22/06/2026
Chama cha Sitting Volleyball kinaendesha mafunzo maalum katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Hii ni fursa ya kipekee kwa wote wenye nia na shauku ya kuendeleza mchezo wa Paravolley nchini!
Michezo ya watu wenye ulemavu inahitaji nguvu yetu sasa hivi. Ni wakati wetu wa kuamka, kuwajibika, na kuonyesha uwezo wetu.
Tarehe: 24 - 28 Mahali: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Usikae pembeni! Jiunge nasi sasa tufanye mapinduzi kwenye Paravolley. Karibuni wote! ππ₯
18/06/2026
UONGOZI MPYA: KARIBU KATIBU MKUU! π
Tunapenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Ndugu Ramadhan Namkoveka kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Kamati ya Utendaji ya Tanzania Paralympic Committee (TPC).
Udumu katika kuiongoza michezo ya walemavu na kuifikisha katika kilele cha mafanikio nchini na kimataifa. Kila la heri katika majukumu haya mapya ya kujenga na kuendeleza vipaji!
27/05/2026
πβ¨ EID AL ADHA MUBARAK β¨π
Tanzania Paralympic Committee wishes all Muslims in Tanzania and around the world a blessed Eid filled with peace, unity, happiness, and countless blessings. π€
May this special occasion bring joy, good health, love, and prosperity to you and your families.
Together for an inclusive and empowered society through Para Sports. πΉπΏβΏ
Eid Njema! ππ
21/05/2026
πΉπΏ KARIBU KATIKA KAMATI YA PARALIMPIKI TANZANIA (TPC)! βΏβ¨
Kamati ya Paralimpiki Tanzania (TPC) kwa furaha kubwa inamkaribisha rasmi Engineer Leonard Marango k**a Katibu Msaidizi mpya wa Kamati ya Paralimpiki Tanzania.
π βUzoefu, Maono na Mabadiliko Chanya.β
Kuapishwa kwako ni hatua muhimu yenye matumaini mapya kwa maendeleo ya michezo ya watu wenye ulemavu nchini Tanzania. Tunaamini uwezo wako, uzoefu wako na maono yako vitaongeza nguvu mpya katika safari ya mafanikio ya TPC kitaifa na kimataifa.
Kupitia uongozi wako tunatarajia:
β
Kuimarika kwa ufanisi, uwajibikaji na weledi katika usimamizi wa michezo ya Paralimpiki
β
Ukuaji wa vilabu na vyama vya michezo ya watu wenye ulemavu nchini
β
Kuandaa wanamichezo wetu kwa ushindani wa kimataifa kuelekea Paralympic Games 2028 π
β
Kuendeleza ari ya ushirikiano, usawa na mafanikio kupitia michezo
π Tuna Imani Kubwa na Wewe.
π₯ Karibu Tuendelee Kuandika Historia Mpya!
πΉπΏ Pamoja Tunaweza Zaidi.
19/05/2026
π₯ KARIBU KWENYE JUKWAA LA MABADILIKO! π₯
Tunayo furaha kubwa kumkaribisha Ernest Justin Nyabalale kwenye Kamati ya Utendaji ya Tanzania Paralympic Committee (TPC) k**a Mwakilishi wa Wachezaji. πΉπΏπ
Uzoefu wako mkubwa k**a mchezaji na kiongozi ni hatua muhimu katika kuimarisha sauti ya wanamichezo wetu na kuhakikisha maslahi yao yanawakilishwa kwa nguvu na weledi.
Kwa kushirikiana na IPC na BMT, tunaendelea kujenga mazingira bora kwa maendeleo ya michezo ya Paralympic Tanzania na kuwapa wanamichezo nafasi ya kungβara kitaifa na kimataifa. πβ¨
Karibu sana kiongozi wetu kazi iendelee! ππ₯
18/05/2026
π KARIBU NDANI YA KAMATI YA UTENDAJI YA TPC! πΉπΏβΏ
Tunajivunia kumkaribisha Ally Yasin Kiponda k**a Mjumbe wa Kamati ya Utendaji β Tanzania Paralympic Committee (TPC).
Kwa uzoefu wake katika michezo ya watu wenye ulemavu, tunaamini atachangia kwa kiwango kikubwa kukuza na kuendeleza michezo hususan Goalball katika Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kusini β Mbeya, Ruvuma na Iringa.
Pamoja tunaendelea kujenga mazingira ya usawa, ujumuishi na maendeleo ya michezo kwa watu wenye ulemavu. πͺπ½π
β¨ Pamoja, tunajenga ustawi na usawa katika michezo!
17/05/2026
ποΈ TAARIFA YA MSIBA ποΈ
Kamati ya Paralimpiki Tanzania (TPC) inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Rais Mstaafu wa TPC, Marehemu GWAKISA MWAKABETA, kilichotokea tarehe 16 Mei, 2026 jijini Dar es Salaam.
Tumempoteza kiongozi madhubuti, mwenye maono makubwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya michezo ya walemavu nchini Tanzania. Uongozi wake utaendelea kukumbukwa na kuthaminiwa milele.
βTumeΒpoteza nguzo, kiongozi madhubuti, na mwanamapinduzi wa michezo ya walemavu nchini. Mchango wako utaishi daima kwenye mioyo yetu.β π€
TPC inaungana na familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wadau wote wa michezo katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina. π―οΈ
15/05/2026
π Hongera sana Madam Thauriya Ahmed Diria kwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania Paralympic Committee (TPC) ππΉπΏ
Uchaguzi huu ni ishara ya imani kubwa katika uwezo wako, uongozi wa kimkakati na mchango wako katika maendeleo ya michezo kwa watu wenye ulemavu nchini Tanzania na kimataifa. π
π
β¨ βUongozi wa Kimkakati, Uzoefu wa Kimataifa, Mapinduzi ya Michezo Nyumbani.β
Kupitia ushirikiano wa Tanzania Paralympic Committee (TPC) na International Paralympic Committee (IPC), tunaamini Tanzania itaendelea kungβara kimataifa kuelekea Road to Paralympic β Los Angeles 2028 πΊπΈπ₯
π Pamoja tunavunja vikwazo, tunafikia malengo!
14/05/2026
ππ Kamati ya Paralympic Tanzania (TPC) kwa kushirikiana na wadau wa michezo ya watu wenye ulemavu, tunatoa pongezi za dhati kwa MR. TUMA DANDI kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kamati ya Paralympic Tanzania (TPC) πΉπΏ
Tunatambua mchango mkubwa wa International Paralympic Committee pamoja na vyama vyote vinavyosimamiwa na TPC, wadau wa michezo, na mamlaka mbalimbali zinazosimamia maendeleo ya michezo nchini kwa kuendelea kuunga mkono ushirikishwaji, maendeleo na mafanikio ya wanamichezo wenye ulemavu. π
βΏ
Tunaamini uongozi wako utaendelea kuimarisha mshik**ano, maendeleo ya michezo ya Paralympic na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa. πβ¨
πͺπΎ Kazi iendelee!