03/08/2026
What goes around comes around.
Habari za michezo kutoka simba sc tanzania. habari za michezo kutoka simba sc tanzania
03/08/2026
What goes around comes around.
02/08/2026
Hiki hapa kikosi cha Simba SC msimu huu. Kwenye kikosi hiki ungeongeza nani au ungemtoa nani?
02/08/2026
Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amesema wachezaji wapya walioungana na timu hiyo wanahitaji muda ili kuzoea mazingira mapya na mfumo wa uchezaji wa klabu.
Barker amesema changamoto kubwa kwa baadhi ya wachezaji wapya ni kipindi cha mwanzo cha kuingia kambini, ambapo wanahitaji kuelewana na mwalimu pamoja na kuzoea mbinu mpya.
Amesema anaamini baada ya muda wachezaji hao wataonyesha uwezo wao mkubwa baada ya kuingia vizuri kwenye mfumo wa klabu.
Akitolea mfano Ibrahim Jabaar, Barker amesema ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa anayehitaji mwongozo sahihi ili kuonyesha kiwango chake halisi.
“Tuko naye sawa kwa sasa, atakuja vizuri kadri atakavyozidi kuzoea mfumo,” amesema Barker
01/08/2026
Winga hatari wa kimataifa kutoka Burundi, Jean Claude Girumugisha, anaripotiwa kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Simba SC.
Girumugisha anatajwa kuwa mchezaji mwenye kasi, uwezo mkubwa wa kupiga chenga na kutengeneza nafasi za mabao, akiwa ameonyesha kiwango bora akiwa na Al Hilal Omdurman na timu ya taifa ya Burundi.
01/08/2026
Umeona U*i mpya wa MNYAMA? Tuambie jezi hizi Kali kutoka kwa Jayrutty.
01/08/2026
DAVID DUCHU “Kameta” ameonyesha kwa nini anaendelea kuwa mmoja wa wachezaji wanaotegemewa ndani ya kikosi cha SIMBA SPORTS CLUB. Utulivu wake akiwa na mpira, maamuzi sahihi, na uwezo wa kuisoma mechi vilionekana wazi Leo dhidi ya SINGIDA BLACK STARS....
•Assist aliyotoa leo Kwa ELIE MPANZU KIBISAWALA si bahati, ni matokeo ya ubora, maono ya mchezo, na uwezo wa kutengeneza nafasi kwa wakati sahihi....
•DAVID DUCHU KAMETA anaendelea kutuma ujumbe kwamba yupo tayari kwa changamoto za msimu mpya.
01/08/2026
Ibraheem Tarafa Jabaar ~ Ukimpa mali una uhakika imefika sehemu salama. Una uwezo wa kumuachia kichumba ukatafuta space kwengine.
Ibraheem Jabaar ana jicho la kupiga pasi vibaya mno. Anatulia na mali mguuni. Uwezo wa kuvunja lines za wapinzani.
Ibraheem Jabaar ana uwezo wa kuendesha mita kadhaa kwa uhakika na ufanisi.
31/07/2026
Msimu uliopita alimaliza na mchango wa magoli 18 ya Ligi kuu, magoli 8 na assists 10.
Leo amerejea na goli, kutoka kua winga tishio hadi mshambuliaji wakati hatari
Steve Barker ame m'badilisha sana Elie Mpanzu, bila ya shaka Simba wataendelea kunufaika na numbers za Mpanzu next season.
Good enough, Washambuliaji wao wote wawili wameingia kambani, Dumbia na Mpanzu.
30/07/2026
Libasse Gueye ni moja ya wachezaji bora kwenye kikosi cha Steve Berker jamaa ana deliver kwenye kila mchezo tena kwa ubora mkubwa sana !…
Msimu uliopita jamaa aliuwasha sana kwenye CECAFA KAGAME CUP ameendelea alipoishia sina shaka na ubora wa Gueye.
30/07/2026
Ibraheem Jabaar naambiwa Simba SC wamepata hii mashine inacheza Kiungo Mkabaji, Kiungo Mshambuliaji na Winga sababu ya uwezo mkubwa wa kutumia mguu wa kushoto.
Silaha ya Siri ya Steven Barker ni hii, kipaji kikubwa ndiyo mana kocha huyo kamvuta Simba SC.
Basi watu wasijimalize, Simba ina silaha za hatari kuliko kawaida.