02/07/2026
WAZUNGU NDIO TUNAIFANYA HII NCHI IENDELEE KUWEPO, HAKUNA MNACHOJUA ZAIDI ULEVI, WIZI NA UZINZI
Kauli kutoka kwa mkazi wa Afrika Kusini mwenye asili ya Ulaya akiwalenga waafrika Kusini weusi.
Kwa ufupi tu hii ni sehemu ya tafsiri ya anachokisema huyo Kaburu hapo ambao ndio wanaomiliki zaidi ya 80% ya ardhi ya Afrika Kusini.
"Naona kuna Waafrika Kusini weusi wengi wanataka kuwafukuza Wazungu pia hapa Afrika Kusini. Nilikuwa najua kwamba nyinyi ni wajinga, lakini sikuwahi kujua kwamba ni wajinga kwa kiwango hicho. Mzungu ndiye jamii pekee inayochangia kuiweka nchi hii hai. Mkifukuza Wazungu kutoka Afrika Kusini, nawahakikishia sasa hivi kwamba hamtakuwa k**a Zimbabwe tu, mtakuwa vibaya zaidi kuliko Zimbabwe.
Msiwasikilize hao wapumbavu wanaosema wanataka kufukuza kila mtu. Nafikiri labda umefika wakati wa wazungu wa Wamalawi, Wazimbabwe na watu wengine wote wasio na hatia Labda sisi ndio tuwafukuze nyinyi mrudi baharini.
Kwa sababu mnadhani nchi hii ni yenu peke yenu. Hapana, kaka yangu au dada yangu. Nchi hii ni ya kila mtu anayeishi Afrika Kusini na anayechangia kuifanya iwe mahali pazuri zaidi. Lakini k**a unachangia kuifanya Afrika Kusini iwe mahali pabaya zaidi, basi sisi ndio tunapaswa kukufukuza.
Mnachojua kufanya ni maandamano tu. 'Sina furaha, nitaandamana, nitapinga...' Lakini hamjui kufanya kazi. Hamjui jinsi ya kuboresha mambo. Kila mara mnapomwona mtu anafanikiwa kuwazidi, mnataka kumfukuza. Kwa sababu mnajua kwamba watu kutoka nchi nyingine wanaofanya kazi Afrika Kusini wanafanya kazi zao vizuri zaidi kuliko ambavyo baadhi yenu mnafanya.
Mnachoweza ni kulala na wanawake, kunywa pombe, kuiba na kuharibu. Hamtaki kujenga."
Chanzo: SiasaTz
02/07/2026
02/07/2026
02/07/2026
02/07/2026
02/07/2026
02/07/2026
02/07/2026