Halisi Max

Halisi Max

Share

Updates 24 Hrs

11/08/2026

🇺🇸 TRUMP AFICHWA KWENYE LORI ABADILISHA NDEGE KWA SIRI BAADA YA TISHIO LA IRAN

Vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, alihamishwa kwa siri kutoka kwenye ndege ya Air Force One wakati akiondoka kwenye mkutano wa kilele wa NATO nchini Uturuki mwezi uliopita, kutokana na tishio linalodaiwa kutoka Iran.

Kwa mujibu wa gazeti la The Washington Post, Trump alionekana mbele ya kamera akipanda Air Force One, lakini baadaye alihamishwa kwa siri kupitia gari la huduma ya chakula la uwanja wa ndege, ambalo lilimpeleka hadi kwenye ndege ndogo ya kijeshi aina ya C-32A.

Operesheni hiyo inadaiwa kufanyika bila baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu pamoja na waandishi wa habari waliokuwa kwenye ndege ya awali kujua kwamba Trump tayari alikuwa amehamishiwa kwenye ndege nyingine.

Maafisa wa Marekani waliambia CBS News kuwa kulikuwa na tishio linaloaminika kutoka Iran dhidi ya Trump, jambo lililosababisha hatua hiyo ya kiusalama.

Awali, Trump alikuwa amesema kuwa yeye ndiye “lengo namba moja” la Iran wakati wa ziara yake nchini Uturuki.
Ikulu ya Marekani bado haijathibitisha rasmi taarifa kuhusu mpango huo wa siri wa kubadilisha ndege.

11/08/2026

Mchezaji Selemani Mwalimu amewaaga kwa mara ya mwisho wana Simba SC

"Ulikuwa Msimu uliobeba historia nyingi kwangu na kwa timu kwa ujumla. Niwashukuru sana wachezaji wenzangu, makocha na watendaji wote kwenye benchi la Ufundi kwa ushirikiano mlionipa kipindi chote nilichovaa jezi ya Simba SC.

Kwa kipekee, niwashukuru sana Mashabiki wote wa Klabu hii ambao mara zote mlikuwa mkiniunga mkono katika kila dakika niliyokuwa uwanjani.

Asanteni sana na Kila la Kheri" Ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram

11/08/2026

Haji Manara asema Feitoto Hawezi kwenda Simba SC hawana uwezo wa Kuilipa Azam Bilioni 7 ili iweze kumuachia Atoa Ahadi ya Kuacha Kazi Wasafi FM.

11/08/2026

"Feisal salum Akienda kucheza Simba This season yaani hili dirisha linalofungwa kesho kutwa nasisitiza Feisal salum akienda kucheza Simba SC Mimi na Wasafi Bye Bye kiufupi Simba Bilioni 7 hawana na hata k**a wanazo Kuzitoa Bilioni 7 ni kitu ambacho mission impossible" Amesema Haji Manara kupitia kipindi Cha Jana na Leo Wasafifm

11/08/2026

Ameandika Mudumoh ✍️

MTIZAMO WANGU: Kuhusu Mabasi Kupelekwa Stendi ya Magufuli
Kwa mtazamo wangu, suala la umbali wa Stendi ya Magufuli halipaswi kuwa sababu ya kupinga mpango huo.

Dar es Salaam ina uwanja wa ndege uliopo Kipawa, lakini watu kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Bagamoyo wanafika huko kwa sababu wanajua ni huduma muhimu.

Stendi ya Magufuli imejengwa kwa kiwango kikubwa na kizuri, na imekuwa ikisifiwa na watu wengi ndani na nje ya Afrika.

Lengo kubwa la kujengwa kwake ni kupunguza msongamano katikati ya jiji na kuweka mfumo bora wa usafiri.

K**a ilivyokuwa zamani wakati stendi ilihamishwa kutoka Kisutu kwenda Ubungo, na baadaye Ubungo kwenda Mbezi, watu walilalamika kuwa ni mbali lakini hatimaye walizoea.

