04/07/2026
DUNIA NZIMA INAMTUKANA Fabrizio Romano
Iko Hivi,
Wakati mechi ikiwa dakika ya 80+, Mwandisho Nguli wa michezo Fabrizio Roman ali-post akisema mechi ya Canada na Morocco imemalizika kwa matokeo ya 0-2.
Kitendo hicho kilizua maswali mengi mtandaoni juu ya weledi wa mwandishi ho ambaye amekuwa na tabia ya kuposti matokeo ya mwisho "FullTime" hata kabla ya mchezo kuisha.
Hata hivyo leo, ilikuwa siku mbaya kazini, Kwani katika dakika Nane za Nyongeza Morocco walipata goli la tatu na hivyo mchezo kumalizika kwa 3-0 badala ya 2-0 aliyoandika yeye.
Licha ya baadaye kufuta post ile, lakini Dunia haijafuta na bado inamjadili kwa kitengo hicho cha kushangaza.
Lets Respect Football
04/07/2026
Kiungo Mshambuliaji wa Girona, Azzedine Ounahi anaitanguliza Morocco, Asisti kutoka kwa beki bora Duniani Achraf Hakimi.
Morocco Wanaipeperusha Vyema Bendera ya Afrika
No Saibari?, No Problem!
04/07/2026
HABARI MBAYA KWA AFRIKA
Staa wa timu ya taifa ya Morocco Ismael Saibari ameshindwa kuendelea na mchezo baada ya kupata "Jeraha la Misuli ya Nyuma ya Paja" katika mchezo dhidi ya Canada.
Jeraha la aina hiyo husababishwa na Kukimbia Kwa Kasi, Kuruka ama Kusimama Gafla baada ya kukimbia kwa muda.
Saibari atafanyiwa vipimo zaidi ili kuona jeraha lake lipo kwenye kiwango gani na muda atakao kaa nje;
Grade 1 (Mild) - Wiki 1-3
Grade 2 (Partial Tear) - Wiki 3-8
Grade 3 (Complete Rupture) - Hatua hii Huhitaji Upasuaji na hivyo kuwa nje Miezi 3-6
Mchezaji huyo mpya wa Bayern Munich amekuwa kwenye kiwango kizuri kwenye michuanio ya Kombe la Dunia akifunga;
⚽️🇧🇷 Goli vs Brazil
⚽️🏴 Goli vs Scotland
⚽️🇭🇹 Goli vs Haiti
⚽️🇳🇱 Penati ya Ushindi vs Netherlands
05/06/2026
FURUSHI LA PESA KUMG'OA OLISE: Vita Mpya ya Madrid na Bayern
Real Madrid C.F. imeweka mezani mpunga mrefu, Euro milioni 150 Ili kumsajili winga tishio wa FC Bayern München
Rais wa Madrid amesema "piga ua lazima Mfaransa huyo atue kikosini"
Ikumbukwe Kuwa mwezi uliopita Rais wa Bayern alisema "Michael Hauzwi hata kwa Euro Milioni 200"
Hii ni Vita ya PESA na Heshima, Je Nani atashinda Vita hii?
Tuandikie kwenye Comment
13/05/2026
Hii move lilistahili Kuwa Goli halali au Siyo Halali?
09/05/2026
K**A WEWE NI YANGA SC, LIKE HAPA