02/09/2026
MBUNGE WA JIMBO LA UKONGA MH, BAKARI SHINGO ATOA MUALIKO AL BAYAAN
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mhe. Bakari Shingo, amewaalika wanafunzi wa Shule ya Msingi AL BAYAAN kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni sehemu ya kuwapa fursa ya kujifunza kwa vitendo
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mhe. Bakari Shingo amesema kuwa ziara hiyo itawajengea wanafunzi hao uwezo na uelewa mpana zaidi, kupitia yale waliyoyajifunza walipotembelea Bunge pamoja na maarifa waliyoyapata katika safari yao
Ni hatua muhimu katika kuwajengea wanafunzi mazingira ya kujifunza kwa kuona, kuuliza na kupata uzoefu wa moja kwa moja nje ya darasa. Elimu inapounganishwa na vitendo, huacha kumbukumbu na kujenga kizazi chenye uelewa mpana