kutafuta mbadala wake katika dirisha hili kubwa la usajili, wakijiandaa kwa msimu ujao wa Ligi Kuu pamoja na michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Jentrix anaondoka Simba Queens baada ya kuwa na msimu bora, akifunga mabao 16 na kuwa mmoja wa wachezaji walioiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.
Miongoni mwa mabao yake muhimu zaidi ni yale aliyofunga dhidi ya Yanga Princess, JKT Queens na Fountain Gate Princess, ambayo yalikuwa na mchango mkubwa katika safari ya Simba Queens kutwaa taji la ubingwa.
Anaondoka Jentrix mshambuliaji bora pekee wa kigeni kuwahi kucheza ligi yetu ya Tanzania (namba zake zinaongea).
๐น๐ฟโก๏ธ๐ช๐ฌ
Powered by Matukio Muhimu Sports Wear
26/06/2026
26/05/2026
26/05/2026
26/05/2026