09/05/2026
Naa_12
Analysis, stories & unforgettable moments
From the streets to the world
09/05/2026
Naa_12
05/05/2026
Ba MaC...
MSIBA MKUBWA KATIKA SHOW YA MONSTER TRUCK: GARI LAPOTEZA MZUNGUKO NA KUGONGA WATAZAMAJI
Kile kilichotarajiwa kuwa burudani ya kifamilia kimegeuka kuwa tukio la huzuni kubwa huko Popayán, Colombia.
Monster Truck moja ilipoteza udhibiti wakati wa onyesho na ikaingia moja kwa moja kwenye umati wa watu, na kusababisha vifo vya angalau watu 3 na zaidi ya 30 kujeruhiwa. Miongoni mwa waliopoteza maisha ni mtoto mdogo, tukio ambalo limeacha simanzi na hasira kubwa katika jamii hiyo.
Mgongano huo ulikuwa wa moja kwa moja na wa kutisha. Familia zilizofika kufurahia show zilijikuta zimenasa katikati ya machafuko huku hofu ikitanda eneo lote. Wengi wa majeruhi, wakiwemo watoto, walikimbizwa hospitalini ambapo baadhi yao bado wako katika hali mbaya sana.
Mbali na maafa ya binadamu, tukio hilo pia lilisababisha uharibifu wa mali, miti kuanguka, na hitilafu ya umeme, hali iliyolazimu mamlaka kufunga na kuzingira eneo lote mara moja kwa ajili ya uokoaji na usalama.
Sasa swali kubwa linabaki: je, hili lilikuwa ajali tu… au janga ambalo lingeweza kuepukwa?
Mamlaka zimeanza uchunguzi kubaini k**a hatua zote za usalama zilizingatiwa wakati wa tukio hilo.
Credit
05/05/2026
Soka linaweza kukuinua hadi kileleni… lakini kosa moja linaweza kukuangusha vibaya kuliko unavyofikiria.
Mwaka 2003, Rio Ferdinand hakukutwa na dawa yoyote mwilini lakini alikosa kipimo cha ghafla cha doping. Kwa mashabiki, hilo lilionekana dogo. Lakini kwa WADA, kukosa test ni sawa na kujaribu kuficha ukweli. Adhabu yake? Miezi 8 nje ya soka.
Mwaka 1995, Eric Cantona aligeuza uwanja kuwa jukwaa la hasira “kung-fu kick” kwa shabiki. Dunia ilisimama. Alifungiwa miezi 8, na hapo ndipo soka likaweka wazi mipaka kati ya mchezaji na mashabiki.
Kwa Mark Bosnich, mambo hayakuwa ya mjadala alikutwa na co***ne. Adhabu ikafuata, na career yake ikaporomoka. Wakati huo huo, Joey Barton alifungiwa kwa betting sio kwa sababu alipiga mtu, bali kwa sababu betting inaweza kuvunja uaminifu wa matokeo ya mechi.
Hata magwiji hawakuokoka. Diego Maradona alifungiwa kwa doping kwenye FIFA World Cup 1994. Na Paul Pogba alipata adhabu ya miaka 4 kwa testosterone homoni inayoongeza nguvu kabla ya kupunguzwa hadi miezi 18. Hapa ndipo wengi hawajui: wakati mwingine doping haitokani na nia mbaya, bali supplements au dawa zenye kemikali zilizopigwa marufuku.
Kwa David Bystroň, alikutwa na methamphetamine dawa nzito sana na kufungiwa miaka 2. Na sasa, Mykhailo Mudryk yuko kwenye hatari ya hadi miaka 4 kwa meldonium dawa ya moyo inayoweza kuongeza stamina. Hii inaonyesha kuwa hata dawa za kawaida zinaweza kuwa hatari kwenye soka la kisasa.
Lakini si dawa tu. Juanito aliwahi kumkanyaga usoni Lothar Matthäus ukatili wa wazi, adhabu kali. Na Roberto Rojas alienda mbali zaidi akajijeruhi mwenyewe ili kudanganya dunia… akaishia kufungiwa maisha.
Mwisho wa yote, kuna ukweli mmoja ambao hauwezi kubadilika:
Soka si mchezo wa miguu tu ni mfumo wa uaminifu. Na ndani yake, kosa la sekunde moja linaweza kukuadhibu kwa miaka… au maisha yote
#12
03/05/2026
1+ leo ni iku yangu 12
Ninashukuru Mungu kwa zawadi ya uhai, afya na kila hatua niliyopiga hadi leo. Sio safari nyepesi, lakini kila changamoto imenijenga kuwa imara zaidi.
Kipekee kabisa, napenda kumshukuru mama yangu—mama ntilie wangu shujaa
Wewe ni mfano wa kazi, uvumilivu na mapenzi ya kweli. Umeamka mapema kila siku, ukapambana bila kuchoka ili mimi nipate nafasi ya kuwa hapa nilipo leo. Jasho lako lina thamani kubwa kuliko maneno ninayoweza kusema.
Leo si birthday yangu tu, ni ushindi wako pia mama.
Asante kwa kila kitu, nakupenda sana
Happy Birthday to me
03/05/2026
Sisi haoo
My dear dada halima
02/05/2026
Ba MaC
01/05/2026
Chini ya jua kali, bado nasubiri green yangu 🚦