29/08/2026
Mashabiki wengi wa soka Tanzania, hasa wananchi Yanga SC, wanadai kwanini nyota mwenye namba yake ya kipekee kabisa achezi Aziz Ki. Ukweli upo wazi juu ya nyota huyo baada ya taarifa kutoka ndani ya klabu kuwa Aziz Ki ni mchezaji maalumu kabisa kwa mechi chache ambazo wamepanga wao kocha mkuu MANQOBA.
Napenda wachezaji wenye kasi sana, pia napenda mchezaji mwenye ubunifu mkubwa sana ndio maana unaona Aziz Ki kuingia ni kazi kwa maana ana kiwango, lakini kasi ya mchezo wa mara kwa mara hawezi. Hivyo bado tunatafuta ni mechi gani anaweza kushiriki vizuri bila tatizo, na niliwambia kabisa kwamba lazima atacheza kwa kasi ninayoitaka mimi, kwa sababu k**a mchezaji ana ubora hawezi kukosa kasi ya mchezo. Kwa hiyo iwe isiwe, lazima atakuwa na kasi ninayoitaka mimi.
Pia Aziz Ki kwenye uwanja wa mazoezi anafanya vizuri sana. Hatutaki kumvuruga nyota wetu kwa mechi za chini, mechi za ugenini tutampa asilimia kubwa, kwani ndio mechi ambazo zina asilimia kubwa za kutoshinda, pamoja na hilo kuwa na kasi ya kawaida.
29/08/2026
Gwiji wa mabao duniani Cristiano Ronaldo, baada ya kuipa ushindi wa bao 2-1 Al Taawoun katika mchezo wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia. Kwa upande wa mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or, mwenye umri wa miaka 41, sasa amebakiza mabao 22 tu ili kuvunja rekodi ya mabao 1000. Upande wa mchezaji ameendelea kufanya makubwa k**a mmoja wa mastaa ambao wataweka historia pana ya maisha ya soka kwa miaka ya hivi karibuni.
29/08/2026
Kiwango cha Selemani Mwalimu kinaanza kumshawishi Manqoba Mngqithi, je, sasa ni wakati wake wa kuanza kwenye kikosi cha kwanza? .
29/08/2026
Safari ya kocha mkuu wa Manchester City, Enzo Maresca, imeanza vizuri baada ya kupata matokeo mazuri katika Premier League 2026/27.
Maresca ameiongoza Manchester City kupata ushindi wa pili mfululizo kwenye ligi, baada ya kuwapa kichapo cha 4-1 Crystal Palace katika mchezo uliochezwa ugenini.
Ushindi huo umeifanya City kuanza vyema safari yake mpya chini ya Maresca. đź‘€
28/08/2026
Nyota wa Yanga SC, Cheikh Toure, amevunja ukimya baada ya mchezo wao kumalizika kwa 2-0 dhidi ya Pamba SC. Akisema kati ya mechi zote nilizo cheza tangu msimu kuanza nikiwa ndani ya klabu yangu mpya ni pamoja na huu mchezo umekuwa mgumu sana. Tumekosa magoli mengi sana, pia walijilinda sana kuondoa mitego yetu kwa namna ya kipekee kabisa. Tunaweza kusema wamefanya kazi nzuri, lakini wao hawakuwa na bahati sana ya kushinda mechi hii ya leo.
Nimefurahi kila mchezo tunao cheza tunashinda, nazidi kuipenda Yanga na daima nitafanya makubwa sana msimu huu. Nipende kusema kwamba mwalimu alituelekeza kuondoa presha. Ni moja wapo ya kutatua makosa ndani ya uwanjani, pia tulifanya k**a anavyopenda moja kwa moja tukapata matokeo mazuri.
28/08/2026
HT || Yanga SC – 2
|| Pamba SC – 0
28/08/2026
|| yanga SC - 2
|| Pamba SC - 0
TOUREO. .
28/08/2026
Wenye king’amuzi wametoa sare ya bao 2-2 dhidi ya Geita Gold FC. Upande wa kocha mkuu Florent Ibengé amesema kati ya mechi ngumu ambazo nilitegemea ni pamoja na hii. Imani yangu ilikuwa ni kubeba goli 3 na kuendelea, ila sasa kulingana na wapinzani wetu walikuja vizuri, hatuna budi kupokea matokeo kwa sababu ni mojawapo ya mchezo. Tunajiandaa na mchezo unaofuata ili kutimiza lengo la timu yetu msimu huu. Kwa upande wangu wachezaji wangu walikuwa sawa.
28/08/2026
Baada ya taarifa kuwafikia mashabiki wa klabu ya Simba SC kuwa mlinzi wa kushoto wa Simba SC Nickson Kibabage kupata majeraha, kupitia ukurasa wa mwanahabari na usajili Tanzania FELIX JASON, amesema kwamba Kibabage anaweza kubaki nje ya uwanja kwa siku zisizopungua 31. Sawa na mwezi mmoja mzima. Kibabage amekuwa akisumbuliwa na tatizo la misuli pamoja na eneo la goti, hivyo inakuwa vigumu kuweza kupona majeraha yake.
Bado kuna pengo ndani ya benchi la ufundi kwa upande wa kocha Steve Barker. Amefanya kazi ngumu kuhakikisha kuwa eneo hilo linalindwa k**a mlinzi huyo alivyokuwa akilinda, angali hajapatwa na majeraha.