Kagaba Media

Kagaba Media

Share

HABARI ZOTE NA MICHEZO NA BURUDANI, KITAIFA NA KIMATAIFA UTAZIPATA HAPA 👐

(USIKAE KINYONGE)

28/08/2026

|58| Epl

Crystal palace 1-2 Manchester city 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿

28/08/2026

🚨Azam FC imeshindwa kupata alama tatu ugenini kwa mara nyingine tena msimu huu baada ya sare dhidi ya Geita Gold.
Kwenye mechi 4 tayari Azam FC ya Florent Ibenge imeangusha alama 4.

NB: Kosa moja la Zuberi Foba la dakika za mwisho limeigharimu mechi nzima ya Azam FC. Foba alitoka golini bila kuwa na mahesabu sahihi.

Mbio za ubingwa zimeingia ugumu kwa Azam FC.

28/08/2026

Full time : Tanzania NBC 🇹🇿

Young Africans 🇹🇿 2➖0 Pamba Jiji

Toure ⚽
nzengeli ⚽

28/08/2026

Haaland Goooooooooooooo

Crystal palace 0-1 man city 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿

28/08/2026

🚨Wananchi hii haikubaliki hata kidogo hiki kipimo sio cha NBCPL kabisa !.. Maxi Nzengeli mwenzako yupo Real Madrid , Toure arudi kwenye ligi ya Saudia , Shashaman hiyo energy umetoa wapi mkuu ?

28/08/2026

🚨Kwenye mjengo wa mashambulizi Yanga inawatumia Ngoma, Bacca na Bakari katika mstari wao wa kwanza, lakini kitu chengine ambacho wanakifanya wachezaji hawa watatu wanakuwa karibu kabisa na mstari wa katikati ya Uwanja.

Ukiachana na hawa watatu wachezaji wengine wote wa Yanga wanakuwa mbele ya mistari ya wachezaji wa Pamba Jiji FC katika robo tatu ya eneo la kushambulia.

Pamba Jiji ni k**a wamefungiwa kwenye Banda hivi, hawapati eneo kubwa la kucheza, isivyo bahati hata pale ambapo wanakuwa na Mpira machaguo ya pasi kwao yanakuwa ni machache sana kwa sababu wanakuwa wamerundikana kwenye eneo kubwa kiasi mistari yao inashindwa kufunguka kwa haraka.

✅ Kitu Chanya kwenye mchezo ukiachana na uharaka wa Yanga wanapokwenda mbele wamekuwa bora pia kwenye recovery runs, wanafunga njia haraka sana, wapo sharp sana na wanashinda mipambanio yao mengi.

Manqoba ni surprise kuanza na Twin Strikers ya Peter Shalulile na Ibrahima Toure.

1. Kuwa wanufaika wa idadi kwenye eneo la mwisho la kushambulia.
2. Kuwa na mshambuliaji mmoja wa ziada kwenye kila tukio ikitokea mshambuliaji wao mmoja anawania Mpira, tazama bao la Toure lilivyokuwa.

28/08/2026

🚨Hawa Yanga wanatuharibia ligi, waende hata south Africa huko

28/08/2026

HT : Tanzania NBC 🇹🇿

Young Africans 🇹🇿 2-0 Pamba Jiji

Toure ⚽
Max ⚽

27/08/2026

🚨💣📝Sio kwamba Coastal Union walikuwa imara, bali Simba SC wenyewe wamefanya mchezo kuwa mgumu kwa kukosa utulivu langoni.

Takwimu zinazungumza zenyewe:
• Ball Possession: Simba 76% - 24% Coastal
• Kona: 15 - 0
• Mashuti Lengo: 8 - 0 (Mashuti ya jumla: 15 - 2)

Beki (CB) Ismael Touré, ameonesha kiwango cha juu. Ameilinda timu, amepandisha mashambulizi, ametengeneza nafasi za kufunga (moja ile kwa Doumbia) na akatupia goli.

MOTM Performance, Nathaniel Chilambo: Alicheza k**a Inverted Left Back kwa ufasaha mkubwa, akaisaidia safu ya kiungo na kumpa nafasi Neo Maema kufanya yake.

• Ibrahim Doumbia, Anajua mpira, anakosa tu bahati ya kufunga kwa sasa. (Leo kaonesha akipewa muda ata-click tu).

Mbali na kosakosa za Doumbia, Chilambo na Touré kuuwasha sana leo, Ancet Oura na Elie Mpanzu sio wa kuanzia nje kwenye hizo squad rotation, Ismail Mgunda anakitu akipata game time.

27/08/2026

Nilisema Toka Mchezo Uliopita Hapa Simba Sc Watabidi Wasubiri Sana Mpaka Atakapojipata Sio Akimweka Benchi Oura Viwango Vyao Ni Mbingu Na Ardhi Yaani Wamepishana Mbali Sana.

Ilikuwa Ni Bora Wangemvumilia Hata Chassambi Huenda Wangekula Matunda Yake Msimu Ila Hapa Simba Sc Wanatakiwa Kuwa Na Subira Sana Mpaka Atakapojipata Kwenye Ubora Wake, Ila Kwa Sasa Kwangu Ni Mchezaji Wa Kawaida Sana Hajafika Hata Level Za Denis Nkane.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Website

Address

Dar Es Salaam