Kautv

Kautv

Share

📺 Kau TV – Online TV ya habari, michezo, na burudani. Live kila siku.🌍 Tazama popote, muda wowote!

14/07/2026

INDONESIA: Imam wa Msikiti wa At-Taqwa uliopo
eneo la Kelurahan Ujuna, anaripotiwa kufariki dunia siku ya Alhamisi (917/2026), punde tu baada ya kumaliza kuongoza Sala ya Alfajiri ya pamoja
(Jamaah) msikitini hapo.

Kulingana na video ya nasa za kamera za usalama
(CCTV) zilizosambaa, marehemu alionekana bado ana nguvu na alifanikiwa kuongoza dhihiri ya pamoja na waumini wenzake baada ya sala kukamilika.

Hata hivyo, katikati ya mfululizo wa dhikr hizo, ghafla alianguka chini na kupoteza fahamu.
Waumini waliokuwa karibu naye walichukua hatua
za haraka kumpa msaada kwa kumnyanyua na kumtoa nje ya safu ya sala (safu). Tukio hilo lilitokea kwa kasi kubwa huku likishuhudiwa na waumini wote waliokuwa bado ndani ya msikiti huo.

14/07/2026

Pastor amefunguka mazito kutoka moyoni kuhusu
anguko la malezi ya mtoto wa kiume siku hizi.
Anasema jamii imelala na inachekea ujinga! Leo hil badala ya kulelea wavulana kuwa wanaume thabiti na wenye misingi, tunawachekea kina “Uncle T” wanaotamba mtandaoni kwa mambo yasiyo na maadili.

K**a jamii isiposimama sasa hivi kurudisha
heshima ya mtoto wa kiume, baadae tutakuwa na taifa la ‘ma-uncle’ wengi lakini wanaume wa kweli wachache sana.
Je, unakubaliana na Pastor kuwa jamii imefeli kwenye malezi ya mtoto wa kiume? Dondosha maoni yako hapa chini.




13/07/2026

EBOO! MPYA JIKONI.
Drama ya Zuchu na Diamond Platnumz inazidi kuchukua sura mpya! Baada ya Zuchu kuandika ujumbe mzito jana usiku akitangazia umma kuwa ameachana rasmi na Diamond, hatimaye mambo yameanza kuvuja.

Mwanahabari maarufu wa udaku nchini, Carrymastory, anadai kufanikiwa kunasa ‘mchongo’ mzima na kupata chanzo cha uhakika kilichosababisha wawili hao kuingia kwenye mgogoro mkubwa hadi kufikia hatua ya kuachana.




13/07/2026

Mfalme wa Bongo Fleva, King Kiba usiku wa jana amezizima rasmi wilaya ya Katoro mkoani Geita baada ya kushusha bonge moja la shoo kwenye sherehe ya Send Off ya Monalisa Sylvester, binti wa mchimba madini maarufu wa eneo hilo.

Alikiba aliteka jukwaa na kuwafanya matajiri wa Geita washindwe kujizuia, ambapo ndugu, jamaa, na marafiki wa familia hiyo walimwaga “mafuriko” ya fedha taslimu jukwaani k**a ishara ya kukubali muziki wake mzuri.

Shoo hiyo imethibitisha kwanini yeye ni mmoja wa wasanii wa gharama kubwa na wenye heshima kubwa kwenye tasnia..👑

13/07/2026

Usalama shakani Ruaka nchini Kenya, majambazi wapora mchana kweupe.. Video ya CCTV imenasisha wakati ambapo genge la majambazi wenye silaha lilipovamia na kuwapora wakazi wa eneo la Ruaka, nje kidogo ya jiji la Nairobi nchini Kenya, mchana wa jua kali.

Tukio hilo la kijasiri limewaacha wananchi wa eneo hilo wakiwa na mshtuko mkubwa na hofu juu ya usalama wao. Kwenye picha hizo za usalama, majambazi hao wanaonekana wakitekeleza unyama huo bila woga wowote huku wakiondoka na mali za raia wasio na hatia.

