Eva Baltazar Gidabuday

Eva Baltazar Gidabuday

Share

Private page

21/08/2026

Unajiandaa na kikapu chako kwenda kuvuna mahali haujawahi kuotesha mbegu wala kupalilia, huo ni ujambazi k**a ujambazi mwingine tu.

Haujawahi kuonekana kwenye picha ya pamoja na unaowaita ni ndugu zako, kwa kuwa haujawahi kuona umuhimu wa kuwa karibu nao, Leo unapata nguvu wapi ya kulazimisha wakuone ni mwenzao? Kutafuta fursa kusikufanye ukose haya na mipaka.

Kuna maisha ukichagua kuyaishi wakati ulipojiona juu, ukawaona wengine chini, Leo unapotumia nguvu kubwa watu hao wakutambie, unasahau kwamba makovu hayawezi kuponywa kwa kuwa Sasa anayeumia ni wewe. Ulifaa kuwekeza katika kujiandalia kesho itakayokuthamini.

Wazee wanasema ardhi inaandika mambo yetu, yawe mazuri kwa mabaya. Jiulize kwako wewe ni kipi kimeandikwa na ardhi iliyokusikia kwa miaka mingi?

Unatamani kutoa Ushuhuda wa ushindi kwa matamanio maovu unayowaza Kila siku, ila matendo yako ya kale yanakuangusha sana, na bado ya Sasa yatakuangusha uendako Ikiwa hautaachana na kupandikiza mbegu mbaya kwa watu uliowatesa kwa miaka.

Likikugusa ndiwe!

01/07/2026

Nani ataelewesha mtu huku jamani? Msimamizi wa mirathi haimaanishi kuwa amemilikishwa mali ya mhusika. Na hawezi kuwa aliyewahi kuwa kwenye migogoro naye!

01/07/2026

Nani ataelewesha mtu huku jamani? Msimamizi wa mirathi haimaanishi amemilikishwa mali ya mhusika? Na hata hawezi kuwa aliyewahi kuwa kwenye migogoro naye.

24/06/2026

Katika mambo ya ajabu maskio kupata kusikia ni pamoja na mtu kuagizwa kuhakikisha anamshusha mwingine ili yeye apande juu! Au kumlaza mwingine njaa ili yeye ashibe, au adui amwombee njaa apate kumshinda. Hii ni mitazamo hasi ya watu waliojiaminisha kwamba huu ulimwengu ni wao na wao wameuumba. Vinginevyo, mengine majubu yatakuja yenyewe kwa wale ambao tegemeo lao linatoka juu
Cha kushangaza huko kumlaza njaa ni pamoja na kuunda mizengwe hatarishi inayoaminiwa na wenye upeo unaofanana na wa kwake. Kwani walio na upeo wao mkubwa hupima mambo na kudadisi uhalisia. Jioni njema lakini, ila huku pia nauza vitu vingi sana k**a mboga mboga, kuku, nyanya, kunde n.k. siyo masendeu pekee. Na njaa silali.

23/06/2026

Umaana unaouona kwako uko kichwani mwako mwenyewe, wengine wala hawana habari nawe. Kila mmoja yuko busy kufanya yale yamfurahishayo uwe unavutiwanayo au la!

12/05/2026

With Sierre-Zinal – I just made it onto their weekly engagement list by being one of their top engagers 🎉

07/05/2026

Mahaba yana pofusha wengi!
Au Ubaguzi unasahaulisha wengi!
Kuna mtu mahali amezoea kupita na kila aina ubaya kwa wengine bila kujulikana, ila siku ambayo mambo yamegeuka hutafuta huruma kwa wasiokuwepo au wasiojua mwanzo wa mambo k**a wapambe wake.

Mfano umetendwa jambo k**a miaka 30, au 20, au 10 iliyopita, wewe mwenzangu ambaye haukuwepo katika picha unanoa mdomo ili iweje, kwamba unajua kuzungumza sana au..?

Kuna watu ni mashetani sirini, ila kwenye macho ya wengi ni watakatifu, ninapowafungia nje ya maisha yangu, uliza kwanza kabla ya kuanza kunoa mdomo.

Fikiri kabla ya kutenda au tafakari Kila mara kabla ya kurukia vitu. Tuchukulie mfano, haujawahi kuonekana umuhimu wa kuunganisha watu k**a familia, badala yake juhudi zilifanyika za kuhakikisha hakuna maelewano, kujenga umoja na wala kuheshimu chaguzi za wenzako. Leo unapata nguvu wapi ya kuamini yale uliyoyapiga vita ni sehemu ya maisha yako sasa?

Mfano mwingine, una Mtoto ambaye alifika nyumbani kwako mara mbili tu katika maisha yake, akiwa na miaka miwili na nusu (hakukubalika) na hakuna aliyemfuatilia baada ya hapo, hadi alipofika miaka 21 kwa mashinikizo ilitakikana aje, kwakuwa sasa tumetaka sisi na baba yake ana kazi, ila mama alipokuwa na kazi na alipojaribu kumleta, mlihakikisha hawaelewani na tunamzuia aje kwa kuwa siyo nyie mmetaka, na hata akija atakwenda kwa wazazi wa mama. Bila kujali maumivu ya Mtoto, ubabe ulifanyika akarudia njiani.

Kweli kwa mara ya pili alifika kunakodhaniwa ni kwao akiwa mtu mzima kwa mashinikizo na ubabe. Ila kwa kifupi, mara ya tatu angekuja katika mazingira ya majonzi tena kwa heka heka za wasiojua mbele wala nyuma, NAMI NIMEKATAA.

K**a hakuna kuheshimu nafasi za wazazi waliopambana kwa miaka zaidi ya 30 ya uvunjanji wa haki ya Kila mtu kujichagulia ampendaye basi na asije. Haukuwepo kwenye maisha yetu, lipi unalojua anyway, zaidi ya kukaa kimya? Ulifanya nini wakati ilipotakiwa jambo lifanyike ili kunusuru utengano wa muda mrefu na mwanafamilia mwenzenu?

05/05/2026

HUWEZI KUPATA UKWELI KUTOKA KWENYE MIDOMO ILIYOZOEA KUSEMA UONGO.

Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility in Arusha?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Address

Maroroni Road
Arusha
13178