Changamoto za mwanzo zipo kwenye kila mabadiliko, lakini tunapaswa kuangalia faida ya muda mrefu kwa jiji letu. Haiwezekani kila mtu atake mabasi yapite mlangoni kwake; wakati mwingine ni lazima wananchi waendane na mipango ya maendeleo.

11/08/2026

Mwamuzi wa Ahmed Arajiga amepewa jukumu na TFF la kuchezesha mchezo wa Ngao ya Jamii 2026 kati ya Simba SC na Yanga SC utakaofungua msimu mpya wa soka Tanzania Mchezo utakaochezwa Zanzibar.

Mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona namna atakavyoiongoza mechi hiyo kubwa ya Kariakoo Derby.

Una Maoni Gani ✍️

11/08/2026

"Kwa hawa Viongozi wana Simba
Tutazidi Kuumia ni bora Timu
Tuwape Jayrutty na Kansela Salaah" Anasema Shabiki wa Simba, Mwijaku.

11/08/2026

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema wamiliki na waendeshaji wa mabasi makubwa ikifika Agosti 17, 2026 wanatakiwa kuyapeleka magari yao katika Stendi ya Magufuli iliyopo Mbezi.

Chalamila amesema baada ya tarehe hiyo utekelezaji wa utaratibu huo utaanza rasmi, ambapo mabasi ya masafa marefu hayatapeleka tena abiria katikati ya jiji.Ameeleza kuwa abiria watakaoshushwa Stendi ya Magufuli wataendelea na safari zao ndani ya Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa ndani k**a mabasi ya mwendokasi, daladala, bajaji, pikipiki pamoja na huduma maalum za usafiri (shuttle) zitakazotolewa na kampuni za mabasi husika.

Kwa mujibu wa Chalamila, hatua hiyo inalenga kupunguza msongamano katikati ya jiji na pia kulinda ajira na biashara za waendeshaji wa usafiri wa ndani, kwani mabasi makubwa yanapoingia maeneo ya mjini yanaathiri nafasi za wadau wengine katika mfumo wa usafirishaji.

Funzo la maisha: Wapo wanaohoji utaratibu huu, lakini wengine wanaona ni hatua ya kupanga jiji. K**a ilivyo kwa uwanja wa ndege ambao una eneo maalum la kufuatwa na abiria kutoka sehemu mbalimbali na hatujawahi Kuusikia watu Walilalamika Airport Ipo mbali, hata stendi inaweza kuwa na utaratibu wake. Mabasi kuzagaa katikati ya jiji kwa muda mrefu kumesababisha changamoto za msongamano, hivyo Stendi ya Magufuli inaweza kuwa suluhisho la muda mrefu.

11/08/2026

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally, amekumbana na lawama kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo baada ya Selemani Mwalimu kujiunga na Yanga SC, siku chache baada ya kutambulishwa mbele ya mashabiki wa Simba kwenye tukio la Simba Day.

Baadhi ya mashabiki wameonyesha kukerwa na kitendo cha kumtambulisha mchezaji huyo kisha baadaye kuondoka kwenda kwa wapinzani wao wa jadi.

Prisca Batister aliandika:"Ulimtambulisha wa nini sasa na mbwembwe zote, kumbe ufala mtupu."

Elizabeth Martin naye amesema:"Tatizo sio Sele kwenda Yanga, tatizo ni nyinyi mmemtambulisha mara mbili mmenyang'anywa. K**a hakuna hela ya usajili semeni, acheni longolongo. Uongozi wa Simba ni mbovu mno."

Ruta K**ala ameongeza:"Wewe na viongozi wenzako mkome kutuzoea, mmetuzoea vibaya sana nyie."

Hali hiyo imeibua mjadala kwa mashabiki wa soka kuhusu namna klabu zinavyoshughulikia masuala ya usajili na utambulisho wa wachezaji wapya.

11/08/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akicheza mchezo wa bao baada ya kuwasalimia wananchi wa Mji Mkongwe (Stone Town) katika eneo la Jaws Corner, Zanzibar, tarehe 10 Agosti, 2026.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address

Mbezi
Dar Es Salaam