Unadhani nini kifanyike na vyombo vya usalama nchini Kenya kukomesha mtindo huu wa uhalifu wa mchana kweupe? Toa maoni yako hapa chini.

👇👇🏿👇🏾

13/07/2026

Monalisa ametoa shukrani hizo za dhati baada ya kufanyika kwa sherehe yake ya Send-Off iliyoweka historia Julai 2, ambapo baba yake alihakikisha mizunguko na shughuli zote za binti yake kwa siku nzima zinafanyika kwa kutumia usafiri wa anga (Helikopta).
Mbali na helikopta hiyo, sherehe hiyo ilitikisa nchi kwa zawadi ya fedha taslimu Shilingi Bilioni Moja na Milioni Nne (Tsh 1,004,000,000/=) iliyotolewa na k**ati, huku burudani ikitolewa na Ali Kiba.

13/07/2026

🗣️ GEITA:::: Sherehe ya kuaga binti mtarajiwa (Send-Off) ya Monalisa Sylvester, mtoto wa mchimba madini maarufu kutoka eneo la Katoro mkoani Geita, imeweka rekodi mpya nchini kufuatia kufuru ya gharama na zawadi zilizotolewa.
Katika tukio hilo la kipekee lililofanyika Julai 2, 2026, mambo makuu matatu yafuatayo yamevuta hisia za wengi mtandaoni na nchini kote:

Zawadi ya Shilingi Bilioni 1.004: K**ati ya maandalizi ya sherehe hiyo imeweka historia kwa kumkabidhi Monalisa zawadi ya pesa taslimu kiasi cha Shilingi Bilioni Moja na Milioni Nne (Tsh 1,004,000,000/=) k**a kianzio cha maisha yake mapya ya ndoa.

Usafiri wa Helikopta, Tofauti na mazoea ya kutumia misafara ya magari ya kifahari, Bibi Harusi mtarajiwa alitumia usafiri wa anga (Helikopta) kwa safari na shughuli zake zote za siku hiyo nzima.

Burudani kutoka kwa Alikiba. Sherehe hiyo ilipambwa na burudani ya kiwango cha juu kutoka kwa nguli wa muziki wa Bongo Fleva, aliyetumbuiza wageni waalikwa.
Tukio hili linatajwa kuwa moja ya sherehe za kifahari na gharama kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla kwa mwaka huu.

🤸

13/07/2026

Ubunifu wa Afrika Mashariki hauishi hamu! 🇺🇬 Mfumo wa ‘Uganda’s Inventory System’ umebadilisha kabisa ulinzi wa magari baada ya kuja na alarm inayopiga kelele za “Mwizii!” badala ya kutoa kile king’ora tulichokizoea.

Gari likijaribu tu kuguswa au kuingiliwa, mfumo huo unalipuka kwa sauti kubwa ya binadamu inayofoka na kupiga yowe, jambo linalomfanya mwizi achanganyikiwe (panic) na kuvuta attention ya kila mtu aliyepo jirani kwa haraka zaidi.
Hii sasa ndio inaitwa ulinzi shirikishi wa kiteknolojia!

Je, wewe uko tayari kulinda chuma chako kwa alarm hii ya kupiga kelele, au unaona itakuletea aibu mtaani kila ikisafishwa? Dondosha comment yako hapa chini! 👇👇🏾

12/07/2026

BREAKING NEWS! Mapya yamezuka.. Saa chache tu baada ya Diamond Platnumz kumfanyia mama yake mzazi (Mama Dangote) sherehe kubwa ya kuzaliwa, msanii Zuchu ameshtusha mashabiki kwa kuposti ujumbe mzito kupitia Insta Story yake unaoashiria kuachana na Diamond.
Jambo hili limeacha maswali mengi, hasa ukizingatia jana tu kila kitu kilionekana kuwa sawa.

Je, unahisi huu ni muendelezo wa “KIKI” za mjini kuelekea miradi mipya ya muziki, au ndio ukweli wenyewe na penzi limefika tamati? Drop comment yako hapa!




Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address

Dar Es Salaam